Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?

Kufuru kivipi?!. Usukuma wangu unaingiaje kwenye bandiko hili?!. Wakristo, Waislamu, Hinduism na Buddhism, dini zote hizi zinaamini kwenye after life, Wakristo na Waislamu wanaamini kuna peponi na jehanam ya moto wa milele, wakati Buddhism na Hinduism wanaamini reincarnation.
Kufuru iko wapi?.
P
Uislam hauamini mtu kuyaona yanayondelea duniani baada ya umauti.

Usiuchanganye na imani za Kikristo na kipagani. Ni tofauti kabisa.

Usukuma wako umeingia kwa sababu umsmetuletea mambo kama fikra na mila zako ulizokulia. Wasukuma si mnajulikana kina Mfalme Zumeradi na kuamini mambo ya kishirikina, uliyoyaandika yana akis usukuma.

Wewe msukuma na uliyemwandika msukuma, itakuwa mna imani ya kujidanganya mkifa mtawaona walio hai.
 
Uislam hauamini mtu kuyaona yanayendelea duniani baada ya umauti.

Usiuchanganye na imani za Kikristo na kipagani. Ni tofauti kabisa.

Usukuma wako umeingua kwa sababh umstuletea mambo kama fikra na mila zako ulizokulia. Wasukuma si mnajulikana kina Mfalme Zumeradi na kuamini mambo ya kishirikina.uliyoyaandika yana akis usukuma.

Wewe msukuma na uliyemwandika msukuma, itakuwa mna imani kuonana mkifa.

=sababu na sio sababh
=umetuletea na sio umstuletea
=akisi na sio akis

Pia jifunze matumizi sahihi ya nukta.
 
Unatafuta laana ya Mungu wewe mwanadamu mwisho wake ni kuoza na kunuka tu utasikia nini huku umeoza na unanuka😄😄
Unless kama wewe ni mpagani usiyeamini Mungu kinachokufa na kuoza ni lile kasha tuu la kumbebea mtu, liitwalo mwili, lakini roho haifi, inaendelea kuishi kwenye uzima wa milele!. Ama mbinguni peponi kwenye raha ya milele!, ama jehanam kwenye ziwa la moto wa milele yaani motoni!.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwa naweletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni kuhusu dhana ya kitu kinachoitwa "Life after Life", ambapo najikita kwenye maswali haya Je, wajua kuwa, binadamu hata baada ya kufa, bado anaendelea kuishi?. Mfano rais Magufuli, japo amekufa, ni amekufa kimwili tuu, ndio hatuko naye, lakini kiroho JPM, bado tuko nae, na huko alipo, bado yuko hai kiroho na kwa kutumia macho ya roho, anayaona mambo yote yanayoendelea kwenye Tanzania yake?.

Je, hiki tunachokifanya kwa baadhi ya wale aliowapenda, are we doing him right?, are we fair to him kwa hawa vijana wake?. Na kama issue ni viongozi waliofanya uovu kipindi cha awamu ya tano, wako wengi wamefanyiwa uovu, Ben Saanane alipotezwa baada ya kuposti kitu humu jf, Azory Gwanda alifuatwa na gari nyeupe ya mkonga ikampeleka hadi shambani kuchukua ufunguo wa nyumba kwa mkewe, wakaenda nae kwake kumpekua, wakaondoka nae and that is the end of him, hakuna majambazi yoyote yanamchukua mtu na kwenda kumpekua kisha kutokomea nae!.

Tundu Lissu alipigwa risasi mchana kweupe kwenye eneo la high security area huku likilindwa na CCTV, mpaka leo hakuna taarifa zozote za uchunguzi. Kumetokea matukio mengi tuu ya kutisha na kusikitisha yaliyotokea Awamu ya 5, swali ni je tuendelee kuwashughulikia kwa double standards kwa kutumia mfumo wa cherry picking kwa kuchagua baadhi tuu wa kushughulikia na wengine kuwa spaired, au tuiachie karma ndio iwashughulikie? kwasababu kwenye karma, hakuna mswalie Mtume, kila jiwe litapinduliwa!.

Muumini wa Karma na After Life
Naomba kuanza kwa kujitambulisha kuwa mimi sio tuu ni muumini wa karma, pia ni muumini wa after life na reincarnation. Hivyo rais Magufuli japo ametutoka na hatupo nae tena, ametutoka kimwili tuu, lakini kiroho bado tuko nae, na huko alipo anayaona yote yanayoendelea baada ya yeye kutangulia mbele ya haki, na anaona jinsi mnavyowatenda baadhi ya viongozi vipenzi wake kwa kuwa persecute kwa kuwa prosecute, kwa kuwadhalilisha!, Jee huku ndiko kumuenzi? Suppose yeye mwenyewe angekuwepo hai, na madudu ya Ole Sabaya yakaibuliwa, Jee Ole Sabaya angetendwa alivyo tendwa majuzi?. Hivi hatuwezi kumprosecute mtu with dignity?. Mjue Magufuli huko aliko bado yupo na anaona yote tunavyowatenda watu watu, asije akakasirika na akamlilia Mungu, watu wengine wakaitwa!.

Mimi na utetezi za haki za binaadamu, sikuanza leo, nilipigania adhabu ya kifo ifutwe, hata wahalifu, watesaji na wauwaji wanastahi kutendewa haki na dignity!
Naomba kujitanabaisha kuwa mimi ni mtetezi huru wa haki za binaadamu, humu jf nina mabandiko zaidi ya 100 ya utetezi wa haki, na kwenye gazeti la Mwananchi la kila Jumatano, na Nipashe la kila Jumapili, nina safu ninaandika makala za utetezi wa haki za binaadamu. Japo siungi mkono matendo ya kihalifu au uhalifu wa aina yoyote, ukiwemo uhalifu wa Ole Sabaya, lakini siungi mkono udhalilishaji wa aina yoyote anaofanywa na jeshi la polisi, magereza, vyombo vya uchunguzi, ofisi ya DPP, na vyombo vya utoaji haki, mahakama, mfano jana pale Mahakamani, Ole Sabaya ameletwa huku amefungwa pingu, as if ni kibaka! Kama haitoshi, akachuchumalishwa as if kumzuia asitoroke!. Huu ni udhalilishaji, huyu ni mmoja wa viongozi vipenzi wa JPM. Kabla hajateuliwa DC, alikuwa anakabiliwa na kesi mbaya ya jinai kufanya tukio la kihalifu kwa kujifanya TISS, JPM akamnasua kwa kumteua kuwa DC ikabidi DPP akaifuta hiyo kesi kwa nolle. Sasa kwa vile kuna ahadi ya kumuenzi JPM kwa mazuri yake, then tumuenzi kwa mtindo wa boga, ukipenda boga, penda na ua lake, na kwasababu sasa JPM hayupo, tukiamua kuwatupa watu wake, then tuwatupe kwa kutumia mtindo wa kumtupa jongoo, ukitupa jongoo, usitupe na mti wake!. Kama tulimpenda JPM, na tukaahidi kumuenzi, then tuwapende na watu wake aliowapenda, hivyo Ole Sabaya, awe treated fairly with dignity huku tukikumbuka kuwa Magufuli anayaona yote tunavyowatenda viongozi vijana wake!, huko aliko, asije akakasirika, akamlilia Mungu, watu wakaitwa bure!.

Life after life in Christianity: Mwili wa nyama ndio unakufa na kugeuka mvumbi, mwili wa roho, haufi, na unaishi milele!.
Hii dhana ya after life, karma and reincarnation sio dhana ya kwenye imani ya dini kuu mbili, za Kikirsto na Kiislamu, hii ni dhana ya dini ya Hinduism na Budhism ila kwenye ukiristo pia ipo.

