RESOLVED Lift moja kati ya zilizokuwa hazitumiki katika jengo la RITA Posta imeanza kutoa huduma

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Nimefika katika jengo la RITA kufuatilia cheti cha mdogo wangu baada ya kupita takribani miezi miwili tangu nilipotembelea mara ya mwisho. Napenda kutoa mrejesho kuhusu changamoto ambayo ilikuwa kero kwa watu wengi, na kwa sasa naona imepungua kwa kiwango kikubwa.

Mara ya mwisho nilipoenda RITA Posta, lift iliyokuwa ikifanya kazi ilikuwa moja tu, huku ikitumika kuhudumia watu wanaokwenda hadi ghorofa ya 20 na kuendelea. Aidha, kulikuwa na masharti kwamba lift hiyo itumike zaidi na wafanyakazi wa taasisi hiyo pamoja na watu wenye mahitaji maalumu, wazee na wajawazito.

Pia soma ~ Jengo la RITA Tower lina ghorofa 26, linatumia lift 1 tena ya kizamani, ukiingia unatoka umeloa jasho

Kutokana na utaratibu huo, watu wengi walilazimika kutumia ngazi au kusubiri kwa muda mrefu ili kupata huduma ya lift. Niliona kero hiyo ikilalamikiwa na wadau mbalimbali, na kwa kweli ilikuwa changamoto kubwa.

Leo nilipofika, nimekuta angalau lift mbili kati ya nne zilizopo zinafanya kazi. Kwa sasa hakuna tena vikwazo vikubwa vya matumizi, jambo ambalo limepunguza muda wa kusubiri huduma ya lift. Natoa pongezi kwa mdau aliyewasilisha kero hii; nina matumaini kwamba ujumbe uliwafikia wahusika na hatua zimeanza kuchukuliwa.

Nami naendelea kusisitiza hoja ya mdau kwamba mamlaka husika zinazosimamia jengo hilo lililopo Posta, Dar es Salaam, zikamilishe matengenezo ya lift nyingine ambazo bado hazifanyi kazi endapo zina changamoto za kiufundi. Hatua hiyo itarahisisha utoaji wa huduma na kuendelea kupunguza kero ya wananchi kutumia muda mwingi kusubiri au kutumia ngazi.
 
Haipiti mwezi wataifunga, lile jengo kufuata huduma unajiuliza sana.
Kusubiri lift mpaka ufike ghorofa ya 20 na mtu aliyepanda SGR anakuwa kishafika Morogoro.
 
Nimefika katika jengo la RITA kufuatilia cheti cha mdogo wangu baada ya kupita takribani miezi miwili tangu nilipotembelea mara ya mwisho. Napenda kutoa mrejesho kuhusu changamoto ambayo ilikuwa kero kwa watu wengi, na kwa sasa naona imepungua kwa kiwango kikubwa.

Mara ya mwisho nilipoenda RITA Posta, lift iliyokuwa ikifanya kazi ilikuwa moja tu, huku ikitumika kuhudumia watu wanaokwenda hadi ghorofa ya 20 na kuendelea. Aidha, kulikuwa na masharti kwamba lift hiyo itumike zaidi na wafanyakazi wa taasisi hiyo pamoja na watu wenye mahitaji maalumu, wazee na wajawazito.

Pia soma ~ Jengo la RITA Tower lina ghorofa 26, linatumia lift 1 tena ya kizamani, ukiingia unatoka umeloa jasho

Kutokana na utaratibu huo, watu wengi walilazimika kutumia ngazi au kusubiri kwa muda mrefu ili kupata huduma ya lift. Niliona kero hiyo ikilalamikiwa na wadau mbalimbali, na kwa kweli ilikuwa changamoto kubwa.

Leo nilipofika, nimekuta angalau lift mbili kati ya nne zilizopo zinafanya kazi. Kwa sasa hakuna tena vikwazo vikubwa vya matumizi, jambo ambalo limepunguza muda wa kusubiri huduma ya lift. Natoa pongezi kwa mdau aliyewasilisha kero hii; nina matumaini kwamba ujumbe uliwafikia wahusika na hatua zimeanza kuchukuliwa.

Nami naendelea kusisitiza hoja ya mdau kwamba mamlaka husika zinazosimamia jengo hilo lililopo Posta, Dar es Salaam, zikamilishe matengenezo ya lift nyingine ambazo bado hazifanyi kazi endapo zina changamoto za kiufundi. Hatua hiyo itarahisisha utoaji wa huduma na kuendelea kupunguza kero ya wananchi kutumia muda mwingi kusubiri au kutumia ngazi.
vipi ile harufu mbaya na uchafu wa vyoo
 
Back
Top Bottom