Licha ya mafuta kushuka bei, LATRA yasema hakuna mpango wa kushusha nauli

Licha ya mafuta kushuka bei, LATRA yasema hakuna mpango wa kushusha nauli

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baada ya bei ya mafuta ya Petroli, Dizeli kushuka, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imesema hawana mpango wa kushusha nauli kwa sababu uendeshwaji wa vyombo vya usafiri hautegemei gharama za mafuta pekee.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema gharama za mafuta zinategemewa kwa asilimia 38 tu, na asilimia 62 ni gharama nyingine.

Chanzo: Tanzania Daima
 
Watz tuache lalamika sana, tufanye kazi
 
Baada ya bei ya mafuta ya Petroli, Dizeli kushuka, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imesema hawana mpango wa kushusha nauli kwa sababu uendeshwaji wa vyombo vya usafiri hautegemei gharama za mafuta pekee...
Lakini nauli zilipanda kwa sababu ya mafuta.
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Hawa LATRA naona walishakula pesa za Wafanya biashara naona wanatafuta sababu za kuzirudisha maana hakuna namna
 
Sipingani na Uamuzi wa LATRA kutokushusha nauli, lakini sababu aliyotoa huyo Mkurugenzi naweza kusema haijakaa kisomi.

Maana wakati wa Upandishaji wa Nauli, sababu kuu ya LATRA huwa ni Gharama za mafuta..
 
Kutegeme hilo punguzo kushusha nauli itakuwa kujidanganya, hilo linaenda kuongeza faida kidogo kwa wasafirishaji baasi...........kama kuna bilioni mia moja imelipwa mahala kwamba itapunguza gharama za usafiri na usafirishaji basi tumepigwa.
 
Sipingani na Uamuzi wa LATRA kutokushusha nauli, lakini sababu aliyotoa huyo Mkurugenzi naweza kusema haijakaa kisomi.

Maana wakati wa Upandishaji wa Nauli, sababu kuu ya LATRA huwa ni Gharama za mafuta..
Nchi ina wahuni sana hii
 
Ukiwa Tz kitu inaweza panda na kushuka ni mashetani hivi vingine havishukagi vikishapanda
 
Anaongea ivyo kwakuwa serikali inamuhudumia vitu kama gari ya ofisi mafuta anawekewa ,mshahara na posho yake juu.....hawezi ona uchungu kwa wananchi
 
Back
Top Bottom