Nasikia comments za watangazaji wa ITV baada ya habari za michezo hapa, na wanasema kuwa bao la Simba la dakika ya 86 walau limepunguza jazba ya mashabiki wa Simba ambao walikasirika kutokana na maamuzi mabaya dhidi yao. Mwamuzi Martin Sanya alitoa maamuzi makubwa matatu yenye kuiminya Simba; kukataa goli halali la Ibrahim Hajibu wa Simba, kukubali goli lisilo halali la Amis Tambwe wa Yanga na kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa Simba, Jonas Mkude.
My take:
Waamuzi tendeni haki ili msije mkawa mnaishi kwa wasiwasi kama ambavyo dondoo za watangazaji wa ITV walivyoongea