Licha ya baadhi ya barabara za Dar kufungwa, TRC yasema ratiba ya Treni zinaendelea kama ilivyopangwa

Licha ya baadhi ya barabara za Dar kufungwa, TRC yasema ratiba ya Treni zinaendelea kama ilivyopangwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-01-27 at 08.03.27_0869cc82.jpg

TAARIFA KWA UMMA

RATIBA ZA TRENI KUFUATIA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM JANUARI 27-28, 2025


Dar es Salaam, Januari 26, 2025.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapenda kuuarifu umma kuwa ratiba ya safari za treni kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, zitaendelea na ratiba yake kama ilivyopangwa licha ya baadhi ya barabara muhimu kufungwa kufuatia mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika, unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Januari 27-28, 2025.

Shirika linawaomba abiria husika kupanga vizuri namna ya kufika mapema stesheni wanazotarajia kupandia treni hususani kituo cha Magufuli jijini Dar es Salaam na cha Samia jijini Dodoma, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Katika hatua nyingine kufuatia kufungwa kwa barabara tajwa na Jeshi la Polisi Tanzania, TRC inapenda kuuarifu umma na abiria wanaotarajia kusafiri kati ya Dar es Salaaam na Dodoma Januari 27 na 28, 2025 kuwa treni zote ikiwemo ya Express, zitasimama kupakia na kushusha abiria katika kituo cha Pugu na kwamba utaratibu huu utahusu pia abiria wa kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Aidha, Shirika linatanguliza shukrani kuelekea kipindi hiki.
Fredy Mwanjala
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano
 
Back
Top Bottom