Ligi Kuu Bara: Simba vs Yanga, 08 Machi 2015

Ebu nitajie hiyo mara tatu ni lini na lini? Unakumbuka tano zilikuwa mwaka gani?
Vipigo vibaya sana, mbona net inapotea hivyo! Kaangalie tena kumbukumbu! Tulikupeni dozi 2012.

Hata nikikutajia bado hautakubali na kusadiki, kwakuwa hata wewe ukumbuki mara ya mwisho simba sports club kutwaa ndoo.!
 
Amavubi endelea kushusha upako huo, huku tunateremshia na bia za bariiidi. Nyama huku tumekula zote jikoni tumemaliza Wadau tunataka tuhame kiwanja.
Mamamaeeeee leo lazima tuwasaidie majogoo kazi ya kuwaamsha yeboyebo, haiwezekani walale mapema halafu wachelewe kuamka, waje tuwakomelee vingine viwili tena.

Au tuombe mechi irudiwe nini, kuifunga yeboyebo kunasaidia mji kuwa katika hali ya usafi kama wakati wa Obama.

Muhudumuuuu...huyo aliyevaa nguo za Yanga..eeh huyohuyo njooo hapa kaa mapajani nikuagize.
 
Last edited by a moderator:
Hata nikikutajia bado hautakubali na kusadiki, kwakuwa hata wewe ukumbuki mara ya mwisho simba sports club kutwaa ndoo.!

Kwa taarifa yako, Yanga wamechukua ubingwa 2009, 2011, 2013 ndo walipogomea hapo, 2012 ilikuwa Simba, 2014 ni Azam, 2015 .........! Sasa hiyo mara tatu toka 2012 sijui viroba vimekulemea kwa dozi au!
 
Hata nikikutajia bado hautakubali na kusadiki, kwakuwa hata wewe ukumbuki mara ya mwisho simba sports club kutwaa ndoo.!

Mara ya mwisho ilikuwa Mei 6 2012 mlipopigwa tano bila.
 
Hata nikikutajia bado hautakubali na kusadiki, kwakuwa hata wewe ukumbuki mara ya mwisho simba sports club kutwaa ndoo.!

Umetajiwa, nimekutajia pale juu mara ya mwisho Simba kuchukua ilikuwa 2012 tena kwa kumkojolea Yanga bao 5 kwa bila. Hiyo mara 3 yenu ni mwaka gani?

Au umejumlisha na ndondo za mtaani kwenu ndiyo umepata mara 3?
 
2013 mkachukua nyie na Azam 2014 au mkuu umeanza ushabiki mwaka huu nini?
 
Nyie mbumbumbu kweli mmesema Yanga timu ya wazee, nikawauliza Mapunda gage inasomaje. Mmenibadilikia tena ama kweli wageni wa ushindi utawajua tu.

poleeeeeeeeee
kufungwa kunaumaaaa
 
Umetajiwa, nimekutajia pale juu mara ya mwisho Simba kuchukua ilikuwa 2012 tena kwa kumkojolea Yanga bao 5 kwa bila. Hiyo mara 3 yenu ni mwaka gani?

Au umejumlisha na ndondo za mtaani kwenu ndiyo umepata mara 3?

Kama bado ana kizunguzungu anaweza hata akamwambia mtu amsaidie, aingie google, zipo hazarani tuu hapo wikipedia, wala hazijachakachuliwa!! Aingie ataziona. Yanga wamechukua mara moja tuuu toka tuwape TANO.
 
Msimamo wa Ligi baada ya mechi za leo, Jumapili. Kwa hisani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Kwa matokeo ya leo mbali ya sisi wanamsimbazi wengine wanaoyafurahia ni wadogo zetu Azam maana sasa pengo la pointi limepungua kutoka 4 mpaka 1.
Na ile kadi nyekundu walioipata kizembe tena mimi nasema refa aliwabeba sana washenzi wale, Mrwanda dakika ya 29 alimsukuma kwa makusudi mchezaji wa Simba mbele ya mwamuzi lakini mwamuzi akatoa kadi ya njano tu. Wamshukuru kocha wao kwa kumtoa maana Messi alishapanga kumtafutia kadi ya pili. Messi bhana iko nakosha mtima wangu mimi.

Leo yeboyebo ilikuwa wacheze 9 uwanjani kama si kocha kumstukia na kumtoa galasa Mrwanda.
 
Kwa taarifa yako, Yanga wamechukua ubingwa 2009, 2011, 2013 ndo walipogomea hapo, 2012 ilikuwa Simba, 2014 ni Azam, 2015 .........! Sasa hiyo mara tatu toka 2012 sijui viroba vimekulemea kwa dozi au!

Mkuu unaongea na Div 5 ya mulugo basi hata inaelewa, ukichanganya na kuvurugwa basi bado litoe udenda tu.
 
Ebu nitajie hiyo mara tatu ni lini na lini? Unakumbuka tano zilikuwa mwaka gani?
Vipigo vibaya sana, mbona net inapotea hivyo! Kaangalie tena kumbukumbu! Tulikupeni dozi 2012.

Net imekata mkuu, leo anaweza kugonga hodi FFU Ukonga badala ya kwake.
 
Ni ule mwaka tuliowapiga tano kwa nunge mechi ya mwisho wa ligi. Je wakumbuka ni mwaka gani? Na baada ya hapo kwani nyie mmechukua ligi mara ngapi?

Amevurugwa huyo hajitambui kama yupo duniani au akhera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…