Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti, 23 mwaka huu katika viwanja tofauti hapa nchini.
Ligi itafunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ndio huashiria ufunguzi rasmi wa Ligi unatarajiwa kuchezwa Agosti 17, 2019 kati ya Bingwa wa Ligi Kuu Simba SC dhidi ya Azam FC Bingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federetion CUP.
Ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari za michezo amesema kwamba Agosti 23 panzia la ligi kuu litafunguliwa rasmi kwa mchezo mmoja kupigwa kati ya Simba SC dhidi ya JKT Tanzania.
Wambura amesema kwamba Yanga SC wataanza kurusha karata yao ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting Agost 28, Azam FC na KMC zinatarajiwa kucheza Agosti 29 mwaka huu.
Simba na Yanga zitakutana kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, January 04, 2020 ambao Simba ndio atakuwa mwenyeji.