Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sawa Mdogo wangu

Tutaanzia zile Opposite na kwenu...PSSSF commercial Complex...Tena bado mpya mpya zile...

Halafu twende na pengine tena[emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] usinikumbushee siku ya kwanza napanda lift nililia kwa sauti, hadi niliyekua nae aliona aibu.

Nilihisi hali ya ajabu, joto maradufu, kizunguzungu, tunapanda juu, mie naona tunateremkaaaa tena bila break [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nisipige yowee afu LA nguvuu, kila nikikumbuka najichekaaa sanaaa. Ushambaa huu mweeeh.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Watu saba wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kwa ajili ya matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jengo la Millenium Tower lililopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema chanzo ni lifti hiyo iliyokuwa imebeba zaidi ya Watu kumi kuzidiwa uzito β€”β€”β€” β€œlifti ilizidiwa uzito na ilikuwa imefanyiwa matengenezo hivi karibuni ambapo leo ilikuwa inajaribiwa na kulikuwa na Fundi ndani”

Askari wa Zimamoto na Uokoaji Assintant Inspector Mohammed kutoka Kinondoni amesema kilichofanywa na Uongozi wa jengo hilo lenye ghorofa 25 ni makosa kwa kuwa hawakupaswa kufanya majaribio ya lift kukiwa na Watu ndani bali walitakiwa kuweka kitu chochote chenye uzito ndani ya lifti ndio waifanyie marekebisho.
 
Watu wanaviburi sana. Hizi lift huwa zina limit ya kilo na idadi ya watu. Wewe unajiona ni saizi ya kiboko na watu waliopo ndani ya lift mnalingana ukiingia mtazidisha uzito ila unafosi kuingia. Mimi bwana lift huwa sipandi kama imejaza watu.

Huwa natetemeka sana nikipanda lift halafu watu wengine wakaingia kwa wingi floor inayofuata tukiwa tunapanda au kushuka.

I hope hili tukio serikali watatilia mkazo kuweka vibao kutoka jeshi la uokoaji raia na mali zao ambavyo vitaelekeza mipaka ya lift.
 
Hapo sipati picha walivyokuwa wakimuita Mungu au Mama zao maana kutoka 10 hadi mwisho wa lift sio kazi ya kitoto
Hapo sipati picha walivyokuwa wakimuita Mungu au Mama zao maana kutoka 10 hadi mwisho wa lift sio kazi ya kitoto
wanasema the best way ya kusurvive elevator falling ni kulalia mgongo tu, hata kama itafall kutoka floor ya 50 una chance kubwa ya kusurvive with minor damages.

Mikao mingine una chance yakuvunjika miguu au spinal cord.
 
Idadi ikizidi kwa lift ya jengo ninalotembelea mara kwa mara milango hua haifungi na inalia alarm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…