Ligi ilinoga zaidi Simba na Yanga walipoacha kushea uwanja

Ligi ilinoga zaidi Simba na Yanga walipoacha kushea uwanja

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Yanga toka ilipoanza kutumia uwanja wa Azam Complex ilionekana kuukubali hadi ikaanza kutamba kama vile wao ndiyo wana umiliki.

Simba ikahisi uwanja kama unawakataa, ikaanza kuhaha huku na kule kutafuta pa kujisitiri. Ni hadi ilipoupata uwanja wa KMC, Simba ndiyo ikaonekana kutulia, ikichangiwa na kosi jipya chini ya Fadlu.

Binafsi nilipenda kuona timu mbili shindani zikitumia viwanja viwili tofauti na vyote vina quality ingawa nadhani Chamazi una quality zaidi kuanzia pitch hadi viti.

Kitendo cha Yanga kukimbilia KMC ni move ambayo nahisi ina mashinikizo ya watu wa nje ya mpira.

Kwa mvuto na ushindani wa ligi, Simba na Yanga wangeendelea kutumia viwanja tofauti. Kujibana kwenye kakiwanja kadogo kama ka KMC ni dalili za kufilisika kisiasa na kufosi kutrend.
 
Hawajakubaliwa bado na sina hakika sababu zao ni za msingi ktk maombi yao ya kubadilishiwa uwanja.
 
Hamia ligi ya Burundi
Wazee wa Simba washasema wanataka kuhamia Burundi
 
Back
Top Bottom