Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

Jamaa kaongea mashudu tu apo
 
Sasa hivi huwezi kumtofautisha Pasco na Jingalao wa JF. Uchama umemuondolea weledi wote aliokuwa nao kabla hajajitoa ufahamu na kuwa muimba pambio za kumsifu na kumuabudu dikteta Magufuli.
 
Mkuu

Ni kweli kabisa
Aisee jamaa ni mchomi hatari sana na ni chawa wa mwendazake
Uyu jamaa PASKALI nae unafiki wake umeumiza wengi.

Na watanzania tungekua wa visasi,
Uyu nae alipaswa aunganishwe na Ole sabaya.

Bad enough,
Unafiki aliwafanyia zaidi familia yake(waandishi wenzake) akifukuzia uteuzi,

Sasa jiulize wewe mtu baki atakufanyia unafiki wa aina gani ukiingia 18 zake.

Lile Gazeti la yule Kiongozi wa jukwaa la wahariri (somebody BALILE)

lilifungiwa kwa chokochoko zake alizoanzisha PASKALI humu humu jf, akijifanya mtanzania mzalendo akitanguliza maslahi ya taifa mbele anachambua na kukosoa makala wanazoandika wenzie kumkosoa jiwe.

Mwisho wa siku,
Wenye mamlaka wakaona gazeti linaisnitch serikali wakalipiga BAN.

TUTAMSIKILIZA KWA LIPI TENA, MNAFIKI KAMA HUYU
 
Hujaacha mambo yako ya kukurupuka.siku ile ulikurupuka ukamtwanga mwendazake swali gumu akakunyima teuzi hadi siku anakwendazake.sasa umeanza kukurupukia mambo ambayo huyajui.Sukuma gang watashugulikiwa sana tena wote we tulia tu.huoni wenyew wamenywea?
 
Uyu jamaa anazeeka vibaya mno,

Nnachokiona kwa paskali,
Watu waovu wote walikua upande wake na amekua akitumia nguvu kubwa sana kuwatetea kwa propaganda dhaifu humu.

Mfano: makonda, jiwe, ole sabaya,mnyeti na ndugai

Paskali ni miongoni watanzania wa kuepukwa mno,

sijui hata majirani zake uko anakoishi anaishi nao vipi bila kuwasnitch.
 
Uncle leo andiko lako limepwaya mnoo,
Labda kwakua imani yangu haiamini juu ya maisha baada ya kifo.... Sitozongumzia hapa kwakuheshimu utofauti was imani zetu.

Pili, naungana na wewe kwenye double standard japo nnaimani mama ametumia njia hii ili kutokuzua taharuki na kuhatarisha serikali yake ( badala ya maendeleo ingeonekana ni awamu ya visasi)

Tatu, nimeshindwa kukuelewa unaposema et kwakua tulimpenda basi tupende na mapungufu yake??? Siamini kama ni wewe Uncle Wangu Mayalla
Nadhani umesahau mamlaka aliyokuanayo kama palikua na amtu alijaribu kumzuia au kumpinga akabaki salama hata wewe ni mhanga everyone knows!

Yeye hayati ameondoka na KARMA yes KARMA na itaendelea kuwatafuna wale woote waliomtii kutoka moyoni. Muache mama aonnyeshe kwa vitendo hofu yake ya Mungu.
 
Pascal Pascal Pascal...

Nimekuita mara 3 kaka yangu Mwana wa Mayala...! Mimi nitadodosa pale ulipokosea tu..! Ni kweli umesema hiyo ni imani yako lakini kwa uhuru tulionao nina haki ya kukukosoa ktk imani yako iliyo kinyime na usawa.

Nakubaliana na wewe kwamba wafu wapo hai. Wamekufa maisha ya dunia lakini huko waliko wana uhai mwingine tunaouita uhai wa kiroho. Lakini hapo hapo napingana na wewe, kwamba wafu hao wanayashuhudia na kuyaona yanayoendelea duniani. Hili nakuomba usafishe kwenye moyo wako na ulifute kwa moto..! Sio sawa, na sio sahihi.
 
