Lift na magari ya wizi.kwa wakubwa tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Lift na magari ya wizi.kwa wakubwa tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
2,320
Reaction score
1,371
Habari wana jamvi ninaamini wote hamjambo na mnaendele kuyafurahia maisha kama vile mlivyo pangiwa na wajanja wachache.
Nashukuru kwa mada iliyopita kuhusu magari maana tulipata michango mingi kutoka kwa madereva na wasafiri.Majibu yalipatikana na wanajamvi walifaidika hata wapita njia pia.Na wengine siku hiyo hiyo walienda field na wenye course work mbaya waliendelea kujinoa zaidi.
Suala ninalolileta leo ni kuhusu hayohayo magari ila leo ni kuhusu magari ya wizi na lift.Nimegundua kuwa wapo watu wengi wanamiliki magari ya thamani sana,nikisema thamani namaanisha muda waliyotumia kuyapata hayo magari au hata fedha walizotumia.Wapo watu kwenye maegesho yao ya nyumbani utakuta wengine wana Benz M-class,Murrano,Toyota fortuner,BMW,Hammer,Cardillac na mengine mengi unayoyafahamu kuwa ni mazuri situ kwa mwonekano hata kwa tabia pia.
Maajabu yanaanzia hapa,unamkuta baba mzima na tai yake kapanda Bedford la mkaa au gari la kubebea ng’ombe tena kawekwa nyuma,au yupo kwenye van ya kubebea mikate au mama mrembo kabisa katulia kwenye gari la taka kavunja kishoka au baba yupo kwenye ki starlet cha wizi na analazimika kupita vinjia vya ochochoroni.
Kibaya zaidi hawa watu wanakuwa mstari wa mbele hayo magari yao kikwama au yakizima wanakuwa kushuka na kuyasukuma au kuyanunulia spea wakati gari zao hawazijali hivyo.Unaweza kukuta benz lake linatembelea tairi kipara wala hajali.
SWALI:JE HAYA MAGARI YA WIZI NA LIFT HAWA WATU HUWA WANAFURAHIA NINI HUKO NA HALI WANAYO YAO MAZURI WAMEYAACHA?
Nawasilisha kwa yeyote atakaye husika
 
Charger bana unaleta thread nzuuuuuuuuuri wakati usingizi umeanza kunishika kesho nitachangia maana saizi naogopa nisijechemsha bure.

Ila nimecheka kweli magari ya taka?? HA ha ha haha
 
Gari la wizi halilipiwi ushuru charger, Pia Vistarlet rahisi kupaki mjini siku hzi parking shida sana
 
Ha ha haaa GAGA we ni mtundu!!:lol::lol:
Gari la wizi halilipiwi ushuru charger, Pia Vistarlet rahisi kupaki mjini siku hzi parking shida sana
 
Usiku mwema Dena kusanya nguvu!!
Charger bana unaleta thread nzuuuuuuuuuri wakati usingizi umeanza kunishika kesho nitachangia maana saizi naogopa nisijechemsha bure.

Ila nimecheka kweli magari ya taka?? HA ha ha haha
 
Ila mkuu threads zako ni balaa nimezikubali, unajua hata ile ya jana na hii nilitaka kukueleza kuwa umekosea forum kumbe ndo kwenyewe. mkuu unatisha wala sitajibu thread zaidi ya kukueleza kuwa nazipenda threads zako ambazo zinaonesha kuwa mtoa mada ni mtu wa kufikiria na mwenye busara sana. Haikosi utakuwa mtu mzima au mwenye umri wa kati! Thanx!
 
Ni tamaa 2 ndo inasababisha watu wanapanda magari ya lifti au ya taka.
 
Ila mkuu threads zako ni balaa nimezikubali, unajua hata ile ya jana na hii nilitaka kukueleza kuwa umekosea forum kumbe ndo kwenyewe. mkuu unatisha wala sitajibu thread zaidi ya kukueleza kuwa nazipenda threads zako ambazo zinaonesha kuwa mtoa mada ni mtu wa kufikiria na mwenye busara sana. Haikosi utakuwa mtu mzima au mwenye umri wa kati! Thanx!

Mgongee thatha.
 
Vipi na zile daladala unalipia kw ruti.ubungo 2 mbagala 600/= ......cku hiz kuna mabasi y mchina makubwa hayo balaa.
 
Gari la wizi halilipiwi ushuru charger, Pia Vistarlet rahisi kupaki mjini siku hzi parking shida sana

Gaga naona wewe sio mwizi au pengine tuseme huna uzoefu na wezi "hujaibwa"....kwanza kuna gharama za mipango na mikakati ya maandalizi...., kuna gharama za mafuta kwani safari wakati mwengine inabidi iwe ndefu kuficha hilo gari, halafu kunagharama za kupaki gari (sehemu zengine zinalipwa kwa masaa...na haijalishi kama ni kistarlet au hammer!!!).....naomba Ni-PM kama unahitaji kujua zaidi...pengine naweza hata kuorganise ka-practical kadogo..weekend moja hivi ...LOL
 
Daah

Chaja bana. Hii sredi bana humu ndo inafiti sana wandugu, tena hii ni FAIVU STAA sredi. Naomba sana wakuu wote waliowakilisha festi sredi muwepo
 
Jamani, gazeti la Mwananchi page kuu ina habari kwamba Daktari wa Wilaya amethibitisha mgonjwa wa ukimwi kupona kwa dawa ya Babu.

Aisee Kakobe lazima akimbiwe na wafuasi zaidi
Samahan kwa off topic
 
Hii thread sikuielewa mwanzo, lakini niliposoma tena nimeipata vizuri. Tunasubiri maoni ya wataalamu wa kuparamia magari ya wizi.
 
Pole sana mkuu kumbe tulitaka kukuacha KATAVI?
Hii thread sikuielewa mwanzo, lakini niliposoma tena nimeipata vizuri. Tunasubiri maoni ya wataalamu wa kuparamia magari ya wizi.
 
Gaga naona wewe sio mwizi au pengine tuseme huna uzoefu na wezi "hujaibwa"....kwanza kuna gharama za mipango na mikakati ya maandalizi...., kuna gharama za mafuta kwani safari wakati mwengine inabidi iwe ndefu kuficha hilo gari, halafu kunagharama za kupaki gari (sehemu zengine zinalipwa kwa masaa...na haijalishi kama ni kistarlet au hammer!!!).....naomba Ni-PM kama unahitaji kujua zaidi...pengine naweza hata kuorganise ka-practical kadogo..weekend moja hivi ...LOL

@ work
 
Daah

Chaja bana. Hii sredi bana humu ndo inafiti sana wandugu, tena hii ni FAIVU STAA sredi. Naomba sana wakuu wote waliowakilisha festi sredi muwepo

Imekaa njema sanaaaaa. Charger kiboko
 
charger,suala lingne watu huwa labda wanafuata mambo ya manual o automatik,what i knw gari za taka ni manual,so mr au mrz anaweza akafuata la taka,ili aendshe mwenyewe
 
Back
Top Bottom