Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

Mwaka jana mwishoni mfanyabiashara na mbunifu wa mavazi Jeffery Mmbungu maarufu kama @Speshoz alifungua kiwanda cha vinywaji vikali, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kiwanda hicho kinaitwa Daren Fabrics Industries Ltd kinazalisha kinywaji chenye jina Faru John.

Mwezi February mwaka huu, aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alimpigia Jeff na kumwambia kuwa CCM itafanya maadhimisho ya miaka 44 tangu kuanzishwa, na yeye ni miongoni mwa wanakamati wanaoandaa maadhimisho hayo.

Akataka kiwanda hicho kichangie TZS 10M kufanikisha maadhimisho hayo. Jeff akamwambia hana uwezo wa kuchangia 10M, lakini akaahidi kuchangia 1M. Sabaya akamnanga kwamba serikali ya CCM ndiyo iliyomuwekea mazingira mazuri ya kibiashara hadi akaweza kufungua kiwanda, kwahiyo kuchangia 1M ni dharau kwa chama, anatakiwa achangie kiasi kisichopungua 10M.

Jeff akamwambia hana pesa hiyo. Sabaya akamwambia nimepitia transaction zako TRA najua unafanya mauzo ya mamilioni ya shilingi. Jeff akamwambia bado kiwanda ni kichanga na hakijaanza kujiendesha kwa faida kiasi cha kumpa Sabaya 10M.

Mwezi May mwaka huu Sabaya akavamia kiwanda hicho akiwa na mabaunsa wake. Wakawa-harass sana wafanyakazi waliokuwepo. Sabaya akiongozana na waandishi wa vyombo 11 vya habari akatangaza kukifunga kiwanda hicho kwa madai kinajiendesha bila vibali.

Vyombo vya habari vikaripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa kwa kufanya uzalishaji wa vinywaji vikali bila kuwa na kibali. Jeff akashangaa kwa sababu alikua na vibali vyote.

Ana leseni ya BRELA nambari 142255766 iliyotolewa July mwaka 2020. Ana leseni ya TRA nambari 142255766 iliyolewa July 2020. Ana leseni ya biashara nambari 03356294 iliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Hai tarehe 25 September 2020.

Ana Leseni ya mkemia mkuu wa serikali nambari B002C000255 iliyotolewa October mwaka 2020, pia ana Leseni ya TBS nambari 3082 iliyotolewa December 2020. Pia kabla ya kuanza uzalishaji alipewa barua ya ruhusa kutoka TBS yenye Kumbukumbu nambari QA/QCCA/3215/17.

Sasa akashangaa imekuaje kiwanda kifungwe kwa kukosa vibali wakati vibali vyote anavyo? Akampigia Sabaya kumuuliza. Akamwambia aende ofisini.

Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande.

Taarifa za kukamatwa kwake zikafika kwa viongozi mbalimbali wa serikali. Wizara ya ya viwanda na biashara ikatoa tamko kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kwa mujibu wa sheria. Wizara ya uwekezaje, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali, Shirika la viwango (TBS), pamoja na ofisi ya BRELA wakaingilia kati na kueleza kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kihalali.

Kesho yake Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro akafanya press na kutoa ufafanuzi kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa hiyo ikaeleza kuwa mwezi April kiwanda hicho kilipewa stika za 200M na kiliweza kuhuisha stika za 93M. Pia kwa siku chache za mwezi May (kabla hakijafungwa) kilikua kimehuisha stika za 13M.

Taarifa ya TRA ikaeleza kuwa kiwanda hicho hakijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala hakijawahi kujiendesha bila kuwa na vibali. Ikatangaza kukifungulia kiwanda hicho na kukiruhusu kiendelee na uzalishaji.

Media zote zilizoripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa zilialikwa kwenye Press ya TRA ili ziujulishe umma kwamba taarifa ya Sabaya haikua sahihi, na kwamba kiwanda hicho kimeruhusiwa kuendelea na uzalishaji.

Lakini Sabaya akazuia media hizo zisiripoti taarifa hiyo ya TRA. Ni ITV pekee walioamua kusimama katika misingi ya taaluma na kutoa ufafanuzi kwa umma. Media nyingine ziliamua kusimama na Sabaya. What a shame?

Tayari Jeff ameshaenda TAKUKURU kuwasilisha ushahidi wake. Pia atawasilisha malalamiko Baraza la habari nchini (MCT) ili media zilizomchafua na zikakataa kumsafisha zichukuliwe hatua, kwa sababu habari ya kiwanda hicho kufungwa imeathiri mauzo kwa kiasi kikubwa

Huyu ndio sabaya gaidi wa kiuchumi
 
Wafu hawajui Neno lolote angekuwa anajua kila kitu asingekubali kufukiwa udongo hata kidogo.
 
