Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Source yangu sio Bible tuu bali logic.
Bible imehaririwa ili iendane.

Kama zaeni muongezeke ni kabla ya tunda, then dhambi ya asili ni nini?.
Bikira Maria kukingiwa dhambi ya asili na kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kuna maana gani?.
P
Ambaye hana dhambi ya asili ni Yesu na siyo bikra Maria mkuu. Mbona unaniangusha
 
Mkuu ina maana Mama yetu kipenzi Hawa alichepuka...[emoji33]OMG



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambaye hana dhambi ya asili ni Yesu na siyo bikra Maria mkuu. Mbona unaniangusha
Mkuu Mtukutu wa Nyaigela, umechanganya mambo ila sio wewe tuu, bali hata Wakatoliki wenyewe, kwenye Litani ya Bikira Maria kuna sifa nyingi za Bikira Maria zimewekwa lakini sio.

Dhambi ya asili ni kumegwa kwa lile tunda. Ili binaadamu azaliwe ni lazima lile tendo la kumegwa kwa tunda lifanyike.

Hakuna popote nimesema Bikira Maria hana dhambi ya asili, kwasababu naye amezaliwa na dhambi ya asili, kwa lile tendo la kumegwa kwa lile tunda ila Yesu ndiye pekee aliyezaliwa bila dhambi ya asili kwa sababu, kutungwa kwake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na sio kwa lile tendo la kumegwa kwa lile tunda. Bikira Maria ndiye binaadamu pekee, aliyekingiwa dhambi ya asili kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu bila lile tendo la kumegwa kwa lile tunda.

Tena kwa vile mimi ni Mkatoliki, kuna maisha ya Bikira Maria baada ya kuzaliwa kwa Yesu, Wakatoliki hawayajui kwa sababu waandishi wa Bible waliamua wasiyaingize kwe Bible hivyo kwa Wakatoliki, Bikira Maria anahesabika alibaki bikira daima.

Ndani ya Bible, baada ya Yesu kuzaliwa na kukimbilia Misri, hakuna details za maisha yao huko Misri hadi alipotimu miaka 12 alipokuja hekaluni na kupotea tena hadi miaka 30 aliporejea. Details zipo ila hazikuwekwa, Baba mlezi wa Yesu Joseph alikuwa mwanamume kamili rijali, hivyo...
Tuachie hapo.
P
 
Mkuu mwanzo wa uzi wako umesema kwamba kitendo cha kufa ni roho kuacha mwili na ukasema kinachokufa ni mwili ambao baadae unaoza na kuwa mavumbi na roho huenda kuishi sehemu ulizozitaja ambazo sio ardhini.

Lakini wakati huohuo unasema tena kina mama wajawazito huwa wanazuiliwa kwenda kuzika kwa kuhofia vichanga vyao vinaweza kuitwa na wafu makaburini. Daaah mbona kama mambo mchanganyiko
 
Mkuu ina maana Mama yetu kipenzi Hawa alichepuka...[emoji33]OMG
Sent using Jamii Forums mobile app
Enzi hizo kulikuwa bado hakuna mambo ya michepuko. Alichofanya shetani ni kumrubuni Mama yetu Eva na kumuonyesha namna tunda linavyomegwa.
Unaweza kujiuliza, kama Mungu aliumba mwanamke mmoja tuu, hao Cain na Abeli, walizaa na nani ili kizazi kiongezeke?.
P
 
Maisha ya hapa duniani ni mafupi sana tena yamejaa shida, ila tunachukua muda mrefu sana na kutumia kila linalowezekana kusoma elimu itakayotusaidia kuyamudu. Ila tunasahau sana kusoma elimu ambayo inaaminika itatuelekeza kwenye maisha ya MILELE ,yenye raha na kutokufa tena. Tumewaachia viongozi watufundishe. Saa nyingine wanatudanganya kwa kutufundisha vitu tofauti na biblia inavyosema,kwa masilahi yao.
 
Mkuu Magallah, mwili ukiishafukiwa ardhini, unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, kaburi ni ishara tuu, as just an rv ya kukutania, lakini roho zinakwenda kwenye ulimwengu wa roho, huko hakuna tena mass, distance wala time, kwa vile roho ni semu ya Mungu, then roho hizo ni omnipotent, omnipresent na omniscience.

Kitendo cha wamama wajawazito kwenda kaburini, vichanga vinamawasiliano na ulimwengu wa Roho, hivyo its just superstition tuu kuwa vikienda makaburini ndio vitaitwa, vinaweza kuitwa tuu vikiwa popote, ila kule kuona makundi ya watu wakilia, wakihuzunika, vinaweza kushawishika, kwa nini nije duniani kisha nije kuliza watu?, bora...
P.
 
