Ligi Daraja la Kwanza 2014/15, updates hapa

Ligi Daraja la Kwanza 2014/15, updates hapa

kundi A maji maji na timu nyingine..
kundi B mwadui fc na toto africans ndio zitakazoingia premier

Mie naiombea sana Toto Africans ipande ili jamaa wa pale Msongamanoni washike adabu. Hata wao nadhni waaiombea Toto isipande maana ni kichomi kwao.
 
wadau vipi naona kimya kimezidi baada ya Mwadui fc kutoa dozi tu..

Mwadui kadraw na JkT Oljoro, Mwadui kuongoza huwa anaongoza lakini hapandi, msimu uliopita aliongoza sana ligi akapanda Stand Utd, msimu ule mwingine aliongoza akapanda Rhino F.C na SASA mwacheni aongoze atapanda Toto, Kwa Shinyanga Stand wanatosha sasa ni zamu ya Mwanza Kuwa na Timu Ligi Kuu.
timu yenye uhakika wa kupanda hadi SASA ni Maji Maji ya Songea
 
Uwanja wa Ccm Vwawa Kimondo imemkamua polisi Dar bao 1-0 mchezo ambao tangu asubuhi ilikuwa mvua kwa kwwenda mbele hivyo kukosa ufundi.Kimondo walipata bao kupitia kwa Mpoki Mwakinyuke dakika ya 27 kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo kimondo ina point 20 na magoli 18 ya kufunga na 18 ya kufungwa na inapanda hatua mbili kwenye msimamo kutoka nafasi ya sita hadi ya nne huku polisi ikiporomoka
 
Ila timu za polisi zipunguze ubabe hata uwanja wa Vwawa baada ya mchezo kwisha wameanzisha vurugu jukwaani, ila wamejibiwa vikali na wananchi na kudhihirisha kupenda shari michezoni
 
Msimamo umekosewa kabisa kwa tarehe 12 january kwani Kimondo ilikuwa na pointi 20 hadi tarehe 12/1/2015 na hadi mchezo wa leo 14/1/2015 Kimondo ina pointi 23 hivyo kuwa nyuma ya Friends rangers na siyo Tessema
 
Back
Top Bottom