Ligi Kuu Bara Oktoba 16 2016: Yanga SC 0, Azam FC 0

Ligi Kuu Bara Oktoba 16 2016: Yanga SC 0, Azam FC 0

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Mechi ya Yanga na Azam, leo itatoa mwanga Ubingwa kwa Simba.

Fuatilia hapa

====
images.jpg

YANGA SC 0 - 0 AZAM FC
From Uhuru stadium
FULLTIME​


Dk 93, Mchezo umekuwa na kasi ya kawaida, inaonekana pande zote mbili zimeridhika na alama moja


Dk 92, dakika mbili za nyongeza zimekatika, mashabiki kadhaa wameanza kuondoka uwanjani.

Dk 90, mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza.

Dk 87, SUB: Azam wanafanya mabadiliko, anaingia Khamis Mcha, anatoka Kangwa.

Dk 83, Azam wanafanya shambulizi kali, inapigwa kona Frank Domayo anapiga kichwa mpira unaelekea wavuni lakini Dida anafanya kazi nzuri, akauokoa mpira na mabeki wake wanaupiga kuuondoa langoni.

Dk 80, Yanga wanafanya mabadiliko, Dante anatoka anaingia Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Dante anatoka baada ya kuumia kutokana na kuchezewa vibaya na Himid

Dk 78, SUB: Azam wanamtoa John Bocco, anaingia Francisco.

Dk 76, Mwamuzi Israel Nkono anasimamisha mchezo kwa muda, anazungumza na Thomas wa Azam ambaye alionekana kupandwa na hasira na kumfokea mwamuzi wa akiba baada ya kuutoa mpira na kuelekea langoni kwake akidhani ulitakiwa kuelekea upande wa Yanga.

Dk 67, Kasi ya mchezo siyo kali, imepungua na mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja huku timu zote zikionekana kutegeana katika kufanya mashambulizi.

Dk 65, Msuva anaingia na mpira lakini anafanyiwa faulo na kiungo wa Azam, Migi.

Dk 60,Yanga wanapata kona.Inapigwa kona lakini mabeki wa Azam wanaoko.

Dk 57, Yanga wanafanya mabadiliko, anaingia Geofrey Mwashiuya, anatoka Deus Kaseke ambaye alikuwa upande wa winga wa kushoto.

Dk 55, Kangwa wa Azam anapata nafasi ya kupiga shuti kali langoni mwa Yanga lakini Dida analidaka.

Dk 53, Azam wanafanya shambulizi lingine lakini kipa wa Yanga, Deo Munis 'Dida' anaokoa.

Dk 50, Azam wanapiga pasi nzuri kuanzia katikati ya uwanja, wanalifikia lango la Yanga lakini mshambuliaji Thomas anashindwa kutumia nafasi anayopata, mabeki wa Yanga wanaokoa.

Dk 47, Mchezo umeanza kwa kasi ndogo, bado timu zote zinaonekana kusomana. Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

KADI Mudathiri kwa kuinua mguu juu ya kichwa cha Twite

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

Dk 44, Chirwa anaruka na kuunganisha krosi ya Msuva lakini inakuwa laini kabisa kwa Aishi

Dk 41, Bocco anaachia shuti kali kabisa, lakini Dida anaokoa na kuwa kona

Dk 36 hadi 40, hakuna shambulizi hata moja na mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja

Dk 34, Morris anafanya kazi ya ziada kukoa mpira mbele ya Chirwa na kuwa kona,inapigwa lakini haina faida

Dk 32, Ya Thomas anaingia vizuri tena na Yanga wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na Mudathir, Yanga wanaokoa

Dk 29, krosi ya Ya Thomas inazuiwa na kuwa kona upande wa Yanga, Azam wanaichonga lakini haina makali, Yondania anaondosha

SUB Dk 27, Mbuyu Twite anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul aliyeumia

KADI Dk 24, Morris analambwa kadi ya njano baada ya kwenda kumuangusha Chirwa

Dk 23, Mudathir anapiga shuti kali kabisa la mpira wa adhabu, Dida anaokoa vizuri na kuwa kona ya kwanza ya Azam FC