Uhai ni nini na kifo ni nini?
Mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa udongo ukapuliziwa pumzi ya uhai, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni roho, life force, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astral body, mwili wa nyama unapokufa, roho haifi, bali roho huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha mtu kukata roho ni kitendo cha roho kuacha mwili, hiyo roho, haifi bali inatoka na ndio inayokwenda mbinguni mbele ya Mungu, ndiyo inayohukumiwa, ndio inayokaa peponi au motoni.

Je, baada ya kifo, hiyo Roho inakwenda kuishi wapi?
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili na roho, mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendelea kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye ziwa la moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu. Hivyo mwili huo wa roho, unaona kila kitu kinachoendelea hapa duniani.

Ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayo fufuliwa ni miili ya roho, ile miili ya nyama ikiisha zikwa, that is the end
Wakristu tunakitu tunaita fumbo la imani, tunaamini Yesu alikufa, Yesu alifufuka na Yesu atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho, ambapo kutatokea ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayohusika kwenye ufufuko wa miili ni miili ya roho na sio hii miili ya nyama. Kuna wengi pale wapendwa wetu wanapokufa, tunawazika kaburini, na kwa kadri ya uwezo, mwili unavishwa vizuri, kaburi linajengwa vizuri, na kuna watu huenda makaburini kufanya ibada za wafu, bila kujijua, hivyo wale wanaochoma miili kuonekana kama hawamtendei haki marehemu, ukweli ni kwamba, roho ikiisha acha mwili, that is the end of body, mwili hauna issue tena, unarudi mavumbini, mambo yote ni roho. Hivyo ninaposema Magufuli yupo na anaona kila kitu, ni kweli yupo na anaona.

Jee Roho za Waliokufa Huweza Kurejea Duniani?.
Yes, kwanza kwa wale wanaokufa katika mazingira ya kutatanisha, miili yao isipatikane wakazikwa rasmi, baadhi yao roho zao hubaki duniani, zikitanga tanga na sometimes zikisumbua, hizi zinaitwa "wondering spirits", kuna baadhi ya majumba hayakaliki kwasababu kuna roho zinasumbua, majumba haya huitwa "hauted houses". Kuna baadhi ya wafu huwatokea walio wazima ama kwenye ndoto, ama kwa visions kama Bikira Maria alivyowatokea wale watoto kule Fatima, Louedes Ufaransa. Mara nyingi wafu hurejea kama mizimu, hivyo kuna wengi wanalindwa na mababu bila ya wao kujijua, uthibitisho ni vitu vinavyoitwa miraculous escapes, inatokea ajali mbaya ya kutisha, gari linabondeka na kuwa chapati, halafu unakuta watu wametoka wazima, hata scratch hawana!.

Je, kwenye ahadi ya kumuenzi Magufuli tumuenzi kwa yote au tuchague mazuri tu?
Kwavile rais Magufuli hakuwa malaika, alikuwa ni binadamu, hivyo ana mazuri yake, na pia ana mabaya yake ya kibianadamu kama binaadamu mwingine yoyote, hakuna aliye mkamilifu, hivyo tumuenzi Magufuli kwa mema na mazuri yake kwa kuyaendeleza, halafu yale ya kibinaadamu, tumuachie mwenyewe, tuwe tumemzika nayo siku ile pale Chato na tusiyazungumzie mabaya yake ili kuepuka kumzungumzia vibaya marehemu, ili kumuacha marehemu apumzike kwa amani, ila kwenye kuzungumzia mabaya hayo kwa lengo la kutoa angalizo kwa kuwasaidia waliopo ili yale mabaya hatarishi yenye bad karmic consequenses yaepukwe, yasije yakajirudia, tukaja kujikuta tunapoteza wengine, maana karma haijui cha nani wala nani, ikifika stage ya karma kula kichwa, karma inakula kichwa!. Kwa vile tuna wazee wa kusoma karma trends humu, tunawajibu wa kuwasaidia viongozi wetu, waliongoze vizuri taifa letu kwa kuepuka kufanya makosa ya nyuma.

Baada ya Bwana Yesu kufa kwa mateso ya kusulubiwa na kifo msalabani, wanafunzi wake walijifungia kwa kuhofia na wao kusulubiwa, ndivyo ilivyo kwa Baadhi ya Watu wa Magufuli
Vivyo hivyo baada ya kifo cha Magufuli, kuna baadhi ya watu walilia kwa mengi wakiwemo wamachinga, Magufuli aliwaruhusu kufanya biashara popote, matokeo yake kwenye baadhi ya maeneo sasa ni balaa!. Siku Wamachinga wakiondolewa, watalia tena na kumkumbuka Magufuli, na wao pia watauliza kama kufukuzwa kwao ndiko kumuenzi Magufuli?. Ili kuwaelimisha watu wa aina hii, ni lazima waelimishwe kuwa hata Magufuli hakuwa mkamilifu, ataenziwa kwa mazuri tuu, hili la kuwaruhusu machinga kufanyabiashara popote, sii miongoni mwa mazuri ya kuenziwa, bali watawekewa utaratibu rasmi wa machinga kufanyabiashara bila kuwa kero kwa wengine.

Vivyo hivyo kwenye wateule wa JPM, kuna baadhi ya viongozi Magufuli aliwapenda sana, matokeo yake wakavimba vichwa, wakajiona kama miungu watu, wanaweza kufanya lolote na wasifanywe chochote, na hawakuamini kama Magufuli naye ni binadamu tuu, leo yupo, kesho anaweza asiwepo, au anaweza kufa. Mmoja wa wa watu hawa ni Comred Ole Sabaya, siku ya mazishi ya Magufuli, mmoja kati ya waliolia sana ni Ole Sabaya, inawezekana alilia kwa mengi, uchungu wa kufiwa na mtu unaempenda sana, au wasiwasi wa nini kitampata baada ya nguzo na egemeo lake kuanguka, ndio maana mkamuona akifanya juhudi kubwa, ikiwemo kwenda Clouds kujisafisha, but very unfortunately, haikusaidia, sasa yuko korokoroni aki treatiwa kama kibaka!.

Viongozi wahalifu kipindi cha Awamu ya Tano ni wengi, sio Sabaya pekee. Kama tumeamua kushughulika nao, tuwashughulikie wote
Kwenye awamu ya Tano, viongozi waliotenda mambo ya ajabu ajabu ni wengi, sio Ole Sabaya peke yake, kama awamu hii ya 6 ya Mama Samia, imeamua kuwashughulikia, then iwashughulikie wote. Tuache kufanya double standard ya cherry picking kuwashughulikia baadhi, na kuwaacha wengine, tena baadhi yao Mama Samia kaamua kuendelea kuwabeba mfano mzuri ni RC mmoja alimuamuru RPC wake kuwa namna ya kupunguza msongamano magerezani, ni kuwapiga risasi na kuwaua papo hapo vibaka wote!, na kujiproud kwa ushujaa wake jinsi alivyo muua kibaka kwa kumpiga risasi mbili za kichwa na kumuua papo hapo, kisha akajipongeza kwa kunywa bia mbili!.

