LHRC yauliza maswali 11 kwa jeshi la polisi sakata la binti kubakwa na kulawitiwa

LHRC yauliza maswali 11 kwa jeshi la polisi sakata la binti kubakwa na kulawitiwa

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa zinazomsambaa kuhusu mwenendo wa tukio la kikatili lililotokea dhidi ya binti mmoja mkazi wa Dar es Salaam.

Tukio hili lilirekodiwa katika picha mjongeo zilizomsambaa katika mitandao mbalimbali zilizoonyesha binti huyo akibakwa, kulawitiwa na kushurutishwa kuomba msamaha kwa “afande”.

Soma Pia:
Pamoja na kusikitishwa, LHRC inajiuliza maswali mengi kuhusu taarifa za jeshi la polisi tangu kuibuka kwa tukio hilo.

i. Swali la kwanza taarifa zipi ni sahihi kutoka jeshi la polisi makao makuu, wizara ya mambo ya ndani au makamanda wa polisi wa mikoa wa Dar es Salaam na Dodoma.

ii. Swali la pili je watuhumiwa ni maafisa wa jeshi lipi?

iii. Swali la tatu watuhumiwa katika tukio hilo walikuwa watano, je huyo mwingine ni nani na yuko wapi?

iv. Swali la nne binti alilazimishwa kumuomba msamaha “afande”, je Afande ni nani?

v. Swali ya tano, je mhanga yupo salama katika mikono ya wanaomhukumu kuwa ni kama alikuwa anajiuza?

vi. Swali la sita, je binti huyo kuwa katika mikono ya polisi hakutaathiri upatikanaji wa haki na ushahidi?
 
Back
Top Bottom