Mwaka flani hv nimeenda zangu maeneo kumtembelea sister,siku hyo sister kasafiri nimebaki na anko 2,ilikuwa wikiend nikaenda zangu kucheki mpira narudi zangu mida kama ya saa 5 hv uck,narudi geti limefungwa,namgongea anko nae kalala kinouma nimekaa kama nusu SAA hv nagonga hakuna kufungua,nikaamua kufungua dirisha nipitie hapo,vile vidirisha vya zamani vinakuwa na nondo katikati aisee,so nikapiga hesabu nikaona kupita na nguo haiwezekani so nikavua nguo nikaziingiza ndani nikabaki na chupi 2 nikajua si napita fasta,
Ile kuanza kupitisha kichwa hakipiti kumbe ni padogo ,kasheshe likaanzia hapo,hangaika wapi, hangaika wapi nikaona jau hili,nikamkumbuka jamaa yangu anakaa mtaa wa pili,ikabidi nitoke pale kwa spidi kali nipo na kichupi 2 nakatiza mtaaan,wikiendi ile mitaa watu wanacjelewa sana kulala so nilikutana na watu wanacheka walijua nimetoka kufumaniwa so nakimbia soo,ile nafika kwa jamaa,jamaa kafungua kunikuta vile anacheka kishenzi,kwa soo lile sikukaa sana ilibidi nirudi home 2