Rais Mama Samia Kaanza Vizuri, Angeweza Kuibwaga Mizigo Yote ya Magufuli, Lakini Kafanya Uungwana Mkubwa ya Kuwatumbua, Kiungwana na Kistaarabu huku Akiwapooza Baadhi
Kwa vile kuna viongozi Rais Magufuli aliwapenda, Rais Mama Samia halazimiki kuwapenda, ndio maana tangu Rais Samia alipoingia tu, ameanza vizuri, mfano kitendo cha kuutengua uteuzi wa Dr. Bashiru kutoka Katibu Mkuu Kiongozi, na kumpa ubunge, japo ni demotion ya kistaarabu, lakini angalau amempooza kwa ubunge. Kiukweli Mama Samia ni muungwana sana na mstaarabu sana, mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuupongeza uamuzi huo, nikazitolea pongezi zangu hewani kupitia Sauti ya Ujerumani na BBC Swahili. Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021

Kwavile hili ni bandiko la life after life, yaani Magufuli huko aliko anayaona yote tunayawatendea aliowapenda, kama wakati wa Magufuli, sisi Watanzania, tuliwavumilia, na sasa wakati wa Samia, pia tuendelee tuwavumilie, na hata kama ni kuwaadhibu, Mungu anatufundisha tusilipize visasi, tusiwasulubishe kwa udhalilishaji kama alivyofanyiwa Ole Sabaya, kitendo cha kutoteuliwa, kutoka mtu uliekuwa everthing, then he is reduced to nobody ni adhabu tosha, itoshe, kwasababu no one knows kwa sasa kule mbinguni Magufuli amepewa wadhifa gani, inawezekana yuko karibu sana na Mungu, hivyo akiona jinsi tunavyowatendea wale aliowapenda kama Sabaya, akakasirika na kumuomba Mungu, awaite baadhi ya watu!. Kama yeye mwenyewe aliweza kuitwa na sasa hayupo, then anyone anaweza kuitwa anytime, lets not risk viongozi wengine kuitwa. Hao waliofanya uovu, baada ya kutoteuliwa, itoshe, tuiachie Karma iendelee kushughulika nao.

Nawaaga kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kazi Iendelee.

Paskali

Lilishachomwa moto lile shetani
 
Uislam hauamini mtu kuyaona yanayendelea duniani baada ya umauti.

Usiuchanganye na imani za Kikristo na kipagani. Ni tofauti kabisa.

Usukuma wako umeingua kwa sababh umstuletea mambo kama fikra na mila zako ulizokulia. Wasukuma si mnajulikana kina Mfalme Zumeradi na kuamini mambo ya kishirikina.uliyoyaandika yana akis usukuma.

Wewe msukuma na uliyemwandika msukuma, itakuwa mna imani kuonana mkifa.
Duh...!
Kumbe wengi hamjui kuwa Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja! Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!. hata hapa pia nomefundisha Je, Wajua Wakristo Wanawasindikizaga Waislamu Kufunga Ramadan?. Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tutafunga Siku 40, Vipi Waislamu Mtatusindikiza?

Adamu na Hawa ndio Adamu na Eva!
Nabii Ibrahim ndie Nabii Abraham
Isaka ndie Izhaq
Ishamel ndie Isumaili
Yakobo ndie Yakub
Joseph ndie Yusufu
Moses ndie Mussa
Yesu Kristo ndie Nabii Issa bin Maryam
Torati ndio Taurat
The Almighty God ndie Allah

Upige goti ujifunze Uislam, usichanganye Uislam na Ukristo, ni vitu tofauti kabisa.

Hata uwe baba na mama mmoja, huwezi kuhukumiwa wewe kwa kosa la ndugu yako, labda muwe mmeshirikiana hilo kosa.
. Usiulinganishe Uislam na Ukristo, ni vitu tofauti kabisa.
 
Upige gotu ujifunze Uislam, usichanganye Uislam na Ukristo, ni vitu tofauti kabisa.

Hatabuwe baba na mama mmoja, huwezinkuhujumiwa wewe kwa kosa ndugu yako labda muwe mmeshirikiana hilo kosa.
. Usiulinganishe Uislam na Ukristo, ni vitu tofauti kabisa.
Ni ufinyu tuu wa uelewa tuu, Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Nabii Ibrahim. Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail aliyemzaa na mjakazi wa Kimisri Hagir kwa ruhusa ya mkewe Sarah na Wakristo ni uzao wa mwanaye wa pili Isaka.

Sheria ya Mungu kwa dini zote mbili ni sheria moja ile ile ya Mussa iliyoshushwa kwenye Kumbukumbu la Torati.

Mungu wa Wakristo ndio huyo huyo Mungu wa Waislamu!.
Naomba hii sasa itoshe usije haribu bure Swaumu yako!.

Ufinyu wa uelewa wa wasukuma nani asiyeuelewa Tanzania hii?
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwa naweletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni kuhusu dhana ya kitu kinachoitwa "Life after Life", ambapo najikita kwenye maswali haya Je, wajua kuwa, binadamu hata baada ya kufa, bado anaendelea kuishi?. Mfano rais Magufuli, japo amekufa, ni amekufa kimwili tuu, ndio hatuko naye, lakini kiroho JPM, bado tuko nae, na huko alipo, bado yuko hai kiroho na kwa kutumia macho ya roho, anayaona mambo yote yanayoendelea kwenye Tanzania yake?.

Je, hiki tunachokifanya kwa baadhi ya wale aliowapenda, are we doing him right?, are we fair to him kwa hawa vijana wake?. Na kama issue ni viongozi waliofanya uovu kipindi cha awamu ya tano, wako wengi wamefanyiwa uovu, Ben Saanane alipotezwa baada ya kuposti kitu humu jf, Azory Gwanda alifuatwa na gari nyeupe ya mkonga ikampeleka hadi shambani kuchukua ufunguo wa nyumba kwa mkewe, wakaenda nae kwake kumpekua, wakaondoka nae and that is the end of him, hakuna majambazi yoyote yanamchukua mtu na kwenda kumpekua kisha kutokomea nae!.

Tundu Lissu alipigwa risasi mchana kweupe kwenye eneo la high security area huku likilindwa na CCTV, mpaka leo hakuna taarifa zozote za uchunguzi. Kumetokea matukio mengi tuu ya kutisha na kusikitisha yaliyotokea Awamu ya 5, swali ni je tuendelee kuwashughulikia kwa double standards kwa kutumia mfumo wa cherry picking kwa kuchagua baadhi tuu wa kushughulikia na wengine kuwa spaired, au tuiachie karma ndio iwashughulikie? kwasababu kwenye karma, hakuna mswalie Mtume, kila jiwe litapinduliwa!.

Muumini wa Karma na After Life
Naomba kuanza kwa kujitambulisha kuwa mimi sio tuu ni muumini wa karma, pia ni muumini wa after life na reincarnation. Hivyo rais Magufuli japo ametutoka na hatupo nae tena, ametutoka kimwili tuu, lakini kiroho bado tuko nae, na huko alipo anayaona yote yanayoendelea baada ya yeye kutangulia mbele ya haki, na anaona jinsi mnavyowatenda baadhi ya viongozi vipenzi wake kwa kuwa persecute kwa kuwa prosecute, kwa kuwadhalilisha!, Jee huku ndiko kumuenzi? Suppose yeye mwenyewe angekuwepo hai, na madudu ya Ole Sabaya yakaibuliwa, Jee Ole Sabaya angetendwa alivyo tendwa majuzi?. Hivi hatuwezi kumprosecute mtu with dignity?. Mjue Magufuli huko aliko bado yupo na anaona yote tunavyowatenda watu watu, asije akakasirika na akamlilia Mungu, watu wengine wakaitwa!.

