Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Deva

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
1,238
Reaction score
1,812
Moja kwa moja niende katika mada.

Leo asubuhi kama kawaida yangu kuna mahali huwa naenda kunywa chai, ni mgahawa wa jamaa yangu mmoja wa karibu, nimekunywa chai, nilipomaliza nikaona kuna funguo juu ya meza, ambazo ninafahamu ni za jamaa yangu(Nimeshazitumia mara kadhaa kukatia kucha kwa maana zina nail cutter), nikatumia katika kukata kucha.

Nilipomaliza kukata kucha nilipigiwa simu, nikasogea pembeni kuzungumza na simu, nikazungumza na simu kwa muda mrefu, hivyo sikuona umuhimu wa kurudi pale tena maana nimemaliza kunywa chai, kumbe wakati huo nimesahau funguo zile nimeziweka mfukoni, nilipofika nyumbani nimeendelea na shughuli zangu bila kuelewa chochote wala kukumbuka, nimekuja kupigiwa simu na binti kuwa kumbe zile funguo zinahitajika, ndio nikakumbuka kujisachi najikuta na funguo kuwa ninazo mfukoni, na kumbe si za jamaa yangu, kumpigia simu anasema si zake kweli, ni za binti anayefanya kazi hapo mgahawani, ni kwamba zimefanana, tukio hili limeniachia fedheha na aibu kubwa maana moja kwa moja nimeonekana kama nilikuwa nina hila mbaya, na hakuna yoyote ninayeweza kumueleza akaniamini, imebaki kuniuma mwenyewe rohoni, maana ningehusishwa na wizi.

Katika maisha kuna mambo ambayo yanatukuta kwa bahati mbaya bila sisi kutarajia, hayo mambo huwa yanapelekea aibu na fedheha ambayo haistahili kwa kweli, na hata haielezeki kwa mtu kirahisi.

Kama na wewe una kisa chochote tupe hapa tupate funzo kidogo.
 
We boya sana yani unakata mikucha yako na nail cutter za mtu mwingine magonjwa yote haya.

Mimi ilinikuta miaka kadhaa iliyopita ndio nimeajiriwa kwenye kampuni flani hapa Dar. Jioni nimekaa na mabosi zangu kupata wine kidogo na kujuana vizuri, tulikuwa tumeweka simu zetu mezani, bahati mbaya nikachukua simu ya bosi mmoja nikatia mfukoni nikijua ni yangu. Mara kidogo jamaa akaanza kuulizia simu yake mimi nimetulia tu nikiamini iliyopo mfukoni ni yangu.

Dah ilivyobipiwa ikaita kwangu halafu hata hawakunipa nafasi ya kujieleza zaidi ya kila mtu kutunza simu yake kwa umakini, nilijisikia fedheha haielezeki.
 
Niliwahi kwenda migahawa koko maeneo flani hivi nikakuta contena la kunawia mikono wameweka pembeni na nyumba ya mtu halafu mgahawa wenyewe uko mbali kidogo, mimi niliponawa nikaingia nyumba iliyokuwa jirani nikidhani ndio mgahawa wenyewe kumbe nimeingia kwenye geto la Mmama flani hivi.

Sasa muda naingia alikuwa bize anakula halafu kageukia upande wa pili wala hakusikia vishindo muda naingia kwa akili za kitoto nilipogundua kuwa nimeingia kusipo nikapata akili ya kutoka kimyakimya tena...! Kumbe muda natoka ndani yule mama akashtuka nikajifanya kuchomoka mule ndani kwa haraka ndio akaniitia mwizi..mwizi...mwizi asee nikajifanya kukimbia nikaishia mikononi mwa wananchi wenye hasira kali aisee sitakaa nisahau kilichonipata yaani kuna watu bongo hii hata ukiwa unatoa maelezo hawayazingatii wao ni kupiga tu na kutafuta petroli....

