BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Upande wa pili kuna Championship au Ligi Daraja la Kwanza ambayo huwa inatoa timu zinazopanda daraja kwenda kucheza katika Ligi Kuu.
Swali au hoja ambayo nilikuwa najiuliza timu ya DTB ikipanda daraja itakuwaje?
DTB ni jina la benki, mdhamini wa Ligi Kuu ni benki pia, kwa moto ambao walikuwa wakiuwasha DTB kwenye Championship ilionekana wazi wanapanda daraja bila wasi, kwanza wana kikosi kizuri na walikuwa wanaonyesha uwezo mkubwa.
Baada ya kufuatilia kwa vyanzo kadhaa nikapata majibu mawili yanayokinzana.
Jibu la 1#: DTB HAWAWEZI KUPANDA DARAJA
Naikumbuka kauli hii niliambiwa mwanzoni kabisa wakati Championship ikiwa hata haijafika nusu ya mzunguko, nikauliza kwa nini wakati moto wao ni mkali?
Nikajibiwa ‘Soka la Tanzania lina wenyewe, hao hata wacheze vipi hawawezi kupanda daraja, wakipanda wataenda kuvuruga mambo, hatuwezi kuwa na mgongano wa kimaslahi, Ligi ni ya NBC kisha timu inadhaminiwa na DTB, hivyo kutakuwa na ushindani wa kibishara na hiyo haitamfurahisha mdhamini mkubwa ambaye ni NBC.
Inamaanisha NBC watakuwa wanatoa dau kubwa la fedha kisha DTB wanaingilia nao wanatangaza kwa dau dogo japo wao ni timu moja, pili jezi ya DTB itakuwa na matangazo mawili ya biashara zinazoshindana.
Kwa jibu hilo naona kama inaanza kuelekea, kwani DTB walikuwa wanaongoza kwa tofauti ya idadi kubwa ya pointi, lakini leo zimebaki mechi tano na wanaongoza kwa zaidi ya pointi 3 tu, hiyo ni dalili mbaya.
Jibu la #2: DTB WATAPANDA, KIGOGO WAO ATAIBADILISHA JINA
Hili jibu nilipewa na mtu mwingine wa karibu na viongozi wa soka kuwa DTB inamilikiwa na kigogo mmoja ambaye ni mwanasiasa.
Huyu aliwahi kumiliki timu flani baadaye ikageuka kuwa tawi la timu moja kubwa kutoka pale Kariakoo, mwisho ikapotea na yeye akaisusa.
Hivyo, kitendo cha kutumia jina la DTB ilikuwa ni geresha tu lakini itapanda daraja, itabadilisha jina maisha yataendelea, hakutakuwa na ushindani tena wa NBC na DTB.
Jibu sahihi ni lipi? TUSUBIRI MUDA UTAZUNGUMZA