Mimi na utetezi za haki za binaadamu, sikuanza leo, nilipigania adhabu ya kifo ifutwe, hata wahalifu, watesaji na wauwaji wanastahi kutendewa haki na dignity!
Naomba kujitanabaisha kuwa mimi ni mtetezi huru wa haki za binaadamu, humu jf nina mabandiko zaidi ya 100 ya utetezi wa haki, na kwenye gazeti la Mwananchi la kila Jumatano, na Nipashe la kila Jumapili, nina safu ninaandika makala za utetezi wa haki za binaadamu. Japo siungi mkono matendo ya kihalifu au uhalifu wa aina yoyote, ukiwemo uhalifu wa Ole Sabaya, lakini siungi mkono udhalilishaji wa aina yoyote anaofanywa na jeshi la polisi, magereza, vyombo vya uchunguzi, ofisi ya DPP, na vyombo vya utoaji haki, mahakama, mfano jana pale Mahakamani, Ole Sabaya ameletwa huku amefungwa pingu, as if ni kibaka! Kama haitoshi, akachuchumalishwa as if kumzuia asitoroke!. Huu ni udhalilishaji, huyu ni mmoja wa viongozi vipenzi wa JPM. Kabla hajateuliwa DC, alikuwa anakabiliwa na kesi mbaya ya jinai kufanya tukio la kihalifu kwa kujifanya TISS, JPM akamnasua kwa kumteua kuwa DC ikabidi DPP akaifuta hiyo kesi kwa nolle. Sasa kwa vile kuna ahadi ya kumuenzi JPM kwa mazuri yake, then tumuenzi kwa mtindo wa boga, ukipenda boga, penda na ua lake, na kwasababu sasa JPM hayupo, tukiamua kuwatupa watu wake, then tuwatupe kwa kutumia mtindo wa kumtupa jongoo, ukitupa jongoo, usitupe na mti wake!. Kama tulimpenda JPM, na tukaahidi kumuenzi, then tuwapende na watu wake aliowapenda, hivyo Ole Sabaya, awe treated fairly with dignity huku tukikumbuka kuwa Magufuli anayaona yote tunavyowatenda viongozi vijana wake!, huko aliko, asije akakasirika, akamlilia Mungu, watu wakaitwa bure!.

Life after life in Christianity: Mwili wa nyama ndio unakufa na kugeuka mvumbi, mwili wa roho, haufi, na unaishi milele!.
Hii dhana ya after life, karma and reincarnation sio dhana ya kwenye imani ya dini kuu mbili, za Kikirsto na Kiislamu, hii ni dhana ya dini ya Hinduism na Budhism ila kwenye ukiristo pia ipo.

Uhai ni nini na kifo ni nini?
Mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa udongo ukapuliziwa pumzi ya uhai, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni roho, life force, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astral body, mwili wa nyama unapokufa, roho haifi, bali roho huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha mtu kukata roho ni kitendo cha roho kuacha mwili, hiyo roho, haifi bali inatoka na ndio inayokwenda mbinguni mbele ya Mungu, ndiyo inayohukumiwa, ndio inayokaa peponi au motoni.

Je, baada ya kifo, hiyo Roho inakwenda kuishi wapi?
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili na roho, mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendelea kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye ziwa la moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu. Hivyo mwili huo wa roho, unaona kila kitu kinachoendelea hapa duniani.

Ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayo fufuliwa ni miili ya roho, ile miili ya nyama ikiisha zikwa, that is the end
Wakristu tunakitu tunaita fumbo la imani, tunaamini Yesu alikufa, Yesu alifufuka na Yesu atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho, ambapo kutatokea ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayohusika kwenye ufufuko wa miili ni miili ya roho na sio hii miili ya nyama. Kuna wengi pale wapendwa wetu wanapokufa, tunawazika kaburini, na kwa kadri ya uwezo, mwili unavishwa vizuri, kaburi linajengwa vizuri, na kuna watu huenda makaburini kufanya ibada za wafu, bila kujijua, hivyo wale wanaochoma miili kuonekana kama hawamtendei haki marehemu, ukweli ni kwamba, roho ikiisha acha mwili, that is the end of body, mwili hauna issue tena, unarudi mavumbini, mambo yote ni roho. Hivyo ninaposema Magufuli yupo na anaona kila kitu, ni kweli yupo na anaona.

Jee Roho za Waliokufa Huweza Kurejea Duniani?.
Yes, kwanza kwa wale wanaokufa katika mazingira ya kutatanisha, miili yao isipatikane wakazikwa rasmi, baadhi yao roho zao hubaki duniani, zikitanga tanga na sometimes zikisumbua, hizi zinaitwa "wondering spirits", kuna baadhi ya majumba hayakaliki kwasababu kuna roho zinasumbua, majumba haya huitwa "hauted houses". Kuna baadhi ya wafu huwatokea walio wazima ama kwenye ndoto, ama kwa visions kama Bikira Maria alivyowatokea wale watoto kule Fatima, Louedes Ufaransa. Mara nyingi wafu hurejea kama mizimu, hivyo kuna wengi wanalindwa na mababu bila ya wao kujijua, uthibitisho ni vitu vinavyoitwa miraculous escapes, inatokea ajali mbaya ya kutisha, gari linabondeka na kuwa chapati, halafu unakuta watu wametoka wazima, hata scratch hawana!.

Je, kwenye ahadi ya kumuenzi Magufuli tumuenzi kwa yote au tuchague mazuri tu?
Kwavile rais Magufuli hakuwa malaika, alikuwa ni binadamu, hivyo ana mazuri yake, na pia ana mabaya yake ya kibianadamu kama binaadamu mwingine yoyote, hakuna aliye mkamilifu, hivyo tumuenzi Magufuli kwa mema na mazuri yake kwa kuyaendeleza, halafu yale ya kibinaadamu, tumuachie mwenyewe, tuwe tumemzika nayo siku ile pale Chato na tusiyazungumzie mabaya yake ili kuepuka kumzungumzia vibaya marehemu, ili kumuacha marehemu apumzike kwa amani, ila kwenye kuzungumzia mabaya hayo kwa lengo la kutoa angalizo kwa kuwasaidia waliopo ili yale mabaya hatarishi yenye bad karmic consequenses yaepukwe, yasije yakajirudia, tukaja kujikuta tunapoteza wengine, maana karma haijui cha nani wala nani, ikifika stage ya karma kula kichwa, karma inakula kichwa!. Kwa vile tuna wazee wa kusoma karma trends humu, tunawajibu wa kuwasaidia viongozi wetu, waliongoze vizuri taifa letu kwa kuepuka kufanya makosa ya nyuma.

Baada ya Bwana Yesu kufa kwa mateso ya kusulubiwa na kifo msalabani, wanafunzi wake walijifungia kwa kuhofia na wao kusulubiwa, ndivyo ilivyo kwa Baadhi ya Watu wa Magufuli
Vivyo hivyo baada ya kifo cha Magufuli, kuna baadhi ya watu walilia kwa mengi wakiwemo wamachinga, Magufuli aliwaruhusu kufanya biashara popote, matokeo yake kwenye baadhi ya maeneo sasa ni balaa!. Siku Wamachinga wakiondolewa, watalia tena na kumkumbuka Magufuli, na wao pia watauliza kama kufukuzwa kwao ndiko kumuenzi Magufuli?. Ili kuwaelimisha watu wa aina hii, ni lazima waelimishwe kuwa hata Magufuli hakuwa mkamilifu, ataenziwa kwa mazuri tuu, hili la kuwaruhusu machinga kufanyabiashara popote, sii miongoni mwa mazuri ya kuenziwa, bali watawekewa utaratibu rasmi wa machinga kufanyabiashara bila kuwa kero kwa wengine.

