Licha ya umeme kufika kila mji na kila kijiji lakini wateja wenye umeme ni mln 5.2 tu out of 65mln people. Kuna umaskini mkubwa sana nchini

Takwimu za mambo ya maendeleo Tanzania ni mchanganyiko wa uongo na porojo za kisiasa.
 
Labda sijaelewa...


Kila nyumba inaishi kwa wastani wa watu watano...

Au ilitakiwa kila mtu awe na umeme wake..?
kusema tupo watu mil 60
Huku ukilalama kuwa kuna wateja mil 5 tu nadhani si sahihi.
 
Hao wapangaji ujue wana familia zao pia na wategemezi ambao hufaidi hiyo huduma ya umeme
Unafahamu pia wateja wa umeme ni pamoja na majengo ya biashara kama mashine za kusaga, kukamua alizeti, stoo, hospitali, ofisi, shule n.k ambayo sio makazi ya watu kuishi?
 
Unafahamu pia wateja ni pamoja na majengo ya biashara kama mashine za kusaga, kukamua alizeti, stoo, hospitali,
ofisi, shule n.k ambayo sio makazi ya watu kuishi?
Mleta ameongelea watu hajaongelea majengo lakini hata.wewe umepotoka shule za bweni watoto hufaidi huduma ya umeme na hospital kuna nyumba za madaktari hupata huduma ya umeme,magerezani pia hufaidi hiyo huduma kambi za jeshi pia

Hiyo idadi kataja sio kweli hajui kuchakata takwimu
 
Ishu ya umeme hatuangalii idadi ya watu Bali tunaangalia makazi
 
Haishangazi Bali inasikitisha
Ina huzunisha,na ndio sababu tunasema mitanobtena kwa yule bibi hapannnnnnna!
Mfano , Kijiji cha Itumbi,wilaya ya chunya ,Kijiji kina umeme,ila waliobahatika kupata huo umeme ni wachache sana sana
 
Ni sawa kabisa na hakuna shida.
We ulitegemea kila mtu ana mji wake peke yake hivyo anatakiwa awe na umeme wake siyo?
Kuna nyumba zinahold 3-30 people na hata zaidi hivyo ukipiga ratio ni watu wachache sana hawana umeme bongo hii.
 
Duuh na tunataka tuuze umeme nje kumbe hata sisi wenyew hatujafikia robo ya wananchi wetu wanaotumia umeme. Najiuliza km ikifikia nusu ya idadi yetu km umeme utatutosheleza.🤔🤔
Shida sio uhaba wa umeme Bali uwezo wa watu kununua na kulinganisha huo umeme kwenye Makazi na Biashara zao.
 
Au Kwa namna nyingine kati ya Jumala ya Majengo Milioni 14.3 yenye umeme ni majengo 5.2mln sawa na asilimia 37% tuu.
 
Najibia Heading tu.
Huduma ya umeme inakwenda kwa mtu mmojammoja au kwa nyumba? Maana naona umetumia takwimu ya idadi ya watu katika kupata huduma ya umeme badala ya nyumba/majengo.
 
Ni sawa kabisa na hakuna shida.
We ulitegemea kila mtu ana mji wake peke yake hivyo anatakiwa awe na umeme wake siyo?
Kuna nyumba zinahold 3-30 people na hata zaidi hivyo ukipiga ratio ni watu wachache sana hawana umeme bongo hii.
Ndio,inatakiwa Kila Mji uwe na umeme hivyo ni sawa na Kila Mtanzania awe na meme

Unapomsema ni sawa unaonekana ni mjinga sana,Nchi za wenzetu hapa hapa Africa wako 90% and above.
 
Una uhakika tuko na KAYA/MAJENGO 14.3M? Sababu bila hivyo hoja yako ya idadi ya wenye umeme (5.2M) vs idadi ya watanzania (65M) unasuggest kwamba ili mission iwe imekamilika basi kila raia aonganishwe na umeme which is impossible.
Umesoma mpaka la ngapi mkuu? Hata kama kukiwa na kaya milion 5 zenye watu milion 65 bado ni kiashiria kikubwa cha umaskini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…