licha ya kubadili dini kuwa muislam"atamani kuokoka....Natamani kumrudia yesu kristo"...Aunt Ezekiel

licha ya kubadili dini kuwa muislam"atamani kuokoka....Natamani kumrudia yesu kristo"...Aunt Ezekiel

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Licha ya kubadili dini na kuwa muislam kisha kupewa jina la Rahma, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amesema sasa anatamani kurejea ‘ulokoleni’ na kumrudia Yesu kwa kuokoka.

Akizungumza na gpl hivi karibuni nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, msanii huyo ambaye alibadili dini kutoka ukristo na kuwa muislam baada ya kuolewa na mumewe, Sunday Demonte alisema anajisikia kurudi kwenye ukristo kwa madai ya kumtumikia Mungu kikamilifu.


Akionesha msisitizo katika hilo, Aunt alisema moyo wake umekuwa ukitamani kusikiliza mafundisho na mahubiri ya kikristo pamoja na kusikiliza nyimbo mbalimbali za injili.





Wakizungumzia mawazo ya kuokoka ya msanii huyo, baadhi ya mashabiki wake walimshangaa huku wakionesha wasiwasi wake juu ya kusilimu na kudai huenda kubadili kwake dini ilikuwa danganya toto.


“Huyu si aseme tu uislam umemshinda? Kasilimu juzijuzi tu hapa na kudai ameanza kusali msikitini, leo anatuambia anatamani kuokoka, hawa mastaa wetu wanamchezea sana Mungu,” alisema Rahma wa Kinondoni jijini Dar.
 
Anatamani kurudi Kwenye ukiristo na kumtumikia Mungu kikamilifu....Dini nyingne Mungu hawana mkamilifu?
 
Si aseme kua alimfata iyobo,sasa penzi limechuja ndio anakumbuka mahubiri!
 
Eti mtu kabadili dini na kuwa Muislam kisha akaolewa na Sunday. Hivi jamani sunday ni muislam au Jumapili akakatishwa jina na kuitwa Juma[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Sattelite c1175b
 
Back
Top Bottom