Vivyo hivyo kwenye wateule wa JPM, kuna baadhi ya viongozi Magufuli aliwapenda sana, matokeo yake wakavimba vichwa, wakajiona kama miungu watu, wanaweza kufanya lolote na wasifanywe chochote, na hawakuamini kama Magufuli naye ni binadamu tuu, leo yupo, kesho anaweza asiwepo, au anaweza kufa. Mmoja wa wa watu hawa ni Comred Ole Sabaya, siku ya mazishi ya Magufuli, mmoja kati ya waliolia sana ni Ole Sabaya, inawezekana alilia kwa mengi, uchungu wa kufiwa na mtu unaempenda sana, au wasiwasi wa nini kitampata baada ya nguzo na egemeo lake kuanguka, ndio maana mkamuona akifanya juhudi kubwa, ikiwemo kwenda Clouds kujisafisha, but very unfortunately, haikusaidia, sasa yuko korokoroni aki treatiwa kama kibaka!.

Viongozi wahalifu kipindi cha Awamu ya Tano ni wengi, sio Sabaya pekee. Kama tumeamua kushughulika nao, tuwashughulikie wote
Kwenye awamu ya Tano, viongozi waliotenda mambo ya ajabu ajabu ni wengi, sio Ole Sabaya peke yake, kama awamu hii ya 6 ya Mama Samia, imeamua kuwashughulikia, then iwashughulikie wote. Tuache kufanya double standard ya cherry picking kuwashughulikia baadhi, na kuwaacha wengine, tena baadhi yao Mama Samia kaamua kuendelea kuwabeba mfano mzuri ni RC mmoja alimuamuru RPC wake kuwa namna ya kupunguza msongamano magerezani, ni kuwapiga risasi na kuwaua papo hapo vibaka wote!, na kujiproud kwa ushujaa wake jinsi alivyo muua kibaka kwa kumpiga risasi mbili za kichwa na kumuua papo hapo, kisha akajipongeza kwa kunywa bia mbili!.

Rais Mama Samia Kaanza Vizuri, Angeweza Kuibwaga Mizigo Yote ya Magufuli, Lakini Kafanya Uungwana Mkubwa ya Kuwatumbua, Kiungwana na Kistaarabu huku Akiwapooza Baadhi
Kwa vile kuna viongozi Rais Magufuli aliwapenda, Rais Mama Samia halazimiki kuwapenda, ndio maana tangu Rais Samia alipoingia tu, ameanza vizuri, mfano kitendo cha kuutengua uteuzi wa Dr. Bashiru kutoka Katibu Mkuu Kiongozi, na kumpa ubunge, japo ni demotion ya kistaarabu, lakini angalau amempooza kwa ubunge. Kiukweli Mama Samia ni muungwana sana na mstaarabu sana, mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuupongeza uamuzi huo, nikazitolea pongezi zangu hewani kupitia Sauti ya Ujerumani na BBC Swahili. Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021

Kwavile hili ni bandiko la life after life, yaani Magufuli huko aliko anayaona yote tunayawatendea aliowapenda, kama wakati wa Magufuli, sisi Watanzania, tuliwavumilia, na sasa wakati wa Samia, pia tuendelee tuwavumilie, na hata kama ni kuwaadhibu, Mungu anatufundisha tusilipize visasi, tusiwasulubishe kwa udhalilishaji kama alivyofanyiwa Ole Sabaya, kitendo cha kutoteuliwa, kutoka mtu uliekuwa everthing, then he is reduced to nobody ni adhabu tosha, itoshe, kwasababu no one knows kwa sasa kule mbinguni Magufuli amepewa wadhifa gani, inawezekana yuko karibu sana na Mungu, hivyo akiona jinsi tunavyowatendea wale aliowapenda kama Sabaya, akakasirika na kumuomba Mungu, awaite baadhi ya watu!. Kama yeye mwenyewe aliweza kuitwa na sasa hayupo, then anyone anaweza kuitwa anytime, lets not risk viongozi wengine kuitwa. Hao waliofanya uovu, baada ya kutoteuliwa, itoshe, tuiachie Karma iendelee kushughulika nao.

Nawaaga kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kazi Iendelee.

Paskali
Utakuwa umetenda haki kama utaandika uzi kama huu huu wenye kumhusu Julius Nyerere Rais wa kwanza wa Tanzania.

Magufuli ni rais wa tano ametanguliwa na wanne kabla. Je, wasaidizi wa Nyerere na wao walitendewa haki?. Je tuliweza kumuenzi Julius Nyerere kwa vitendo akiwa mwasisi wetu?.

Magufuli ni matunda ya awamu ya Nyerere na Mwinyi, ndio wale waliosomeshwa bure miaka ile ya 1960 na 1970, tungeanza kwanza kupeleka mawazo kama hayo katika awamu ya kwanza.
 
JPM kama ni kusoma bure ni primary tuu!. Sekondari alisomea shule ya kulipia ya Seminar ya Katoke, akafukuzwa Shule na Rector wa seminary hiyo enzi hizo Padri Severino Niwemugizi kwa kosa fulani!. Akahamia Lake Sec ya Mwanza ni sekondari ya kulipia!.