Nakuelewaga saaana bro, asante kwa somo hili adimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujanjaujanja tu wa kucheza na maneno na hisia za watu ila kiuhalisia hamna ukweli wowote juu ya insha hii bro.
 
Mungu ni Roho nao wamubuduo yawapasa kumwamubudu katika roho na kweli.

Well; wewe na wenzako hamuwezi kuamini haya especially kama mungu wenu mnaemuabudu ni yule anaemuombea mtume wake, mwenye uso, miguu na mikono yote ya kushoto.
Umeshasema hatuamini.... obvious ikishakuwa imani tayari hayo ni mashaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna ukweli wowote juu ya bandiko hili,umetumia mfano mmoja tu ambayo hauna ushahidi wowote.
Umeujengea hoja mfano wako kwa hisia ya tukio husika kwa kuutafutia maneno ya kiraghai.

Wote tutakufa yes,lakini sio kwa kuitana bali ni kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu.

Hapa nimekutaa Bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Losser Bad, kwanza ni kweli, aliyetuumba, na kutupa uhai, ndiye pekee mwenye mamlaka kuruhusu Roho iache mwili kwa kifo, mwili urudi kuwa mavumbi na Roho iende kwenye ulimwengu wa roho.

Hayo yote ni mipango na mamlaka ya Mungu, ila zaidi ya miili yetu kuwa na Roho wa Mungu, pia Mungu ametupa utashi, conscious ya kuamua, tumfuate yeye na kuzishika amri zake tuishi milele, au tumfuate shetani na mambo yake, tufe. Wazazi wetu wa mwanzo waliamua kutenda dhambi iliyotuumbia kifo, hivyo japo kifo ni kwa mapenzi ya Mungu, lakini kuna vifo vingi ni mipango ya mwovu shetani, japo anayetoa kibali sasa Roho iache mwili ni Mungu pekee.

Katika ule utashi, conscious Mungu aliotupa kuamua, ndani yake kuna powers za maamuzi zinaitwa "will Powers" ambazo ndicho kitu chenye nguvu kuliko kitu chochote duniani, hizo Will Powers, ni nguvu za Mungu zilizo ndani yetu na kila mtu anazo, nguvu hizi ndizo huamua hatima yetu, nikimaanisha sisi tuna nguvu za Kimungu ndani yetu, na shetani yupo kiturubuni tumuasi Mungu, kwa kutenda dhambi na kumfuata yeye. Mungu baada ya kutupa amri zake, pia ametupa utashi wa kuamua kumfuata yeye Mungu au kumfuata shetani, hivyo kuna baadhi ya matendo ya dhambi tunazotenda, yanasababisha vifo, japo Roho kutoka ni kazi ya Mungu.

Mfano ukiamua kumuua mtu kwa kumpiga risasi, huo ni ushetani, na kikawaida, risasi moja tuu inatosha kutoa roho ya mtu, lakini kama Mungu hajaruhusu Roho ile itoke, hata ukifanya ushetani mkubwa wa kumfyatulia mtu risasi 16, kama Mungu hajaruhusu Roho ile itoke, then mtu huyo atapona, na hata kama ingetokea akafa, huwezi kusema risasi zile ni mpango wa Mungu, no ni mpango wa shetani japo kibali cha Roho kutoka ni kazi ya Mungu

Hivyo kuna vifo vingi ni mipango ya shetani, ajali, maradhi, majanga, etc, na ndani ya vifo hivyo kuna vingine ni mtu mwenyewe ame will afe, kwa kukubali kuitwa na walio kifoni na yeye kukubali, hivyo ugonjwa, ajali, majanga ni kutafuta tuu sababu ya kuhalisha kifo ili tuu mtu uchomoke, lakini unaweza kuitwa kifoni, kwa kupitia will yako ukakataa kuitika, utaendelea kuishi

Watu walio karibu na wagonjwa mahututi, hufikia kipindi, mgonjwa anauona ulimwengu wa roho, anatamka kuwaona baadhi ya watu waliokufa zamani wanamfuata, atawataja kwa majina, kwa vile na nyinyi mko na mgonjwa wenu, na nyinyi hamuwaoni hao watu, basi mnamuona mgonjwa wenu kama anaona maluweluwe kisha mnanuona kama anaweweseka, kumbe ndio safari, kuitwa, kaitika, safari kimoja jumla

P.
Rejea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…