Ligi Kuu Bara kuanza kutimua vumbi Agosti 23 mwaka huu, Simba na Yanga kukutana mwakani

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti, 23 mwaka huu katika viwanja tofauti hapa nchini.

Ligi itafunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ndio huashiria ufunguzi rasmi wa Ligi unatarajiwa kuchezwa Agosti 17, 2019 kati ya Bingwa wa Ligi Kuu Simba SC dhidi ya Azam FC Bingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federetion CUP.

Ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari za michezo amesema kwamba Agosti 23 panzia la ligi kuu litafunguliwa rasmi kwa mchezo mmoja kupigwa kati ya Simba SC dhidi ya JKT Tanzania.

Wambura amesema kwamba Yanga SC wataanza kurusha karata yao ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting Agost 28, Azam FC na KMC zinatarajiwa kucheza Agosti 29 mwaka huu.

Simba na Yanga zitakutana kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, January 04, 2020 ambao Simba ndio atakuwa mwenyeji.
 
Write your reply...Aliyeiona naomba aniambie timu yangu pendwa Biashara united tunaanza na nani please.
 
Simba vs Yanga January 4 , wakati huo hip Mapinduzi Cup inaanza January 2 yaani Apo hicho kiporo Tayari hate ligi haijaanza
Sasa kama ratiba zote za mashindano yote mawili wanayo kwanini wasisimamishe shindano moja? Hapo ligi inapaswa kusimama tu
 
Kiporo kimoja tayari!
Sasa kama ratiba zote za mashindano yote mawili wanayo kwanini wasisimamishe shindano moja? Hapo ligi inapaswa kusimama tu
Hahahaha, halafu useme kuna watu wako serious na kazi zao? Hata kuwaza tu kwa haraka wameshindwa

Tikiona ratiba yote itakua na viporo kibao ,maana msimu wa 2019/20 CAF timu NNE tunaingiza + mechi za stars CHAN
 
Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti, 23 mwaka huu katika viwanja tofauti hapa nchini.

Ligi itafunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ndio huashiria ufunguzi rasmi wa Ligi unatarajiwa kuchezwa Agosti 17, 2019 kati ya Bingwa wa Ligi Kuu Simba SC dhidi ya Azam FC Bingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federetion CUP.

Ofisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura leo Jumatatu wakati akizungumza na waandishi wa habari za michezo amesema kwamba Agosti 23 panzia la ligi kuu litafunguliwa rasmi kwa mchezo mmoja kupigwa kati ya Simba SC dhidi ya JKT Tanzania.

Wambura amesema kwamba Yanga SC wataanza kurusha karata yao ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting Agost 28, Azam FC na KMC zinatarajiwa kucheza Agosti 29 mwaka huu.

Simba na Yanga zitakutana kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, January 04, 2020 ambao Simba ndio atakuwa mwenyeji.
N wadhamini bado hakuna,Tiii Efu Efu kweli kichefuchefu
 
Back
Top Bottom