Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Mungu anatupenda hawezi kutuchoma moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kaka na kukubali sana kwenye nyanja za siasa,uchumi na kazarika.hayo mambo mwachie mshana jr.sijamaliza kusoma uzi wako.maana naona kichwa cha habari kama
lowasa kumfuta magu ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
Utakuwa humsomi vizuri Huyu Bwana Njaa ngosha pasikali au pasiko....kwenye hizi issue yuko kitambo sana na ana nyuzi zenye nyama kwenye mambo ya spirituality...hebu msake upate darsa lililotukuka ( in ff voice)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anatupenda hawezi kutuchoma moto

Sent using Jamii Forums mobile app
It's true, tena tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo, Mungu baada ya kutuumba, pia ametupa utashi wa kuamua kumfuata yeye tupate uzima wa milele au kumfuata shetani na kwenda kwenye moto wa milele. Motoni sio kwa Mungu ni kwa shetani, anayechomwa ni shetani na wote watakaomfuta, wataungana naye motoni.
P
 
Aisee!!.
Kwahiyo na jamaa akaona ma soul mate wake ni wa maana sana kuwafuata wakaendelee kupiga stori kuliko kubaki na watoto japo wakue ndio asepe
Pascal Mayalla, kwanini mwenzi mmoja akitangulia na kisha mwenzie kumfuata, Huko waliko wasiwaite watoto wao pia wawafuate na badala yake wanawaacha hapa duniani wakiteseka na kuhangaika bila msaada wowote?
Ukiisha zikiliza sauti za ulimwengu wa Roho, you loose touch na ulimwengu wa mwili, ila huko huko walipo, watasimamia show, japo wamewaacha yatima, lakini watoto watatunzwa na watasoma, ila kiukweli kabisa sometimes God is not fair at all, maana mambo mengine ni mambo ya karma, watoto malaika wa Mungu, hawana kosa lolote lakini wanaadhibiwa.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako! - JamiiForums
P
 
Mind and soul is one and the same, mind is controlled by conscious while soul is controlled by the subconscious and its immortal
P

No Sir!

Kindly check your facts again.

HINT:
Body - Physical structure

Mind - Consciousness, Semi and Unconsciousness (mental)

Soul - Spirit (ever living influenced by divine or non-divine connection)

Correction on the quote above. It is the body which is controlled by the soul and the mind. Kuna ushahidi mwingi mno kuthibitisha haya niliyoandika. Just check your facts
 
Roho za waovu zitateswa kwa muda kisha zitaharibiwa, Uzima wa milele ni kwa wale walioishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu tu!!

Tazama, UZIMA WA MILELE - Kama Roho za watenda maovu zitaendelea kuchomwa moto inamaana nazo zitakuwa na uzima was milele japo katika mateso ya moto.

Kuna mwili usioharibika kiBiblia unaitwa Theofani hizo Roho za wafu ndio zitavaa.

Kuna mambo mengi kutoka hapa tulipo kuuendea UTAWALA WA MIAKA ALFU MOJA kisha HUKUMU kisha UZIMA WA MILELE.
 
Not fare at all kwakwel.Sema ndio hivyo tena ushaseema Mungu kwahiyo inabid ukubal hata kama ina pain
 

Theoretically may be true!
 
Mkuu nadhani haya uliyoandika ni masimulizi uliyoyapata kutoka kwenye mapokeo ya kabila lako (Culture beliefs)
Kwa mujibu wa biblia ,nafsi hai ni muunganiko wa udongo na pumzi ya Mungu. Tunapoongelea uhai(nafsi hai) ni kuwa mwili Hivyo huwa hakuna uhai ikitokea hivi vitu viwili vikitengana.

Roho inayomrudia Mungu wakati wa kufa ni ile pumzi ya uhai. Hakuna mahali katika Biblia ambapo roho inaelezwa kuwa ina uhai, hekima au hisia baada ya mtu kufa. Ni “pumzi ya uhai”, si Zaidi.

Mwanzo1:7''Na Yehova Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi+ ya nchi+ na kupuliza katika mianzi ya pua yake pumzi ya uhai,+ naye mtu akawa nafsi hai.''

