charger
JF-Expert Member
- Nov 21, 2010
- 2,320
- 1,371
Habari wana jamvi ninaamini wote hamjambo na mnaendele kuyafurahia maisha kama vile mlivyo pangiwa na wajanja wachache.
Nashukuru kwa mada iliyopita kuhusu magari maana tulipata michango mingi kutoka kwa madereva na wasafiri.Majibu yalipatikana na wanajamvi walifaidika hata wapita njia pia.Na wengine siku hiyo hiyo walienda field na wenye course work mbaya waliendelea kujinoa zaidi.
Suala ninalolileta leo ni kuhusu hayohayo magari ila leo ni kuhusu magari ya wizi na lift.Nimegundua kuwa wapo watu wengi wanamiliki magari ya thamani sana,nikisema thamani namaanisha muda waliyotumia kuyapata hayo magari au hata fedha walizotumia.Wapo watu kwenye maegesho yao ya nyumbani utakuta wengine wana Benz M-class,Murrano,Toyota fortuner,BMW,Hammer,Cardillac na mengine mengi unayoyafahamu kuwa ni mazuri situ kwa mwonekano hata kwa tabia pia.
Maajabu yanaanzia hapa,unamkuta baba mzima na tai yake kapanda Bedford la mkaa au gari la kubebea ngombe tena kawekwa nyuma,au yupo kwenye van ya kubebea mikate au mama mrembo kabisa katulia kwenye gari la taka kavunja kishoka au baba yupo kwenye ki starlet cha wizi na analazimika kupita vinjia vya ochochoroni.
Kibaya zaidi hawa watu wanakuwa mstari wa mbele hayo magari yao kikwama au yakizima wanakuwa kushuka na kuyasukuma au kuyanunulia spea wakati gari zao hawazijali hivyo.Unaweza kukuta benz lake linatembelea tairi kipara wala hajali.
SWALI:JE HAYA MAGARI YA WIZI NA LIFT HAWA WATU HUWA WANAFURAHIA NINI HUKO NA HALI WANAYO YAO MAZURI WAMEYAACHA?
Nawasilisha kwa yeyote atakaye husika