Ligi ipi bora Afrika Mashariki?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Afrika Mashariki ina nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. Kote huko mpira wa miguu unachezwa barabara. Lakini Je ni nchi ipi ina ligi bora zaidi kutokana na vigezo vyako?
 
Bila shaka ni VPL.

Kwanini nasema VPL. Nimejaribu kupima mafanikio madogo ambayo vilabu kwenye hizi ligi zimefikia.
1. Vpl imeto vilabu vinavyoshiri na kufikambali mara nyingi kwenye michuani ya bara cafcl na cafcc.
2. Watazamajina wafuatiliaji. VPL inataamwa na kufuatiliwa na watu wengi zaidi kuliko ligi nyinginezo, zingatia wastani wa match attendance
3. Mishahara ya wachezaji. VPL inaongoza kulipa pesa ndefu sana wachezaji ukilinganisha vilabu vya ligi mbalimbali za afrika mashariki. (azam,yanga,simba,singida utd.............mtibwa,kagera,mbeya city)
4. VPL ina udhamini mnono kuliko ligi yeyote hapa mashariki.
 
hata wachezaji wa kigeni ni wengi VPL
 
Bila shaka vpl imejaribu kuufanya mpira kuwa ni biashara yenye mafanikio kwa wachezaji ila ina marefa wabovu kuliko ligi zote Afrika mashariki.
 
Bila shaka vpl imejaribu kuufanya mpira kuwa ni biashara yenye mafanikio kwa wachezaji ila ina marefa wabovu kuliko ligi zote Afrika mashariki.
linalalamikiwa na wengi, dawa ya hili ni nini? Malinzi alijaribu kuwafungia Karia akawafungulia waliofungiwa kwa kuboronga.
 
VPL
Ndio ligi yenye mkwanja mrefu zaidi na inavutia zaidi japo ubabaishaji mwingi

VPL ni platform kwa wachezaji wa ligi nyengine east and central africa kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…