Dk 16, mpira wa adhabu wa Juma Abdul, kichwa safi cha Chirwa lakini Aishi anaonyesha anaweza na kudaka vizuri kabisa

Dk 15, Yanga inapata kona ya tano baada ya shuti la Kamusoko kuokolewa na mabeki wa Azam FC

Dk 13, Azam wanapoteza nafasi nzuri kabisa, krosi nzuri, Ya Thomas anaunganisha lakini kiduchu kabisa inatoka nje ya lango la Yanga

Dk 10, Azam wanafanya shambulizi kubwa, lakini Yanga wanaokoa na Juma Abdul anachukua mpira na kuanza kazi

KADI Dk 7, Nyoni kalambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva

Dk 3, Yanga inapata kona ya tatu ndani ya dakika tatu, lakini inakuwa haina madhara tena kwa Azam

Dk 2, Msuva anaingia vizuri kabisa, lakini Azam FC wanaokoa na kuwa kona

Dk 1, Kamusoko anaachia shuti kali lakini kipa Aishi Manula anaokoa na kuwa kona, inachongwa na haina madhara

Dk 1 Mechi imeanza kila upande ukimvizia mwingine

Vikosi ndo vinaingia uwanjani

Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Azam FC
Deo Munishi Dida, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vicent Andrew, Kelvin Yondani, Saidi Makapu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Deus Kaseke

Benchi:
Beno Kakolanya, Oscar Joshua, Kanavaro, Matheo Simon, Mbuyu Twite, Geofrey Mwashiuya, Juma Mahadhi

Kikosi cha Azam FC leo dhidi ya Yanga SC
Aishi, Bocco, Erasto, Amoah, Morris, Jean, Himid, Mudathir, Salum, Gonazo, Kangwa
 
Bado mapema mkuu,,,,,, simba bado tunahesabu tu tutatoa kauli baadaye!
 
Vyovyote itakavyokua.. Simba S.C ni bingwa wa VPL msimu huu.. Hili halina mjadala kabisa.
Ubingwa huobni wa kuota au wa ramli
Maana hata raundi ya kwanza haijaisha sijui umejuaje mkuu
 
Wacheze netball au baseball, tumeshamalizana nao..
 
Vyovyote itakavyokua.. Simba S.C ni bingwa wa VPL msimu huu.. Hili halina mjadala kabisa.
Wewe utakua ni mzungu wao yule ambaye hata mwaka jana ulisema tukifika mwezi May tukuulize bingwa ni nani.. [emoji16] [emoji16] mbumbumbu fc buana, wanachekesha sana. Mchezo huu hautaki hasira mkuu,... Twende mdogo mdogo, safari bado bado sana
 
simba zee haendi mbali ataishiwa pumzi mda c mrefu...ngoja aanze madudu yake akikutana na toto africa
Mlisema hivi hivi, tulipoanza ligi.. Mlianza ngoja akutane na Mtibwa.. Tukamgonga.. Mkaja ngoja akutane na Azam.. Tukamgonga.. Mkaendelea ngoja akutane na Yanga.. Mkabebwa.. Hamkutosheka, ngoja akutane na Mbeya City.. Tukamgonga.. Sasa naona mmegawanyika.. Wengine ngoja mkutane na Toto.. Wengine na Stand United.. Na nadhani tukishawagonga hao.. Mtaamia majimaji
 
Wewe utakua ni mzungu wao yule ambaye hata mwaka jana ulisema tukifika mwezi May tukuulize bingwa ni nani.. [emoji16] [emoji16] mbumbumbu fc buana, wanachekesha sana. Mchezo huu hautaki hasira mkuu,... Twende mdogo mdogo, safari bado bado sana

Mkuu.. Kwenda mdogo mdogo nendeni nyinyi.. Sisi ni Mwendokasi mwanzo mwisho.. Mpaka tutangaze ubingwa mapema kabisa.
 
Naona waganga wameanza kupga ramli zao
Haya mm nasubiria Time will tell me
 
Back
Top Bottom