“Roho ya Mungu i katika pua yangu.” Ayu. 27:3. Tunajua kilichopo puani ni pumzi na Ayubu anaita ni Roho Ya Mungu

. Je, mtu aliyekufa anaweza kujua au kuelewa kiasi gani?
“Walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote linalofanyika chini ya jua.” “Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu (kaburini) uendako wewe.” Mhu. 9:5,6,10. “Sio wafu wamsifuo BWANA.” Zab. 115:17.

Litawatokea jambo gani wenye haki waliokufa, wakati wa kuja kwa Yesu mara ya pili?
“Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” Ufu. 22:12. “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,… nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza… na hivyo tutakuwa na Bwana milele.” 1 Thes. 4:16,17. “Sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua,… na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu… Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika…” 1 Kor. 15:51-53.
Kusingekuwa na haja ya ufufuo kama waliokufa wanakwenda mbinguni baada ya kufa.
Uongo wa kwanza kabisa wa Ibilisi ni upi?
“Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa.” Mwa. 3:4. “Yule joka… yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote.” Ufu. 12:9.
Kwa hiyo mkuu Pascal Ukiamini kuwa kuna some sort of life inaendelea somewhere, maana yake unaungana na shetani aliyemwambia Hawa kuwa hata akila lile tunda hatakufa.
 
Twende mdogo mdogo, maadam unajua kuwa tulipuliziwa pumzi ya Mungu tukapata uhai, hiyo pumzi ya uhai ndio Roho, hivyo kifo ni kukata Roho, pale Roho hivyo inapoacha mwili, unakuwa ni mwisho wa uhai kwa mwili tuu, Roho ambayo ni spirit, haina mwisho, it's eternal.

Kuna vingi vimesemwa kwenye Bible vinakuhitaji kufunuliwa ndipo uvielewe.
Ile pumzi tuliopuliziwa ndio Roho wa Mungu na haifi. Na siku ya ufufuo wa miili, miili tunayofufuliwa nayo sio hii miili ya mavumbi ni miili mipya ya spiritual.
P
 
Kuna vitu vimeandikwa kwenye Bible kwa mafumbo na kuleta to coherence ili kupunguza contradictions.

Mungu alimuumba Adam na Eva, lile tunda la mti wa katikati, wa mema na mabaya sio tunda tunda bali ni lile 'tunda', na ule mti wa katikati sio mti mti bali ni 'mti'.

Adam na Eva wakaambiwa fanyeni yote, kuleni vyote, lakini wewe Adam usitumie mti kumega lile 'tunda' la Eva, na wewe Eva, usitoe 'tunda' limegwe na Adam.

Shetani alijigeuza nyoka ili kupenya tuu bustanini, na alipofanikiwa, alijigeuza mtu kijana handsome boy na kumtokea Eva ndipo kumdanya.

Katika kundanganya kule alimega lile tunda la Eva, ndipo Eva nae akamlazimisha Adam kumega na wakaishia usingizini, si unajua yale mambo ya kufika, ndipo walipoamshwa wakajiona wako uchi baada ya kujua kazi ya mti wa katikati na kumega lile'tunda'.

Tangu hapo sasa ndio wakaadhibiwa na kuruhusiwa kuzaa kuongezeka kuijaza nchi yote na hilo 'tendo' ndio dhambi ya asili.

Yaani ili binaadamu azaliwe ni lazima kwanza dhambi ya asili itendwe, tunda limegwe ndipo mimba itungwe.

Mtu pekee aliyezaliwa bila dhambi ya asili ni Bwana wetu Yesu Kristo, kwa Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, bila tunda tunda kumegwa na dhambi kutendwa.

Jee uliyajua hayo?. Vivyo hivyo kifo ni mwili tuu, Roho haifi na sio ushetani.
Yesu alisema ukifa siku moja ni kama miaka elfu moja na miaka elfu moja ni ni kama siku moja. Wanaokufa leo, jana, juzi, na watakaokufa kesho, wote wanalipwa the same, kwenye ulimwengu wa Roho, hakuna mass, distance and time.
P
 
Mkuu kuzaa na kuongezeka kuliagizwa kabla ya kula tunda. Soma upya biblia yako.
 
Mkuu kuzaa na kuongezeka kuliagizwa kabla ya kula tunda. Soma upya biblia yako.
Source yangu sio Bible tuu bali logic.
Bible imehaririwa ili iendane.

Kama zaeni muongezeke ni kabla ya tunda, then dhambi ya asili ni nini?.
Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili na kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kuna maana gani?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…