Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Mwaka huu tutavunja record nyingine duniani FISADI awe raisi ?Tanzania my country akitaka aupate uraisi namshauri EL awe muwazi atuaambie hadharani deal la Richmond alipiga na nani huko CCM hiko ndo kizingiti kinachomwangamiza
Ndiyo
 
Thamani yako imeporomoka kama ya Lowassa. Ndo tatizo la kuwa bendera kufuata upepo. Vijana mnaoonekana kuwa na uelewa mkubwa mnajidhalilisha kwa kutumika kama toilet paper. Sasa mnavuna mlichopanda...

hapa hata sijakuelewa mkuu unaweza kufafanua sijaona kosa la pascal ktk huu uzi?
 
Na humu pia ukipita na kusoma comments ndio utajua kwamba matatizo yetu hayapo kwa wapigiwa kura tu, bali yameenda mbali hadi kwa wapiga kura wenyewe 😀😀😀
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Paskali
.Baada ya kuyasoma hayo, nimetambua inawezekana ule mchezo wa kulikata jina la Lowassa uliandaliwa vizuri na JK, na kwa kujua kuwa supporters wa Lowassa wangekasirika baada ya pale, akamuacha Membe asogee hatua moja zaidi mbele kwenye ule mchakato wa uchujaji, ili hasira ziwapande vizuri wale wajumbe wa Lowassa.
Ni kweli, it's true.
P
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Mtoa habari wangu amesema kamati ya maadili ya CCM, itamchinja Lowassa kwa kumpa alama za chini kabisa kuliko wagombea wengine wote ili kuirahisishia kazi Kamati Kuu ambayo inatakiwa lazima itoke na majina matano kuyaingiza Halmashauri Kuu, ambapo mgombea rasmi wa CCM ameishachaguliwa, hivyo hili zoezi la kutangaza nia na kuomba uteuzi ni kwa lengo la kukamilisha tuu taratibu.

Sifa za Wagombea Watano watakao pitishwa na CC kuingia tano bora ya NEC ni hawa...
1. Mgombea mmoja mwanamke
2. Mgombea mmoja Muislamu
3. Mgombea mmoja kutoka Zanzibar
4. Mmoja wa Mawaziri Wakuu ambaye ameandaliwa kama kingio la huyo aliyeshachaguliwa!
5. Mgombea aliyeshachaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

NEC itawapigia kura, ambapo mgombea tajwa, ataongoza kwa kura nyingi atasindikizwa na mgombea mmoja mmoja Mwanamke kutoka Zanzibar na Yule Waziri Mkuu Kingio, ambapo kwenye Mkutano Mkuu, wale wagombea wasindikizaji wawili watajitoa hivyo mgombea huyo kupaswa bila kupingwa kisha Wajumbe wa Mkutano Mkuu watapiga kura zuga tuu na matokeo, atakuwa amechaguliwa kwa asilimia 99%, na hiyo asilimia 1% itakayo mkataa ni kuzungia tuu kuwa CCM demokrasia!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, kwa kumchinjia rasmi baharini kwa kumpa maksi za chini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakabali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo wa uongozi, wa kulibadili taifa hili kuwa nchi ya neema, na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingi huko nyuma na ikabaki salama, hivyo kama ni kweli hiki ndicho walichopanga kukifanya this time!, hakitabaki salama!. Yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Paskali
Mayalla unajua Mwangonda ndo alimmaliza lowassa hadi Mkapa akapata wazo kwamba akatwe? Alikuwa kijana planted na Mkapa tokea 2017 japo mkapa na kikwete walikuwa hawaelewani, Na kikwete alianza kumuheshimu Mkapa tarehe 17/10/2010 sababu ntaziweka kwenye Uzi nao andaa
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Mtoa habari wangu amesema kamati ya maadili ya CCM, itamchinja Lowassa kwa kumpa alama za chini kabisa kuliko wagombea wengine wote ili kuirahisishia kazi Kamati Kuu ambayo inatakiwa lazima itoke na majina matano kuyaingiza Halmashauri Kuu, ambapo mgombea rasmi wa CCM ameishachaguliwa, hivyo hili zoezi la kutangaza nia na kuomba uteuzi ni kwa lengo la kukamilisha tuu taratibu.

Paskali

Maadam sasa Lowassa ametangulia, huu ni wakati kwa wale wote waliomhujumu, wamuombe msamaha hata wa kimoyo moyo, mtu hata akiwa kifoni, huko ni kwenye ulimwengu wa roho, anaona yote na anasikia yote, hivyo akiombwa msamaha hata wa kimoyo moyo anasamehe.

Naendelea na My Tribute to this fallen hero, Mwamba wa Kaskazini, kwa kujikumbusha baadhi ya mabandiko yangu kumhusu shujaa huyu mpaka siku atakapo pumzishwa kwenye makao yake ya milele, let's celebrate the life and the times of Edward Lowassa.

RIP Shujaa Laigwanani Comred Edward Ngoyai Ole Lowassa,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu, imani umeilinda.
Bwana alileta
Bwana ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Mwaka huu tutavunja record nyingine duniani FISADI awe raisi ?Tanzania my country akitaka aupate uraisi namshauri EL awe muwazi atuaambie hadharani deal la Richmond alipiga na nani huko CCM hiko ndo kizingiti kinachomwangamiza
Nam
 
Back
Top Bottom