Mshika Tester
Member
- May 3, 2020
- 38
- 35
- Thread starter
-
- #41
Mkuu kila upande una kanuni zake...upande wa Giza unakanuni zake na upande wa nuru una kanuni zake hakuna kitu kama fungu LA kukosa au fungu la kupata ...fata kanuni za upande uliopo kama upo upande wa nuru fata kanuni za huko hakika utaona matunda ya kazi yako.
Hakikisha humuibii Mungu zaka na sadaka ya mapato yako ...katika kila jambo mtangulize Mungu usizitegemee akili zako nae atakunyooshea mapito yako....kanuni ya kupokea ni kutoa hakuna mchawi katika hilo... Na kila jambo na wakati wake trust the process.
Kikubwa usikate tamaa amini ipo siku na wewe utatoboa
Never give up
Hakuna mtu aliyeandikiwa atakuwa masikini hii dunia.Hata Mungu wa Mbinguni anachukia masikini.
Tafuta,tafuta ipo siku utapata hata kama usipokifaidi sana wewe watakifaidi wanao.Watajiuliza dogo yule kapataje mali? Karithi kutoka kwa baba yake.Wataanza kutafuta kuhusu wewe ulifanikiwaje.Yawezekana ukawa ushaondoka duniani ila utafungua fahamu za wengi huku nyuma.Mimi nina malengo yangu.Nataka ninavyohangaika hivi,sitaki wanangu wahangaike kabisa.Najitahidi kuwawekea misingi toka wadogo yaani.Nawaanda wawe wasimamizi wa miradi ikitokea nimerudi mavumbini.Nataka wajivunie mimi kuwa baba yao hata nisipokuwepo.
Achana na njia za giza.Zitakugharimu wewe.Na kibaya zaidi wanao.Yaani bora usipopata uwaache tu wakue watapata zao.
Work smart mkuu.
Nampenda Mungu kwa kadir ya uwezo wa akil zangu na nguvu na roho yangu pia LAKINI hapo kwenye ishu ya ZAKA kwakwel huwa napata napo shida sana sana.Hilo somo halijawah kuniingia vizur (may be sijakutana na mafundisho mazuri ya kiroho ukiweka mbal haya ya kisanii sanii) na kwakwel mm sio mtoaji wa zaka kabisaa na hata hizo mara chache nilizotoa sijawah kutoa kwa moyo mkunjufu na kwakwel sikumbuki matokeo yoyte mazuri ya kiuchumi ya kutoa zaka but nataman .
Though sina uhakika sana kama hii inaweza ikawa sababu pia ya mimi ku struggle sana.
Nilivyosoma unatakata tamaa sioni maana ya kitu unachokiongea ..unamiaka mingap?
Ongea na Yesu Kristo mwambie kila shida yako na mwombe akusaidie kupata kazi na riziki ya kutosha, omba, omba, omba bila kuchoka.Kamwe usiende kwa waganga kwani mambo yako ndio yatakuwa mabaya zaidi.
mimi huwa napenda sana kusaidia ombaomba njiani kuliko kutoa sadaka.
Pitia ushauri huoSijui ndiyo nimeanza kukata tamaa kwa kweli sijielewi! Zamani niliamini uwezekano wa kupata pesa kwa njia halali ni mkubwa sana, niliamini uchawi si chochote lakini sasa naanza kuingiwa na kaimani, watu tunataabika miaka mingi kutafuta mali kwa njia halali tunawahi kuamka daily, tunapiga kazi bila kuchagua, tunajibana kula na kuvaa, hatuna mademu wakali, hatuni nyumba, magari, tumechelewa kuzaa na kuoa.
Lakini tunaowaona wazembe kila siku wanapiga hatua tu wanaenjoy maisha vyote tunavyojizuia kufanya ili tufanikiwe wao wanafanya tena kwa speed kama yote hata hivyo mafanikio yanaendelea kuwafuata (sina maana sipendi wengine wafanikiwe ila ni mfano wa kulinganisha na sisi tunao hastle).
Naanza kuamini upepo wa pesa, nuksi, mikosi na chuma ulete nk, tunapata pesa haikai na ukiangalia hatuna majukumu mengi kama kusomesha, kutunza wazazi, kutunza familia cha ajabu zaidi hatuna matumizi ya anasa, lakini bado hela haikai kila siku umaskini unaongezeka makali.
Niliamini nitakuja kuwa tajiri siku moja lakini kadiri siku zinavyosonga mbele mambo yanachange, naamini pia vijana wengi wa kati ya 18-27 wanaamini watakuja kuwa matajiri pia.
Angalizo! Usiamini kama mimi inawezekana mimi nimenza kukata tamaa au kuna maarifa fulani sahihi nimekosa katika harakati zangu, hebu na wewe jipe muda kufanya utafiti kabla hujaanza kuwaza kama mimi.
Yesu mwokozi naomba nisaidie nisiingie kwenye ushirikina angalau nipe ishara za kwenda peponi niridhike kuwa sitakuwa tajiri lakini nitaenda peponi kuliko hivi sasa. Sijui nikifa nitaenda kuteseka katika moto wa milele au nitaenda peponi. Naogopa nisije nikawa nimeteseka duniani na mbinguni nikateseka pia nikiwa moja ya viumbe vilivyoumbwa kwa ajili ya kuteseka.