P
 
KIGOGO2014 (DIDIER MLAWA): KUTOKA UANAHARAKATI WA MTANDAONI HADI UTAPELI​

APRIL 5, 2023BY MKUFI DINDAI
KIGOGO2014 (DIDIER MLAWA): KUTOKA UANAHARAKATI WA MTANDAONI HADI UTAPELI

SHARE THIS POST?​

FacebookTwitterPinterest
Kuanzia mwaka 2019, jina Kigogo2014 lilijipatia umaarufu mkubwa na wafuasi wengi wa mtandaoni nchini Tanzania. Kigogo2014 ambaye jina lake halisi ni Didier Mlawa alijizolea umaarufu huo kwa machapisho yake ya utetezi wa demokrasia, haki za binadamu na ubadhirifu chini ya utawala wa Rais John Magufuli. Uanaharakati wake huo ukamjengea maadui wakubwa kwenye utawala wa Magufuli ikabidi aikimbie Tanzania na kupewa hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza. Kwa mujibu wa sheria za Uingereza, kiasi fulani cha fedha zake za kujikimu na kodi ya nyumba anakipata kutoka katika ruzuku ya serikali ya nchi hiyo ambayo kimsingi ni fedha za walipakodi wa Uingereza. Mbali na Uingereza, amepokea pia misaada kutoka shirika la Marekani la Ford Foundation.
Machi 17, 2021 Tanzania ilikumbwa na msiba mkubwa kitaifa Rais John Magufuli alipofariki akiwa madarakani. Siku mbili baadaye, Machi 19, Makamu wake, Samia Suluhu akaapishwa kuwa Rais na mambo yakaanza kubadilika. Rais mpya akaanza mazungumzo na wapinzani, akawatoa wengine gerezani na kuwafutia mashtaka. Wafanyabiashara ambao nao walikuwa wameteswa na kukwapuliwa hela zao wakati wa Magufuli pasi haki wakarudishiwa amana zao. Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa pia ikaruhusiwa tena. Kutokana na hatua hizi za Rais mpya kuipa nchi uponyaji wa kisiasa na haki, waliokuwa wameikimbia Tanzania wakaanza kurudi.
Hata hivyo licha ya maendeleo hayo mazuri kwenye haki za kibinadamu ambayo Rais Samia alikuwa ameanza kuonesha, Mlawa aliendelea kuipinga serikali ya Tanzania kama vile hakuna lililokuwa limebadilika. Mtazamo wake huo ukadumu kwa miezi michache kisha ghafla akaanza kuwa mtetezi wa serikali. Kutokana na umaarufu aliokuwa nao mtandaoni, kubadilika kwake huku kukaonekana kama usaliti na kuwa amefika bei na kununuliwa na serikali na wanasiasa Tanzania.
Licha ya kubadilika na kuwa mtetezi wa serikali, Mlawa hakurudi rasmi Tanzania kama vile ambavyo wakimbizi wenzake wa kisiasa walikuwa wanafanya na badala yake akaanza kuja Tanzania kisiri. Toka Rais Samia aingie madarakani, Mlawa amefika Tanzania mara tatu. Mara zote tatu amekuwa akikutana na wanasiasa mbalimbali, wafanyabiashara na viongozi wa serikali. Katika mikutano hiyo amekuwa anauza “kukusemea vizuri” mitandaoni kama bidhaa kwa kiasi kikubwa cha fedha. Unamlipa kukusema vizuri kwenye mitandao, kukupamba na pia kuwasemea vibaya mahasimu wako kwa propaganda mbalimbali.
Hata hivyo, wachambuzi wanauliza inakuwaje Mlawa anakuwa na uthubutu wa kuingia Tanzania nchi ambayo aliondoka na kuomba hifadhi Uingereza akisema si salama kwake? Je! Uingereza inachukuliaje mwenendo wake huu?
Jibu ni hilo kwamba amekuwa akiingia nchini kwa kificho, kuwaficha Idara ya Uhamiaji ya Uingereza kwamba haji Tanzania bali Kenya. Anachofanya ni kuwa huaga Uingereza kuwa anakwenda Kenya. Akifika Kenya anachukua usafiri wa gari na kuvuka mpaka wa Kenya na Tanzania mara nyingi mpaka wa Horohoro mkoani Tanga. Anapovuka mpaka huwa hagongi muhuri katika pasipoti ili asionekane alikuja Tanzania. Baadhi ya wanaharakati wanaona jambo hili na utapeli mkubwa na uhalifu na sasa wanaishinikiza Idara ya Uhamiaji ya Uingereza kumfutia Mlawa hisani ya ukimbizi kuishi nchini Uingereza. Shirika la Marekani la Ford Foundation ambalo awali lilikuwa likimpa misaada tayari limemuondoa katika orodha yake ya wanufaika. Awali lilimpa msaada wa zaidi ya dola 15,000 (shilingi milioni 35).
Safari yake ya mwisho kuja Tanzania ilikuwa Januari mwaka huu kama ifuatavyo; Januari 5 mwaka huu aliondoka katika uwanja wa ndege wa Heathrow London akiwa abiria kwenye ndege namba QR006 ya shirika la Qatar Airways kuelekea Doha. Doha akabadili ndege na kuelekea Nairobi, Kenya, ndege namba QR1335 ya shirika hilo hilo. Alitua Nairobi Januari 6 saa moja na dakika 20 asubuhi. Kutoka Nairobi alitumia usafiri wa gari binafsi na kuvuka mpaka wa Horohoro, Tanga kisha kuingia Tanzania, bila kugonga pasipoti muhuri mpakani. Alikuja moja kwa moja hadi Dar es Salaam na kati ya tarehe 7 hadi 13 mwezi huo huo wa Januari alifanya mikutano ya kificho na wanasiasa na viongozi mbalimbali. Baada ya mikutano hiyo akarudi tena Nairobi kwa barabara. Nairobi akapanda ndege ya shirika la Qatar kurudi Uingereza kwa kupitia Doha. Aliondoka Nairobi tarehe 14 Januari saa nne usiku katika ndege namba QR005.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Mlawa (Kigogo) amejibadili toka kuwa mwanaharakati hadi kuwa tapeli na mhalifu wa mtandaoni. Mfano katika akaunti yake rasmi ya Twitter ya Kigogo2014 amejitangaza kwamba anazisemea vizuri kazi za Rais Samia Suluhu. Hata hivyo, uchunguzi unaonesha anazo akaunti zaidi ya 100 zikiwemo TanzaniaLeaks, Insightfactortz na Tanzania Whistleblowers Group ambazo amekuwa akizitumia kumshambulia Rais Samia, familia yake na serikali ya Tanzania. Utaratibu wake ni kwamba akishakushambulia katika akaunti hizo kwa propaganda huja kwa mlango wa nyuma na kuwaomba watu hao hao wampe fedha ili azishughulikie akaunti hizo ikiwemo kuzidukua kana kwamba si zake. Vyanzo vinaeleza kwamba huchukua kati ya shilingi milioni 10 hadi 50 na zaidi kwa vitendo hivyo ambavyo kimsingi ni uhalifu dhidi ya wahanga wake.
Pia anatoa huduma za kuwasemea vibaya maadui za wanasiasa. Anachofanya ni kupendekeza kwako kwamba fulani ni adui, au kupata taarifa za fulani ni adui yako kisha hukuomba fedha ili aweze kueneza propaganda na uongo dhidi ya huyo adui yako kisiasa au kwenye biashara. Mbali na haya, amevujisha pia taarifa nyingi za wanaharakati aliokuwa akifanya nao kazi na baadhi hivi sasa wanahofia uhai wao.
Ni dhahiri kwamba Kigogo sasa anajiingizia fedha kutoka kwa kazi hii aliyochagua na hatahitaji hisani ya kuishi Uingereza kwa msaada za walipakodi wa nchi hiyo. Pengine ni wakati sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania na Uingereza kuanza uchunguzi juu ya Mlawa ili hatua zichukuliwe ikiwemo Uingereza kumfutia hadhi ya ukimbizi wa kisiasa inayompa haki ya kuishi nchini Uingereza hivi sasa. Ni wakati pia wa umma kumpuuza jambo ambalo lilianza pale tu ilipoonekana wazi amenunuliwa na serikali.
Imran Mjanenga
Safarini Dodoma Tanzania
imjanenga@gmail.com

cc; @Pascalmayalla
MWALLA umeamua kumchana Kigogo.

Tuongezee nyama kidogo, maana kigogo alikuwa anafichua ya mvunguni, who were/are his sources?
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwa naweletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni kuhusu dhana ya kitu kinachoitwa "Life after Life", ambapo najikita kwenye maswali haya Je, wajua kuwa, binadamu hata baada ya kufa, bado anaendelea kuishi?. Mfano rais Magufuli, japo amekufa, ni amekufa kimwili tuu, ndio hatuko naye, lakini kiroho JPM, bado tuko nae, na huko alipo, bado yuko hai kiroho na kwa kutumia macho ya roho, anayaona mambo yote yanayoendelea kwenye Tanzania yake?.

Je, hiki tunachokifanya kwa baadhi ya wale aliowapenda, are we doing him right?, are we fair to him kwa hawa vijana wake?. Na kama issue ni viongozi waliofanya uovu kipindi cha awamu ya tano, wako wengi wamefanyiwa uovu, Ben Saanane alipotezwa baada ya kuposti kitu humu jf, Azory Gwanda alifuatwa na gari nyeupe ya mkonga ikampeleka hadi shambani kuchukua ufunguo wa nyumba kwa mkewe, wakaenda nae kwake kumpekua, wakaondoka nae and that is the end of him, hakuna majambazi yoyote yanamchukua mtu na kwenda kumpekua kisha kutokomea nae!.

Tundu Lissu alipigwa risasi mchana kweupe kwenye eneo la high security area huku likilindwa na CCTV, mpaka leo hakuna taarifa zozote za uchunguzi. Kumetokea matukio mengi tuu ya kutisha na kusikitisha yaliyotokea Awamu ya 5, swali ni je tuendelee kuwashughulikia kwa double standards kwa kutumia mfumo wa cherry picking kwa kuchagua baadhi tuu wa kushughulikia na wengine kuwa spaired, au tuiachie karma ndio iwashughulikie? kwasababu kwenye karma, hakuna mswalie Mtume, kila jiwe litapinduliwa!.

