Habari wakuu,
Baada ya mwisho wa wiki hii kukosa burudani ya ligi kuu bara, uhondo umehamia Jumatano ya leo kwa viwanja kadhaa kuwaka moto. Mjini Mbeya, Mbeya city atamvaa kinara wa ligi, Simba SC. Yanga baada ya sakata la vurugu uwanjani watahamia uwanja wa Uhuru leo kuwakaribisha wakata miwa kutoka Turiani. Uwanja wa Kambarage, Stand united watawakaribisha wana-lambalamba kutoka Chamazi.
Tuwe sote pamoja kufatilia nani atalia na nani atacheka leo.
=========
Mbeya City Vs Simba
SUB 68, Ndemla ameingia kuchukua nafasi ya Ajib, Mohammed Ibrahim anaingia kuchukua nafasi ya Kichuya ambaye ameumia
Dk 63, Ame Ali anapoteza nafasi nzuri ya kufunga hapa na City wanaokoa
Dk 58, hatari kwenye lango la Simba, shuti kali linagonga mwamba na kuokolewa
SUB Dk 58, Ame Ali anaingia kuchukua nafasi ya Blagnon
Dk 55, Simba wanapata kona, inachongwa maridadi hapa na Kichuya lakini mwamuzi Mahagi anasema kipa City amefanyiwa madhambi
Dk 49, Raphael anapiga faulo inamgonga usoni Angban na mabeki wa Simba wanaokoa lakini yeye yuko chini anatibiwa
Dk 46, City ndiyo wanaanza kwa kasi wakishambulia lakini Lufunga anawahi na kuokoa ndani ya 18
MAPUMZIKO
-Mbeya City wanafanya shambulizi na kupata kona baada ya mpira kumbabatiza Bukungu lakini Angbani anadaka kwa ufundi wa juu kabisa
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, bado mambo yanakwenda si makali na katikati ndiyo kunaonekana kuwa na upinzani zaidi
Dk 38 hadi 42, mpira unaonekana kupooza, Simba ndiyo wanaoumiliki zaidi lakini wanacheza taratibu na Mbeya City wanaonekana kuingia kwenye mtego huo
Dk 36, Kichuya tena anapiga shuti kali lakini kipa anaokoa na kuwa kona, inachongwa wanaokoa, Bukungu anapiga tena, kona. Inachongwa tena, wanaokoa Mbeya City
GOOOOOOOOOO Dk 34, pasi safi kabisa ya Mkude, Kichuya anaingia vizuri kabisa na kufunga kwa ufundi kabisa
Dk 22, Kichuya anaingiza krosi nzuri sana, lakini Rajab Zahir anaokoa vizuri kabisa
Dk 18, mpira wa kona unachongwa vizuri kwenda kwenye lango la Simba lakini kipa Angban anaokoa vizuri kabisa lakini mwamuzi Mahagi anasema amechezewa faulo
Dk 14, Blagnon anakwenda vizuri hapa anapiga na anashindwa, kipa anaokoa hapa
Dk 13, PENAAAAAAAAT anaangushwa Blagnon
Dk 8, Simba wanaingia vizuri hapa lakini
GOOOOOOOL DK 6, Ajib anaifyungia Simba faulo moja safi kabisa nje ya 18 na kufunga bao safi
Dk 4, Kichuya anawachambua mabeki wa Mbeya inakuwa ni faulo hapa
Dk ya 1, Blagnon anapoteza nafasi nzuri kabisa hapa....
Yanga Vs Mtibwa
GOOOOOOOOO Dk 79, Mwashiuya anaingia vuzuri, anapiga krosi safi na Ngoma anamalizia vizuri kabisa na kuiandikia Ynaga bao la tatu
SUB Dk 75, Kelvin Friday anaingia kuchukua nafasi ya Chanongo upande wa Mtibwa
Dk 73, Juma Said Makapu anatoka na Mbuyu Twite anaingia kuchukua nafasi yake
GOOOOOOOOO Dk 68, Msuva anaifungia Yanga bao safi kwa shuti, mpira ukienda nyavu ndogo
Dk 64, Yanga wanaonekana kucharuka zaidi, Mtibwa wanalazimika kuwa makini kwa kuwa wana makosa mengi.
GOOOOOOOOOO Dk 63, Chanongo anafunga kali kabisa na kuandika bao safi kabisa kwa shutu kalii baada ya Mbonde kuwavuruga Yanga
Dk 58, Mtibwa wanaonekana kubadilika na kucheza kwa kushambulia zaidi. Hata hivyo wanaonekana kuwa na tatizo la umaliziaji
Dk 52, Yanga wanaendelea kushambulia kwa nguvu ingawa mashambulizi yao hayana 'macho'
DK 46, Mechi imeanza kwa kasi, bado Yanga wanaonekana kushambulia kwa kasi lakini Mtibwa wanaonekana wako vizuri zaidi katikati ya uwanja
=====
45+1' Chirwa anaingia wavuni kuiandikia Yanga goli la kwanza, Yanga 1-0 Mtibwa.
Dk 39 Yondani anapanda kusaidia mashambulizi, anatoa pasi nzuri kwa Juma Abdul lakini Mtibwa wanawahi ana kuokoa
Dk 35, bado inaonekana mambo si mazuri kwa pande zote, hakuna dalili za kupata bao na mpira unachezwa katikati zaidi
Dk 32, Simba wanaingiza krosi safi, hatari kabisa lakini mchezaji wa Mbeya City yuko chini, anatibiwa pale
Dk 29, Kamusoko anageuka na kupiga shuti kali lakini Tinocco anaokoa vizuri kabisa hapa
Dk 26, Juma Abdul anapiga krosi safi hapa, lakini Baba Ubaya ashika, faulo na inachongwa na Juma Abdul hapa, Dante anaruka na kupiga, anashindwa kulenga lango
Dk 24, Issa Rashid au Baba Ubaya anapigwa krosi safi hapa al manusura, lakini Dida anaokoa hapa
Dk 17, Juma Abdul anapiga shuti kali kabisa hapa, lakini linapita juu kidogo tu
16' Bado hakuna mashambulizi mazuri kutoka kila upande, mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi
13' Tambwe anaingia vizuri hapa, anapiga chenga mabeki wawili lakini anajichanganya mwenyewe
09' Yanga wanaonekana kumiliki mpira zaidi na wakicheza kwa kasi, lakini mara kadhaa Mtibwa Sugar wanajibu kupitia Jeba hasa sehemu ya kiungo
02' Chirwa anaingia vizuri na kufanya shambulizi kali lakini kipa anaokoa na mabeki wanaokoa
01' Juma Abdul anaingia na kupiga shuti kali, goal kick
Kwa hisani ya Saleh Jembe