kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Lieberman atoa wito wa kurejeshwa kwa sera ya mauaji ya kigaidi Ukanda wa Gaza
Jun 20, 2023 07:36 UTC
Waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amelitaka jeshi la utawala huo kutekeleza tena sera ya kuwaua kigaidi makamanda wa harakati za mapambano ya ukombozii ya Palestina katika Ukanda wa Gaza na kutekeleza operesheni kubwa za kijeshi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Shirika la habari la Sputnik limeripoti kuwa, Avigdor Lieberman, waziri wa zamani wa vita wa Israel, amesema katika mkutano wa kikundi cha wabunge wa chama chake cha Yisrael Beiteinu (Israeli Nyumba Yetu) kwamba: "Ni lazima turudi kwenye mauaji ya kigaidi dhidi ya makamanda wa harakati ya Hamas huko Gaza."
Lieberman ameongeza kuwa: Haiwezekani kwa viongozi wa Hamas kuchochea moto katika Ukingo wa Magharibi na kisha kuwa na kinga huko Gaza.
Lieberman pia amelitaka jeshi la Israel kuanza operesheni kubwa na ya kina ya kijeshi katika Ukingo wa Magharibi.
Matamshi hayo yamefuatia mapigano makali yaliyotokea jana baada ya wanajeshi wa Israel kushambuliia mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi na kukabiliwa na upinzani mkali wa wanamapambano wa Palestina ambapo waisrael wanne waliangamizwa katika makabiliano hayo.
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimelazimika kukiri kwamba mapambano yaliyotokea jana Jumatatu kwenye mji wa Jenin huko Palestina yalikuwa tata na ya kipekee kutoka kwa wanamapambano wa Palestina.