Hadi leo nikikuta mwizi anapigwa huwa napenda kusikiliza maelezo yake kama yanaleta logic....Maana ningechomwa moto na sijawahi kuiba wala kutapeli cha mtu!
 
Dah hii kweli fedheha.
 
Pole sana mkuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aise nimechekasana. Pole sana Mkuu
Mungu tu alikuokoa sidhani kama kuna mtu angekuelewa kirahisi kwa maelezo hayo.

[emoji23][emoji23][emoji28]
Dah watu unamatukio aisee.
 
Niliwahi kujamba mbele za wanafunzi wangu, nikiwa mbele ya wanafunzi wananisikiliza kwa umakini wa hali ya juu sasa hapo kijambo kikaja cha kimyakimya ..duh kumbe ilikuwaa inanuka hatari...niliona wengine walijuwa mimi halafu wingine wakamsingizia dogo flani ambae anajambagajamba ovyo duh nilijisikiaa ovyo kwelii....
 
Fedheha nnazozipataga mimi ni ndogo ndogo kwenye matumizi ya vyombo vya mzungu.
Kuna mabomba ufunguaji wake mrahisi ila kama hujui hangaika sana afu anakuja mtu tu anakufungulia kirahisi[emoji23]
Siku ya kwanza kupanda mwendokasi sijui kuscan ticket aibu tupu
Siku ya kwanza kutumia lift[emoji3] nk
Yani vitu vya aina hio ndo aibu nnazopataga
 
Siku moja mama mkwe aliniomba kiasi fulani cha hela mida kama saa sita mchana basi bila kusubiri nikaingia kwenye menu ya mobile banking nikamtumia, kama sekunde tano nikaona sms ya exim sikutaka hata kusoma nikaacha simu getini kwa mlinzi maana hatuingii na simu kazini kutokana na sensitivity ya process inayofanyika humo ndani.

Saa kumi jioni natoka nakuta missed calls kibao plus sms "mwanangu ninashida na hiyo pesa nitumie then nitakurudishia!". Nikashangaa hela si nimeshatuma tangia mchana!? Ile kucheki ile sms ya exim kumbe muamala ulifeli. Sikuwahi kufedheheka kama nilivyofedheheka ile siku kwa kuonekana mnyimi japo sikuambiwa hivyo.
 
Kuna siku nipo Hamad International Airport kule Doha Qatar, Nimeingia toilet nikajihudumia saafi kabisa sasa nimetoka ninawe mikono naona tuu kuna koki za maji ila hakuna cha kufungua ili kuruhusu maji yatoke. Basi nimesimama pale mara nishike hapa, kule, huku sioni hata kibatan cha kubonyeza tuu.....

Kumbe muda wote kuna muarabu ananipimia tuu ninavyombwela pale. Akaja kunielekeza kumbe mabomba yanatumia sensor ukisogeza tuu mkono ina activate valve inafungua maji... Jamaa aliondoka anaongea kiarabu hata sikumuelewa huku nikibaki nimetunukiwa fedheha iliyofanya hata safari niione ndefu.
 
Hatari mzee kwahiyo ukafanyaje???
 
Ilitokea nimekuja Dar kwa ndugu yangu aliepanga chumba maeneo ya uswahilini Temeke, nyumba ilikuwa na vijana na mama mwenye watoto wa kike pale, sasa ilitokea siku moja usiku nimeenda kuoga mida ya usiku nikaona sio mbaya nitoe na haja kubwa kabisa, kumbe nimemaliza kujisaidia na maji nimemwaga yalikuwa machache, asubuhi si ndo akaja mwenye zamu kufagia choo akaukatana nayo, kila akimwagia maji mzigo hausogei mbele ikabidi aulize tu ni nani alikuwa wa mwisho si ndo nikatajwa mimi.. daaahh ilikua fedheha kwa watoto wa kike wale maana mama alikazia neno 'Alafu yule kaka ni mwembamba ila ana mavi magumuuuuu' sikumsalimia mpaka namaliza likizo naondoka
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…