Ligi Kuu Bara: Klabu ya Yanga imeshindwa kung'ara mbele ya Klabu Singida Utd baada ya kutoka sare ya goli 1-1

Ligi Kuu Bara: Klabu ya Yanga imeshindwa kung'ara mbele ya Klabu Singida Utd baada ya kutoka sare ya goli 1-1

Hazard CFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2015
Posts
16,627
Reaction score
38,689
Kikosi cha Young Africans kitakachoanza dhidi ya Singida United katika mechi ya Ligi Kuu Bara

Youthe Rostand, Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Abdallah Shaibu, Kelvin Yondani , Papy Tshishimbi, Yusuph Mhilu, Raphael Daudi, Obrey Chirwa, Pius Buswita, Ibrahim Ajibu

Kikosi cha akiba
Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Nadir Haroub, Said Makapu, Geofrey Mwashiuya, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi

FB_IMG_1523449988776.jpg

Kikosi cha Singida United dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara leo

Ally Mustapha, Miraj Adam, Shafik Batambuze, Malik Antiri, Kennedy Juma, Mudathir Yahaya, Deus Kaseke, Nizar Khalifan, Papy Kambale, Kenny Ally, Kiggy Makasi

Kikosi cha akiba
Peter Manyika, Salum Chuku, Yusuph Kagoma, Rolland Msonjo, Elinywesia Sumbi, Lubinda Mundia, Danny Usengimana

Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

Mchezo umeanza
01': Yanga wanamiliki mpira, wanpiga pasi lakini Singida nao wapo makini.

02': GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

04': Yanga ni kama bado hawajajipanga.
Krosi ya Kigi Makasi inatua mguuni kwa Saliti Kambale anamalizia wavuni

06': Singida wanapata mpira wa kurushwa pembeni ya uwanja.

09': Mpira umeganda kwenye lango la Yanga lakini walinzi wanakuwa makini kuzuia

10': Yusuph Mhilu anapiga shuti linamgonga beki na kuwa kona langoni mwa Singida.

12': Kipa wa Singida , Ally Mustapha 'Barthez' yupo chini ameumia wakati wa kurukia mpira.

14': Mchezo unaendelea.

15': Yanga wanafanya mashambulizi mawiali makali, wanapata kona mbili mfululizo.

16': Yanga wanafanya shambulizi kali, inakuwa kona.

20': Biswita anacheza faulo. Inapigwa kueleka kwa Yanga

23': Tshishimbi anapiga shuti linatola nje kidogo ya lango la Singida.

24': Chirwa anashindwa kutumia vizuri pasi aliyopewa na Ibrahim Ajibu.

29': Yanga wanahitaji kuwa makini, Singida wanapata nafasi ya kupiga shuti la wazi lakini mpira unapaa.

34': Raphael Daudi anacheza vibaya inakuwa faulo kuelekea kwa Yanga

SUB, 36': Yanga wanamtoa kipa mkongwe Ally Mustapha 'Barthez' na nafasi yake inachukuliwa na Peter Manyika

38': Daud anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, ilikuwa ni hatari na jaribio la kwanza Manyika akiwa langoni

40': kinda Mhilu yuko chini pale, inaonekana aliumizwa

42': Kambale anajaribu kuingia kwa kasi, lakini Yondani anazuia vizuri kabisa hapa

SUB, 43': Salum Chukwu, anaingia kuchukua nafasi ya Batambuze raia wa Uganda

44': Chukwu anawahadaa mabeki wa Yanga, anaingai ndani ya boksi, lakini Yondani yuko makini tena

45': Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa, unamgonga beki Juma na kuwa kona

GOOOOOOOOO Dk 45, Shaibu au Ninja anaruka kuunganisha kona ya ya Ajibu na kuiandikia Yanga bao safi kwa mpira huo wa kichwa

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

Mpira safi wa adhabu wa Ajibu, Buswita anaishaaa juuuu...ilikuwa hatari ndani ya lango la Singida

