Unapouliza kama kuna maisha baada ya "kifo",unatakiwa ueleze ni kifo gani unakizungumzia ili uweze kujibiwa!
Kwani kuna vifo vya aina ngapi hapa duniani? Labda tuanzie hapo
Kwanza kabla sijakueleza kuna vifo vya aina ngapi,hebu niambie wewe ulizungumzia kifo gani?
Mi nimezungumzia kifo cha kimwili mkuu; Kifo ambacho kinafanya viungo vya mwili visiweze kufanya kazi tena.
Jibu lako hili linaonesha kuna kilicho ndani ya mwili kisichokufa,sasa nakuuliza,kwanini unaamini hivi?