Life during Apartheid in South Africa

Bwana unajitahidi lkn unachagua picha hovyo. Hii hapa juu si Afrika Kusini, ni picha kutoka Marekani. Bao za aina hii zilitumiwa mjini Montgomery, Alabama (inawezekana pia penginepo, lakini mfano huu ni wa Montgomery). Mwaka 1955 Rosa Parks alikataa kuitikia amri ya dereva kumwachia kiti chake mtu mweupe akakamatwa na hii ilikuwa chanzo cha ugomwi wa kupigania haki za wamarekani weusi uliongozwa na ML King.
Sare ya mwanajeshi ni pia ya Kimarekani.
 
Katika tembea yangu pande mbalimbali za ulimwengu ingawa ubaguzi kama unavyosimuliwa enzi hizo zilizopita kihistoria haupo , bado zama zetu hizi huona sisi watu wa asili ya kiafrika bado twapenda kukaa siti za nyuma siyo ktk mabasi tu pia hata katika mijadala hatujitokezi kama wengine kwa wingi.

Wenzetu wana kina PLO Lumumba kibao ktk mijadala mizito ya kijamii, sayansi, teknolojia, saikolojia ,anga za Juu (space), n.k ila siye wamatumbi tuna wachache sana pamoja na usomi wa ngazi zote mpaka PhD waafrika wapo kibao. .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…