MAPUMZIKO

45': Yanga wanaanza kwa kasi wakionyesha wamepania kusawazisha

47': Singida wanaingia vizuri lakini Makasi anashindwa kupiga krosi na kuanguka

48': Kambale anataka kumpita Yondani lakini anamdhibiti vizuri kabisa

50': Yanga wanaendelea kusukuma mashambulizi ya kushitikkiza, lakini Singida wanaokoa na kuwa kona
Krosi safi ya Kessy lakini Juma anaokoa kwa kichwa

53': Kaseke anageuka na kumtoka Mwinyi, anaingia lakini anaonyesha papara hapa na kupiga shuti hoooovyo

55': kwa sasa mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja ingawa Singida United kama wanapoteza muda hivi

57': Mhilu anaingia vizuri lakini uzoefu unamfanya kutokuwa na maamuzi sahihi

59': Manyika analazimika kufanya kazi ya ziada na kuondosha mpira mbele ya Chirwa aliyekuwa amepitishiwa kimo cha nyoka

61': kwa takribani dakika moja nzima, Singida wamekuwa wakimiliki mpira wao, Nizar Khalfan na Mudathir wakifanya wanavyotaka wao katikati ya uwanja
Mpira wa adhabu wa Chukwu, Mwinyi anaruka na kuokoa, konaa

62': Chukwu anachunga kona, inatua kwa Kaseke, anamuachia Mudathir anayepiga mkwaju mkali wa chinichini, goal kick

63': Ajibu anajaribu kuchambua, anaachia mkwaju mkali kabisa, goal kick

64': Chirwa anaingia vizuri hapaaa, chini. Mwamuzi anamuambia simama ucheze mpira...Kennedy Juma alimgusa kwa mkono pia mguu akaanguka

66': Mhilu anachambua watu watatu, anampa Chirwa anamchambua beki mmoja, lakini hakuwa shap katika kuupiga mpira

67': Mwinyi anaingia vizuri lakini krosi yake inatua mikononi mwa Manyika

68': Ndani ya 18, Chirwa anageuka na kuachia mkwaju mkali kweli, Manyika anapangua na kuwa kona

SUB 68': Kagoma anaingia kuchukua nafasi ya mkongwe Nizar Khalfan

69': kona ya Ajibu, Manyika anaruka juu kabisa na kudaka kwa ustadi

71': Kaseke anagongeana vizurik na Miraj Adam, anajaribu ilikuwa ni hatari lakini goal kick

73': Chukwu analazimika kulala na kuutoa nje mpira wa Mhilu, kona

SUB 73': Juma Madhadhi anaingia kuchukua nafasi ya Buswita
Mkwaju safi wa kona wa Ajibu, Manyika anaokoa na anagongwa, mwamuzi anasema ni faulo

KADI 77': kadi ya kwanza katika mchezo wa leo inatoka na inakwenda kwa KAseke ambaye ameushika mpira kwa makusudi kabisa

SUB 78': Ajibu anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Goefrey Mwashiuya

KADI 79': Kadi ya pili ya njano inatoka, nayo ni kwa Singida United, anazawadiwa Chukwu

80': Krosi matata ya Kiggi, lakini Kambale anafanya madhambi kwa kumuangusha Ninja

83': Zaidi mpira unachezwa katika ya uwanja na hakuna mashambulizi mengi makali

84': Bado hakuna mipango kwa Singida United, tofauti na Yanga. Singida wanapaswa kuwa makini au watafungwa
Mhilu tena, anaingia vizuri kabisa na kutoa pasi nzuri ya Chirwa, ndani ya miguu 12 anapiga shuti kuuuubwaaaa

KADI, 86': Kessy anapewa kadi njano kwa kumuangusha Chukwu

88': Kaseke anaingia mpira wake unaokolewa na kuwa kona

89': Yanga wanamuingiza Martin kuchukua nafasi ya Chirwa

90': Kiggi anakwenda kuchonga hiyo kona, Kambale anaruka peke yake na kupuga kichwa, goal kick

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
 
wapi Akilimali?
maana alikuwa kimbelembele kumpiga vita kibosile Manji!!
 
Back
Top Bottom