Muumini wa Karma na After Life
Naomba kuanza kwa kujitambulisha kuwa mimi sio tuu ni muumini wa karma, pia ni muumini wa after life na reincarnation. Hivyo rais Magufuli japo ametutoka na hatupo nae tena, ametutoka kimwili tuu, lakini kiroho bado tuko nae, na huko alipo anayaona yote yanayoendelea baada ya yeye kutangulia mbele ya haki, na anaona jinsi mnavyowatenda baadhi ya viongozi vipenzi wake kwa kuwa persecute kwa kuwa prosecute, kwa kuwadhalilisha!, Jee huku ndiko kumuenzi? Suppose yeye mwenyewe angekuwepo hai, na madudu ya Ole Sabaya yakaibuliwa, Jee Ole Sabaya angetendwa alivyo tendwa majuzi?. Hivi hatuwezi kumprosecute mtu with dignity?. Mjue Magufuli huko aliko bado yupo na anaona yote tunavyowatenda watu watu, asije akakasirika na akamlilia Mungu, watu wengine wakaitwa!.

Mimi na utetezi za haki za binaadamu, sikuanza leo, nilipigania adhabu ya kifo ifutwe, hata wahalifu, watesaji na wauwaji wanastahi kutendewa haki na dignity!
Naomba kujitanabaisha kuwa mimi ni mtetezi huru wa haki za binaadamu, humu jf nina mabandiko zaidi ya 100 ya utetezi wa haki, na kwenye gazeti la Mwananchi la kila Jumatano, na Nipashe la kila Jumapili, nina safu ninaandika makala za utetezi wa haki za binaadamu. Japo siungi mkono matendo ya kihalifu au uhalifu wa aina yoyote, ukiwemo uhalifu wa Ole Sabaya, lakini siungi mkono udhalilishaji wa aina yoyote anaofanywa na jeshi la polisi, magereza, vyombo vya uchunguzi, ofisi ya DPP, na vyombo vya utoaji haki, mahakama, mfano jana pale Mahakamani, Ole Sabaya ameletwa huku amefungwa pingu, as if ni kibaka! Kama haitoshi, akachuchumalishwa as if kumzuia asitoroke!. Huu ni udhalilishaji, huyu ni mmoja wa viongozi vipenzi wa JPM. Kabla hajateuliwa DC, alikuwa anakabiliwa na kesi mbaya ya jinai kufanya tukio la kihalifu kwa kujifanya TISS, JPM akamnasua kwa kumteua kuwa DC ikabidi DPP akaifuta hiyo kesi kwa nolle. Sasa kwa vile kuna ahadi ya kumuenzi JPM kwa mazuri yake, then tumuenzi kwa mtindo wa boga, ukipenda boga, penda na ua lake, na kwasababu sasa JPM hayupo, tukiamua kuwatupa watu wake, then tuwatupe kwa kutumia mtindo wa kumtupa jongoo, ukitupa jongoo, usitupe na mti wake!. Kama tulimpenda JPM, na tukaahidi kumuenzi, then tuwapende na watu wake aliowapenda, hivyo Ole Sabaya, awe treated fairly with dignity huku tukikumbuka kuwa Magufuli anayaona yote tunavyowatenda viongozi vijana wake!, huko aliko, asije akakasirika, akamlilia Mungu, watu wakaitwa bure!.

Life after life in Christianity: Mwili wa nyama ndio unakufa na kugeuka mvumbi, mwili wa roho, haufi, na unaishi milele!.
Hii dhana ya after life, karma and reincarnation sio dhana ya kwenye imani ya dini kuu mbili, za Kikirsto na Kiislamu, hii ni dhana ya dini ya Hinduism na Budhism ila kwenye ukiristo pia ipo.

Uhai ni nini na kifo ni nini?
Mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa udongo ukapuliziwa pumzi ya uhai, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni roho, life force, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astral body, mwili wa nyama unapokufa, roho haifi, bali roho huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha mtu kukata roho ni kitendo cha roho kuacha mwili, hiyo roho, haifi bali inatoka na ndio inayokwenda mbinguni mbele ya Mungu, ndiyo inayohukumiwa, ndio inayokaa peponi au motoni.

Je, baada ya kifo, hiyo Roho inakwenda kuishi wapi?
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili na roho, mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendelea kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye ziwa la moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu. Hivyo mwili huo wa roho, unaona kila kitu kinachoendelea hapa duniani.

Ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayo fufuliwa ni miili ya roho, ile miili ya nyama ikiisha zikwa, that is the end
Wakristu tunakitu tunaita fumbo la imani, tunaamini Yesu alikufa, Yesu alifufuka na Yesu atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho, ambapo kutatokea ufufuko wa miili na uzima wa milele, miili itakayohusika kwenye ufufuko wa miili ni miili ya roho na sio hii miili ya nyama. Kuna wengi pale wapendwa wetu wanapokufa, tunawazika kaburini, na kwa kadri ya uwezo, mwili unavishwa vizuri, kaburi linajengwa vizuri, na kuna watu huenda makaburini kufanya ibada za wafu, bila kujijua, hivyo wale wanaochoma miili kuonekana kama hawamtendei haki marehemu, ukweli ni kwamba, roho ikiisha acha mwili, that is the end of body, mwili hauna issue tena, unarudi mavumbini, mambo yote ni roho. Hivyo ninaposema Magufuli yupo na anaona kila kitu, ni kweli yupo na anaona.

Jee Roho za Waliokufa Huweza Kurejea Duniani?.
Yes, kwanza kwa wale wanaokufa katika mazingira ya kutatanisha, miili yao isipatikane wakazikwa rasmi, baadhi yao roho zao hubaki duniani, zikitanga tanga na sometimes zikisumbua, hizi zinaitwa "wondering spirits", kuna baadhi ya majumba hayakaliki kwasababu kuna roho zinasumbua, majumba haya huitwa "hauted houses". Kuna baadhi ya wafu huwatokea walio wazima ama kwenye ndoto, ama kwa visions kama Bikira Maria alivyowatokea wale watoto kule Fatima, Louedes Ufaransa. Mara nyingi wafu hurejea kama mizimu, hivyo kuna wengi wanalindwa na mababu bila ya wao kujijua, uthibitisho ni vitu vinavyoitwa miraculous escapes, inatokea ajali mbaya ya kutisha, gari linabondeka na kuwa chapati, halafu unakuta watu wametoka wazima, hata scratch hawana!.

Je, kwenye ahadi ya kumuenzi Magufuli tumuenzi kwa yote au tuchague mazuri tu?
Kwavile rais Magufuli hakuwa malaika, alikuwa ni binadamu, hivyo ana mazuri yake, na pia ana mabaya yake ya kibianadamu kama binaadamu mwingine yoyote, hakuna aliye mkamilifu, hivyo tumuenzi Magufuli kwa mema na mazuri yake kwa kuyaendeleza, halafu yale ya kibinaadamu, tumuachie mwenyewe, tuwe tumemzika nayo siku ile pale Chato na tusiyazungumzie mabaya yake ili kuepuka kumzungumzia vibaya marehemu, ili kumuacha marehemu apumzike kwa amani, ila kwenye kuzungumzia mabaya hayo kwa lengo la kutoa angalizo kwa kuwasaidia waliopo ili yale mabaya hatarishi yenye bad karmic consequenses yaepukwe, yasije yakajirudia, tukaja kujikuta tunapoteza wengine, maana karma haijui cha nani wala nani, ikifika stage ya karma kula kichwa, karma inakula kichwa!. Kwa vile tuna wazee wa kusoma karma trends humu, tunawajibu wa kuwasaidia viongozi wetu, waliongoze vizuri taifa letu kwa kuepuka kufanya makosa ya nyuma.