Si bure Paschal utakuwa mchawi, Magufuli hajui Neno lolote Kwa vile yeye ni mfu na wafu hawajui lolote. Ingekuwa wanajua au kama JPM angekuwa anajua asingekubali kufukiwa kamwe.
Kwamba Kwa kuwa tunamienzi Magufuli tuwapende na aliowapenda hata kama walikuwa majambazi, hivi familia zile ambazo ndugu zao waligongelewa misumari ya ugoko nao wamuenzi JPM Kwa kumpenda Sabaya?
Alafu kumbuka waliotoa ushahidi wa kubakwa walikuwa wanavyuo huenda wangine ni ndugu zako.
MTU anayeamua kufunga kiwanda cha MTU Kwa sababu Tu hajampatia milioni 10 apendwe?
Paschal Katika hili ungenyamaza Kwanza ukasoma upepo kulikojuandika huu upuuzi
 
Thank you 🙏🏾 Sir 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾👍🏽
 
Awamu ya tano wahalifu walikuwa wengi waadhibiwe wote bila double standard-Mwenye awamu yake alitumbua baadhi tu ya viongozi kutafuta attention lkn wengine aliwakumbatia ilhali walistahili adhabu ya kutumbuliwa kwa sababu na wao waliharibu kama walivyoharibu aliowatumbua

Sabaya kafungwa pingu na kachuchumalishwa sio sahihi- mwenye awamu ya tano aliwaweka watu mahabusu kwa amri tu bila makosa yoyote au kwa tuhuma za kusingiziwa bila kupelekwa mahakamani

Tuenzi mazuri ya awamu ya tano wakati mwenye awamu yake hakuenzi awamu ya nne alisikika tu akiituhumu awamu ya nne ilikuwa awamu ya wezi

KWA WALIOIPENDA AWAMU YA TANO WAJITAHIDI KUMUOMBEA DUA KIPENZI CHAO HUKO ALIPO APUNGUZIWE ADHABU YA MWENYEZ MUNGU KWANI SIAMINI KAMA ANAPATA HATA TIME YA KUZINGATIA HAYA YANAYOENDELEA HUKU[emoji120][emoji120][emoji120]
 
ngonjera na stori za vijiweni haziana maana mbele ya mahakama, hayo yanabakia kuwa maneno ya Majungu na fitina, kinacho takiwa ni ushahidi sio maneno matupu.

kama ni majungu tu kila mtu anasemwa, hata wewe mwenyewe wapo wanao kusema vibaya lkn hakuna ushahidi.

kila kiongozi ktk nafasi yoyote ile anasemwa, analalamikiwa, sasa tukianza kuokoteza malalamiko basi wote watashitakiwa, wote watafukuzwa.

ushauri wangu;
viongozi walio pewa dhamana ya kuamua hatima ya walio chini yao kamwe wasiwaonee watuhumiwa kwa kusikiliza malalmiko ya majungu.
 
So what? Who cares?
 
Huyu nae anapaswa kufunguliwa mashtaka
 
Hana uwezo wowote hata akiyaona.

Ingekuwa hivyo angewasema nop angesema course of his death
 
Umelaaniwa nanuzao wako. Ridisha aliowaua Sàbaya? Aliowaua Makonda? Mrudishe mama yake Kabendera. Acha talalila zako Pascal. Wapendwa wetu wako wapi waliopotea kwenye regime ya Jiwe? Acha hizoo Pascal, ulaaniwe na uzao wako!
 
Baada ya bandiko reeeeefuuuuu.... Je Mkuu wadhani Mungu halipi? Ama wadhani uhalifu au udhalimu unaolindwa na wanadamu huwa haulipwi? Usijihangaishe kutetea wanaotuhumiwa uhalifu ati sababu walikuwa vipenzi vya mwendazake. Ikiwa kumuenzi mwendazake ni kubariki maovu yaliyotendwa na wateule wake wanaoaminika ni vipenzi. Ni nani hakumjua Mzee Mramba? Je alivyofagia pale ofisi ya umma pale Kigamboni haikuwa kumdhalilisha? Sihitaji kukumbusha mengi ila jiweke kwenye familia za Azory Gwanda, Ben Saanane, Roma, Mo Dewji, Mzee Rugemalira na wengineo wengi ambao tunawajua na tusiowajua ambao walinyanyaswa na walinyanyasika huku 'media na raia wakitazama na wengine kushangilia madhila" wengine hata kwa kuporwa wake na mali zao huku wapendwa "hawakupata kuhojiwa walikotoa magari ya kifahari na makasri ya kifalme kwa mishahara yao ya utumishi hata wakajinadi kula raha kuliko mtu yeyote!!"
 
Neno tu kwako, diginity! Wahanga wote wa Sabaya hawakuwa treated with diginity, so if you lived by sword, you must die by sword!
 
Neno tu kwako, diginity! Wahanga wote wa Sabaya hawakuwa treated with diginity, so if you lived by sword, you must die by sword!
ndio maana hata ukiwateka mateka vitani unatakiwa uwape haki zao za kimateka hutakiwi kuwadhalilisha eti kwa kuwa alikuwa anapambana na wewe na ameua askari wenzako.
sheria za kimataifa zinakataza udhalilishaji, pia sheria zetu zinakataza kumdhalilisha mtuhumiwa, bado ni mtuhumiwa tu, bado hizo dhana unazo mdhania hazija thibitika, yawezekana ni uongo lkn pia inawezekana ni ukweli, hivyo kwa sasa asihukumiwe.
 
Kuna mtu mmoja wa pale Makumbusho aliniambia kwa kujiamini kabisa kwamba Mr. Ben ataondoshwa na kweli baada ya siku 15 akafa.. sababu ni wale wabadilisha ukomo wa uraibu walijua atakuwa kikwazo kwao
 

Kula tano boss, hapa umemwambia ukweli Paskali kuwa sio mtu wa principle. Eti anasema Magufuli anaona na tumesema tunamuenzi, hakuna mtu anamuenzi mtu muovu, yale yalikuwa ni maneno ya kuzugia tu, lakini watu wengi wanajua pasi na shaka kuwa alikuwa mtu muovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…