Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Hiyo ilinitokea miaka kama sita iliyopita, Sikh hiyo nimeenda ukweni kwa Mara ya kwanza kabisa, sasa lile wenge la kuonana na babamkwe( Wakati tunafika hakuwepo,alipiga simu yupo njiani anakuja) Basi nikawa naenda chooni kukojoa.

Ile nafika chooni nakuta kuna mzigo haujasukumwa, duh palepale nikaghairi kujisaidia ile nafungua mlango nitoke uso kwa uso na babamkwe,

A see hata domo lilikuwa zito maana lazima angejua ni Mimi ndiyo nimesababisha, ile anaingia naskia anafyonya. Acha kabisaaa.
🤣🤣🤣🤣
 
Kuna rafiki yangu wa kike (Sio Girlfriend) aliweka whtsp status ya rafiki yake mwanamke aliyevaa kimini na wkt hana ushepu, sasa mimi nikaichukua ile nikaituma ktk group la jamaa wa ofisini kulikuwa na mada kuhusu mavazi ya wanawake huku mie nikimtolea mfano huyo mdada pasipo kufahamu kuwa ni mke wa staff mwenzetu na yeye yupo ktk group. Mara paap naona washikaji wananitumia sms inbox kuwa kaka unaharibu, umepatwa na nn mbona unatolea mfano mke wa Flani amekukosea nini au umelewa upo vyombo hapo ulipo? Kumbe masikini ya Mungu mimi sikuwa nafahamu, jamaa naye akaja inbox akaniambia "Ahsante kaka nashukuru sana". Nilijisikia vibaya kila nikijaribu kum-please kuwa sikuwa najua jamaa hapokei simu wala hajibu sms, na kipindi kile whatsapp haikuwa na feature ya kudelete sms kama ilivyo sasa. Sitakuja sahau aisee hilo jambo..
Duh aseee
 
Niliwahi kushikwa tumbo la kuharisha ukweni
Ilikuwa hivi:
Kuna binti nkikuwaga namnyandua enzi hizo na alikuwaga ananisaidia mambo mengi sana miaka hiyo maana nilikuwa na maisha magumu kiaina
Sasa mahusiano yetu yakafikia binti kutaka akanitambulishe kwao ilikuwa wilaya tofauti.
Siku ikafika mwanaume huyo mpaka ukweni nafika naandaliwa msosi tukaanza kula
Kosa kubwa walilofanya kunipa maji ya kunywa yaliyowekwa water guard (enzi hizo ilikuwa dawa maarufu ya kuweka kwenye maji ya kunywa) sasa hiyo kitu huwa sipatani nayo nilipokunywa tu hayo maji nikasikia tumbo linaunguruma kama nimemeza chura wa bwawani!
Kilichofuata ni maumivu makali ya tumbo yakiambatana na kichefuchefu cha makalio(kubanwa kunya)
Nilijizuia nikashindwa kabisa ikabidi nimuombe binti anielekeze chooni ikabidi kustop kula nikanawa mikono haraka bahati nzuri sebureni tulikuwa tumeachwa watatu tu ndo tunakula nilikuwa mimi, binti na kidogo chao cha kiume hivyo tulitoka na binti ili anipeleke chooni ilikuwa choo cha uani.
Ile tunatoka nje ya nyumba kufika kule uani ambako ndiko kuna choo na vyumba vingine vya wapangaji tukakuta mama mkwe amekaa na wanawake wengine kama wanne nahisi ni wapangaji halafu walikuwepo na mabinti wengine mashemeji kama watatu yaani mbaya zaidi wamekaa pale pale karibu na mlango wa kuingia chooni wanasukana hapo na kupiga umbea waliponiona walijikausha nikapita kuingia chooni huku binti akibaki nao hapo nje ile nafunga mlango wa chooni tu nilisikia vicheko vya kisirisiri kwa nje nikajipa moyo kwamba ntavumilia tu hii aibu maana ishatokea
Mbaya zaidi ile nachuchumaa tu chooni niliharisha kinoma kiasi kwamba yalikuwa kama yanamwagika maji huku zinasikika sauti za mripuko kama radi nilijaribu kujibana nizuie hizo sauti za kujamba lakini zikawa kama ndo naongeza wakati huo huko nje nasikia vicheko vya wazi wazi kabisa iliniuma sana nilitamani nitokee juu ya paa nipotee kabisa eneo lile lakn haikuwezekana.
Nilimaliza kujisaidia naanza kujisafisha kulikuwa na maji kidogo kwenye ndoo yakaisha nikajaribu kufungulia bomba maji hayatoki nahisi yalikuwa yamekatika halafu hapo sijamwaga maji kwenye sinki la choo kinyesi kimejaa na kutapakaa kwenye sinki ikabidi nijitoe aibu nivae tu nitoke nikamuite binti pembeni nimwambie maji chooni hakuna ikiwezekana anisaidie kwenda kumwaga maji kabla hawajastukia lakn cha ajabu ile natoka tu nawakuta wale wadada wamekaa ila mamkwe na mchumba wangu sikuwakuta nahisi walikuwa ndani ikabidi nizame ndani huku nyuma bado nasikia vicheko watu wanacheka mpaka wanaanguka chini!
Nafika ndani namkuta yule dogo bado anakula nikamuuliza dadake yuko wapi akasema ameenda dukani mama mkwe naye sikumuona nahisi alijifungia chumbani kwa aibu!
Nikarudi pale uani ili nijitoe ufahamu niwaombe wanisaidie maji lakn kabla sijafanya hivyo namuona binti mmoja kati ya wale mashemeji zangu anatokea mule chooni na ndoo mkononi akapitiliza ndani akachota maji na kurudi chooni akaanza kusafisha chooni!
Ile kitendo ilinifanya nijiskie aibu ambayo sijawahi kuona!!!!
Kufupisha story nilijikuta nje ya geti ambako nilimuona mchumba wangu anarudi na kibahasha cha dawa mkononi akanipa eti alienda duka la dawa kuninunulia vidonge vya kuzuia kuharisha nilivimeza pale pale mlangoni nikaondoka sikutaka tena kurudi ndani maana sio kwa aibu ile.
Hii kali mkuu
 
Kuna shule nilikuwa nafundisha halafu wanafunzi wakawa wananicheka navyovaa, bahati mbaya kipindi hicho sikuwa na pesa kabisa, mavazi nikawa naungaunga tu.
Mkuu ulikuwa una vaa mashati makubwa na suruali kubwa?
 
Back
Top Bottom