Mimi bandiko lote kuna sehemu ndogo nimeinasa na uzuri mabandiko ya Paskali yana u prophetic flani.

Kama sikosei Paskali amekulia kota za "wazee" na "mzee" wake .... pia amepokea sakramenti zake zote St Peter jirani na "wazee"......

Nitarudia hili bandiko tena naweza kuokota kingine! Mnaosoma kishabiki hamtomwelewa.
 
Duh aisee ni balaa
Mzee mahiga walikua na tofauti ipi tena na mwendazake au ile ya kumpokea obama k.i.a
Adhabu ya kunyongwa kumbe ipo maana hata mwendazake alisema anaogopa kuipitisha
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla nimesoma uzi wako wote na kuna hoja nakubaliana nazo na kuna zingine sikubaliani nazo kabisa.

Hoja ya "life after life" sikubaliani nayo. Imani yako wewe kama Mkristo inapaswa kujikita na NENO la MUNGU na siyo hadithi za kufikirika, fables or myths.

Unasema eti roho haifi, siyo kweli ndugu, soma Biblia vizuri, roho ya mwanadamu inakufa. Soma Ezekieli 18:4 imeandikwa hivi, "Tazama roho zote ni mali yangu, kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu, roho ile itendayo dhambi itakufa".

Pia hebu soma Mhubiri 9:10.

Itoshe tu kusema kwamba mtu akifa, amekufa, na roho yake haiwezi kamwe kuona, kunusa, wala kusikia yanayofanyika duniani. YESU KRISTO alitoa hadithi ya mfano kuhusu nini kinatokea baada ya kifo, hadithi ya Lazaro na yule tajiri. Luka 16:19-31

Anyways, mtu akifa haoni chochote kinachotokea hapa duniani. Magufuli amekufa na haoni na hayupo tena. Tusiogope kuchukua maamuzi sahihi kisa tu eti "wafu" wanatuona. Hapana hiyo siyo kweli, ni imani yako tu.

Kuhusu kuwashughulikia watuhumiwa nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%. Washughulikiwe wote pasipo ubaguzi, wote wenye tuhuma wachunguzwe na ikionekana wana hatia basi sheria iachwe ichukue mkondo wake. Asionekane tu mtu mmoja kuwa ndiye mkosaji wakati kuna wengine pia. Lengai Ole Sabaya asiwe "mbuzi" wa kafara.
 
Bwana Mayalla kama utawala uliopita kwa jinsi ulivyo upigia debe haukuambulia chochote basi hawa watu achana nao tu wewe endelea na issue zako.Huenda Mungu akakuona huko mbele kwa mbele!
 
Mtu kama Paskali akipewa madaraka atatenda mabaya kuliko hata huyo sabaya mwenyewe.

Ni mtu hatari sana
 
Mama anajitahidi kuweka taasisi imara zenye uwezo wa kumsaidia kusimamia taratibu na sheria
 
Mjue Magufuli huko aliko bado yupo na anaona yote tunavyowatenda watu watu, asije akakasirika na akamlilia Mungu, watu wengine wakaitwa!.

Hapa kwa kweli sijakuelewa!
Ninachojua kuwa wafu hawana ijara tena hapa duniani.
 
Mungu alimuumba binadamu akiwa amegawanywa katika sehemu tatu:roho,nafsi, na mwili(spirit, soul and,body) sivyo ulivyosema katika mada yako.Tatizo kubwa la mwendazake,nionavyo aliikubali sana nafsi yake badala ya roho aliyopewa na Mungu.Ndo maana viongozi tunaowachagua tunawaombea sana kwa Mungu ili roho zao ziongozwe na Yeye sio nafsi zao.
 
Dikteta alishakufa hakuna cha roho inaishi wala nini? hawa majangili wote wakamatwe akina Makonda, Bashiru Ndugai, Mwigulu, Polepole, Msiba, Hapi na Lugola
Nimekudharau!
Hapo kwa kosa lipi, Bashiru Kwa kosa lipi kikatiba, Polepole naye,

Huu ushabiki wa kipumbavu mnaoufanya hapa, hauna maana zaidi ya chuki zenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…