Hakuna anayejali
JF-Expert Member
- Jun 3, 2023
- 418
- 526
Mimi siwaiti madereva bali waendesha pikipiki za biashara wanapitia changamoto za uonevu toka kwa mabosi wao na jeshi la polisi.
Niliwahi kuelezwa kisa kimoja cha boda aliyekuwa anaendesha boda ya mkataba. Ishu ilikuwa hivi: huyu boda anaendesha boda ya tati kwa bosi mmoja, sasa akakodiwa mahala huko akashambuliwa na washambuliaji wakapora pikipiki.
Sasa kijana alipomjulisha bosi baada ya tukio, bosi akamtia ndani bila kijana kupata haki ya matibabu, na akazuia dhamana kwa hoja kuwa kijana atakuwa amepanga mpango wa kumuibia pikipiki. Polisi nao wakakubali kubaka haki ya dhamana ya mtuhumiwa.
Mama mwenye mtoto alijitahidi kudhamini akakataliwa na mwisho bosi akamtafuta mama wa kijana na kumwambia waende kwa mwanasheria wakaandikishane lini atalipa boda.
Hapa ndipo penye hoja: Kwanini kijana anyimwe haki ya tiba, kwanini anyimwe haki ya dhamana? Hao polisi na bosi wanaosema kijana hajapasuka ila kavimba tu, je, wao ni wataalam wa afya?
Je, ikiwa bosi ndiye alipanga njama ili kupora na hatimaye kumlimbikizia deni? Hayo ni mtazamo wangu, je ninyi mnaonaje?