Lifahamu zao la Macadamia (Karanga Pori) na jinsi ya kulilima

Lifahamu zao la Macadamia (Karanga Pori) na jinsi ya kulilima

Najaribu mkuu kama macadamia yanakubali Egypt sidhani kama Dar yatagoma nafanya jaribio...miche nimeagiza kwa Lily Tony yumo humu JF mtafute ana miche ya kila aina.
Egypt ni Mediterranean na Dar ni 100 tropiki. Tabia au sifa ya Mediterranean ni kukubali Matunda,Egypt ipo katika ukanda wa hivi na South pia,japo sio part ya Egypt yote ni Mediterranean.
 
Jamaa alitaka kutudanganya. Ni kweli ni ngumu kuota lkn si mwaka mzima. Wengine tumeotesha kitalu na zimeota.
Ukiokota fresh kabisa chini ya mti kama hazijakaa sana ni mwezi na nusu zinaota ila zikikauka sana ni wastani wa miezi mitatu. Hii itakulazimu uziloweke kwa walau siku 3
 
Uthubutu ni nzuri sana nimependa.
Ila passion ndogo au kakara mwitu asili yake ni maeneo ya baridi kama mgeta,soni na Njombe,unaweza kutupa mrejesho kwa jaribio na uthubutu.
Yameanza kuviringa sijajua kwenye kuzaa nitaleta mrejesho eneo ni Bunju Beach
 
Yameanza kuviringa sijajua kwenye kuzaa nitaleta mrejesho eneo ni Bunju Beach
Soon mimi nitapanda ukanda wa pwani na nalima kibiashara!!kwa tabia ya hali ya hewa ya macademia hili zao litastawi nahitaji wenye miche tafadhali au aje inbox tuhamue
 
View attachment 1546458
View attachment 1546456

macadamia%252520nuts.jpg
Karanga pori,asili yake ni Australia.Mti wa karanga pori unatokana na jamii ya mimea ya proteaceae,aina zote zinalika ambayo mimea yote miwili ni Macadamia intergrifolia na Macadamia tetraphllya mchanganyiko wa mbegu zote mbili bado unafaa kama zao la kilimo la biashara.

Kwa Afrika,Karanga pori inalimwa Kenya,Malawi.Swaziland,Zimbabwe na Afrika ya Kusini.Karanga pori unaota kwenye eneo lolote la udongo na hali ya joto la kawaida kati ya 25c na 35c.Uzalishaji wa mimea inapendekezwa umbali kutoka usawa wa bahari mita 800.Hali ya hewa inachangia zaidi kuliko mwinuko kutoka usawa wa bahari katika kupata mazao bora.

Mvua katika maeneo yote ya uzalishaji kusini na mashariki ya Afrika,Mvua ni kati ya 800 na 1200mm kwa mwaka hivyo asilimia 70 zinanyesha katika kipindi cha kiangazi na ukame.Kumwagilia kunasaidia hasa kwa miti ile michanga ili kusaidia ikue haraka na kutoa mazao.

Aina nzuri ya karanga pori ni ile yenye uwezo wa kuzalisha tani 4 ya karanga kavu zenye maganda kwa hekta,mmea ukiwa umekomaa katika umri wa miaka chini ya 12 au juu kidogo.Aina bora ya karanga pori huanza kuzaa ukiwa na miaka mitatu au juu kidogo.

Mavuno hutegemea mbinu za uzalishaji na taratibu za maandalizi.Miti ikiwa na umri wa miaka 12-15 mazao huwa kilo 15-50 ya karanga kavu zenye ganda la ndani kwa mti.

Bei ya karanga pori ni dola za Marekani 2.1 kwa kilo kwa karanga zenye ganda la ndani.Wastani wa mazao kwa mti ni kilo 15 kama unachanganya karanga pori na mazao mengine inashauriwa kupanda miti 35 kwa ekari.

Kama huchanganyi na mazao mengine basi huoteshwa miti 270 kwa ekari ambapo pato lake hufikia hadi shilingi za kitanzania milioni 16 kwa mavuno.

Aina inayozalishwa kwa njia ya matawi huanza kuzaa ikiwa na umri wa miaka mitatu hadi minne,lakini mazao halisi hupatikana kati ya miaka 12 hadi 15.Mti wa mkaranga pori huishi kwa miaka 50.


Wadau wanaohitaji kufahamu kuhusu zao hili la macadamia

Wadau,

Kuna fursa kubwa kwenye kilimo cha matunda especially kwa nchi yetu ambayo ina ardhi nzuri na ambayo inafaa kwa mazao mengi.

Zao la Macadamia ni miongoni mwa mazao ya muda mrefu ambalo linaweza kubadirisha kilimo cha Tanzania, kwa sasa kuna mtaalamu ambaye ana kitalu cha miche ya macadamia (mche mmoja unauzwa shs 2,000) macadamia inaweza kustawi vizuri kwenye sehemu za baridi lakini siyo baridi sana hivyo kilolo, ifakara, morogoro, arusha, lushoto inaweza kustawi kwa uzuri zaidi.

Mimi nimechukua miche michache kwa ajiri ya kujaribu kwenye maeneo ya kisarawe.



Michango ya wadau

----
Napendaga hizooo
 
Wengine naona wanachanganya macadamia nuts na pachira aquatica.
FB_IMG_16717735836951179.jpg

Hii ni pachira aquatica siyo macadamia
 
Macadamia inatoa mbegu za mafuta kama ilivyo korosho. Hizo mbegu zinahitajika sana kwa watengenezaji wa chocolate vile vile unaweza kukamua mafuta na ubora wake ni sawa na mafuta ya mizeituni (olive oil). Bei ya Roasted and salted Macadamia Nuts kule Australia naona ni $18. Kule Kenya naona wanalamika utoroshwaji wa Macadamia kuja Tanzania kutayarishwa kwa kusafirisha nje.

Upekuzi zaidi unasema macadamia yanastawi sehemu ambazo avocado, mapapai, na ndizi hustawi. Wakulima wengi wa kenya wanang'oa kahawa ili kupanda macadamia.
Asante Mkuu
 
Alamsiki wanaJF
ninahitaji kujua wapi nitapa hizi macadamia nuts
Mikoa gani inalima sana hizi na pia kama kuna mwenye kujua wapi nitazipata kwa manunuzi ya tani za kutosha
Natanguliza shukrani
Ngoja nilale Kwanza,kukicha narudi kukujibu mkuu
 
Nenda Handeni, kanisa Katoliki wanalima mashamba makubwa sana ya macadamia nuts. Kunaitwa Sakarani.
 
Back
Top Bottom