Baada ya Bwana Yesu kufa kwa mateso ya kusulubiwa na kifo msalabani, wanafunzi wake walijifungia kwa kuhofia na wao kusulubiwa, ndivyo ilivyo kwa Baadhi ya Watu wa Magufuli
Vivyo hivyo baada ya kifo cha Magufuli, kuna baadhi ya watu walilia kwa mengi wakiwemo wamachinga, Magufuli aliwaruhusu kufanya biashara popote, matokeo yake kwenye baadhi ya maeneo sasa ni balaa!. Siku Wamachinga wakiondolewa, watalia tena na kumkumbuka Magufuli, na wao pia watauliza kama kufukuzwa kwao ndiko kumuenzi Magufuli?. Ili kuwaelimisha watu wa aina hii, ni lazima waelimishwe kuwa hata Magufuli hakuwa mkamilifu, ataenziwa kwa mazuri tuu, hili la kuwaruhusu machinga kufanyabiashara popote, sii miongoni mwa mazuri ya kuenziwa, bali watawekewa utaratibu rasmi wa machinga kufanyabiashara bila kuwa kero kwa wengine.

Vivyo hivyo kwenye wateule wa JPM, kuna baadhi ya viongozi Magufuli aliwapenda sana, matokeo yake wakavimba vichwa, wakajiona kama miungu watu, wanaweza kufanya lolote na wasifanywe chochote, na hawakuamini kama Magufuli naye ni binadamu tuu, leo yupo, kesho anaweza asiwepo, au anaweza kufa. Mmoja wa wa watu hawa ni Comred Ole Sabaya, siku ya mazishi ya Magufuli, mmoja kati ya waliolia sana ni Ole Sabaya, inawezekana alilia kwa mengi, uchungu wa kufiwa na mtu unaempenda sana, au wasiwasi wa nini kitampata baada ya nguzo na egemeo lake kuanguka, ndio maana mkamuona akifanya juhudi kubwa, ikiwemo kwenda Clouds kujisafisha, but very unfortunately, haikusaidia, sasa yuko korokoroni aki treatiwa kama kibaka!.

Viongozi wahalifu kipindi cha Awamu ya Tano ni wengi, sio Sabaya pekee. Kama tumeamua kushughulika nao, tuwashughulikie wote
Kwenye awamu ya Tano, viongozi waliotenda mambo ya ajabu ajabu ni wengi, sio Ole Sabaya peke yake, kama awamu hii ya 6 ya Mama Samia, imeamua kuwashughulikia, then iwashughulikie wote. Tuache kufanya double standard ya cherry picking kuwashughulikia baadhi, na kuwaacha wengine, tena baadhi yao Mama Samia kaamua kuendelea kuwabeba mfano mzuri ni RC mmoja alimuamuru RPC wake kuwa namna ya kupunguza msongamano magerezani, ni kuwapiga risasi na kuwaua papo hapo vibaka wote!, na kujiproud kwa ushujaa wake jinsi alivyo muua kibaka kwa kumpiga risasi mbili za kichwa na kumuua papo hapo, kisha akajipongeza kwa kunywa bia mbili!.

Rais Mama Samia Kaanza Vizuri, Angeweza Kuibwaga Mizigo Yote ya Magufuli, Lakini Kafanya Uungwana Mkubwa ya Kuwatumbua, Kiungwana na Kistaarabu huku Akiwapooza Baadhi
Kwa vile kuna viongozi Rais Magufuli aliwapenda, Rais Mama Samia halazimiki kuwapenda, ndio maana tangu Rais Samia alipoingia tu, ameanza vizuri, mfano kitendo cha kuutengua uteuzi wa Dr. Bashiru kutoka Katibu Mkuu Kiongozi, na kumpa ubunge, japo ni demotion ya kistaarabu, lakini angalau amempooza kwa ubunge. Kiukweli Mama Samia ni muungwana sana na mstaarabu sana, mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuupongeza uamuzi huo, nikazitolea pongezi zangu hewani kupitia Sauti ya Ujerumani na BBC Swahili. Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021

Kwavile hili ni bandiko la life after life, yaani Magufuli huko aliko anayaona yote tunayawatendea aliowapenda, kama wakati wa Magufuli, sisi Watanzania, tuliwavumilia, na sasa wakati wa Samia, pia tuendelee tuwavumilie, na hata kama ni kuwaadhibu, Mungu anatufundisha tusilipize visasi, tusiwasulubishe kwa udhalilishaji kama alivyofanyiwa Ole Sabaya, kitendo cha kutoteuliwa, kutoka mtu uliekuwa everthing, then he is reduced to nobody ni adhabu tosha, itoshe, kwasababu no one knows kwa sasa kule mbinguni Magufuli amepewa wadhifa gani, inawezekana yuko karibu sana na Mungu, hivyo akiona jinsi tunavyowatendea wale aliowapenda kama Sabaya, akakasirika na kumuomba Mungu, awaite baadhi ya watu!. Kama yeye mwenyewe aliweza kuitwa na sasa hayupo, then anyone anaweza kuitwa anytime, lets not risk viongozi wengine kuitwa. Hao waliofanya uovu, baada ya kutoteuliwa, itoshe, tuiachie Karma iendelee kushughulika nao.

Nawaaga kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kazi Iendelee.

Paskali
Wewe Sukuma Gang tulishakupuuza na kwa taarifa yako hata ulie hupati uteuzi ng'o!!
 
Wanabodi,
Magufuli huko aliko anayaona yote tunayawatendea aliowapenda, kama wakati wa Magufuli, sisi Watanzania, tuliwavumilia, na sasa wakati wa Samia, pia tuendelee tuwavumilie, na hata kama ni kuwaadhibu, Mungu anatufundisha tusilipize visasi, tusiwasulubishe kwa udhalilishaji kama alivyofanyiwa Ole Sabaya, kitendo cha kutoteuliwa, kutoka mtu uliekuwa everthing, then he is reduced to nobody ni adhabu tosha, itoshe, kwasababu no one knows kwa sasa kule mbinguni Magufuli amepewa wadhifa gani, inawezekana yuko karibu sana na Mungu, hivyo akiona jinsi tunavyowatendea wale aliowapenda kama Sabaya, akakasirika na kumuomba Mungu, awaite baadhi ya watu!. Kama yeye mwenyewe aliweza kuitwa na sasa hayupo, then anyone anaweza kuitwa anytime, lets not risk viongozi wengine kuitwa. Hao waliofanya uovu, baada ya kutoteuliwa, itoshe, tuiachie Karma iendelee kushughulika nao..

Paskali
Asingeachiwa ingekuaje
Read read read.
Ukiona bado hujaelewa nitakuelewesha
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwa naweletea makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni kuhusu dhana ya kitu kinachoitwa "Life after Life", ambapo najikita kwenye maswali haya Je, wajua kuwa, binadamu hata baada ya kufa, bado anaendelea kuishi?. Mfano rais Magufuli, japo amekufa, ni amekufa kimwili tuu, ndio hatuko naye, lakini kiroho JPM, bado tuko nae, na huko alipo, bado yuko hai kiroho na kwa kutumia macho ya roho, anayaona mambo yote yanayoendelea kwenye Tanzania yake?.
Paskali
Hata huku kufutwa kwa jina lake kwenye Stendi ya Magufuli, Magufuli mwenyewe huko Aliko anaona, na ule msemo wa " First impression lasts longer", then Standi ya Magufuli, japo imebadilishwa jina, lakini Itaendelea kuitwa ni stendi ya Magufuli, mioyoni mwa watu kwa miaka mingi ijayo, hadi pale his legacy itakapofutika kwa kizazi kijacho ambacho hakijawahi kumjua Magufuli.
P
 
Back
Top Bottom