Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Aprili 18, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 311- Ndanda 1 vs Yanga 1.
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kutokana na timu yake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 4, 2019 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Hilo ni kosa la nne msimu huu kwa timu ya Yanga kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo.
Nayo klabu ya Ndanda SC imetozwa faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na nusu) kwa kosa hilo hilo. Hilo ni kosa la kwanza msimu huu kwa timu ya Ndanda SC kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi. Adhabu dhidi ya Ndanda pia ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo.
Vilevile Yanga imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakirejea vyumbani baada ya mechi hiyo kumalizika. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 317- Tanzania Prisons FC 2 vs Mwadui FC
Mchezaji Laurian Mpalile wa Tanzania Prisons amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Mwadui FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 3, 2019 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mechi namba 200- Mbeya City FC 0 vs Azam FC.
Mchezaji Paul Peter wa Azam FC amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Mbeya City FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 14, 2019 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mechi namba 202- Yanga SC 3 vs Kagera Sugar FC
Mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2019 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Mechi namba 326- Singida United 2 vs Kagera Sugar FC
Meneja wa Kagera Sugar FC, Mohamed Hussein amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kutolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi katika mchezo huo uliofanyika Aprili 6, 2019 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Mechi namba 329- Mbao FC 0 vs Azam FC
Mchezaji Aggrey Morris wa Azam FC amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Mbao FC katika mechi hiyo ya Aprili7, 2019 iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji