Mechi kati ya Simba inaendelea muda huu Simba wakiwa mbele kwa bao 2 dhidi ya Fountain gate.
Simba yupo ugeninim, Goli kwanza limefungwa na Chama, la pili limefungwa na Gueye. Na sasa ni kipindi cha pili
-----
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate FC leo. Katika mchezo huo uliopigwa leo jioni, Simba walionyesha utofauti mkubwa wa kiufundi, wakitumia vema makosa ya wapinzani wao na kutawala eneo la kiungo, jambo lililowapa urahisi wa kufika langoni mwa Fountain Gate mara kwa mara na kuondoka na ushindi huo muhimu wa ugenini.
Karamu ya mabao ya Simba ilifunguliwa na kiungo fundi Clatous Chama katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza (45+4'), kabla ya Gueye kupigilia bao la pili mnamo dakika ya 58 ya mchezo. Hali ikazidi kuwa mbaya kwa Fountain Gate katika dakika ya 71, ambapo shinikizo la mashambulizi ya Simba lilipelekea beki wa Fountain Gate kujifunga goli la tatu wakati akijaribu kuokoa hatari langoni. Ushindi huu wa mabao matatu kavu unazidi kuwapandisha chati Simba, huku Fountain Gate wakijutia makosa ya ulinzi yaliyowagharimu pointi zote tatu nyumbani.
DK 72, Simba wanapata chuma ya tatu
Klabu ya Fountain Gate ikiwa nyumbani imekubali kichapo cha mabao 3 kwa 0 kutoka kwa Simba SC
Kwa matokeo hayo Simba imeongeza pointi 3 na kufikisha alama 39 ikibaki nafasi ya pili huku Fountain Gate ikibaki nafasi ya 14 na alama 16 kati ya timu 16 kwenye Ligi Kuu Bara