Ligi Kuu NBC kuendelea leo August 17, Simba kukipiga na Geita

Ligi Kuu NBC kuendelea leo August 17, Simba kukipiga na Geita

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ligi kuu ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Agosti 17, 2022 kwa mechi 4.

Simba SC watakuwa na nafasi ya kujiuliza kufuatia kipigo cha Ngao ya jamii wakichuana na Geita Gold katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 12:15 jioni.

Wagosi wa Kaya, Coastal Union watakuwa wenyeji wa vijana wa Kinondoni, KMC FC katika dimba la Sheikh Amri Abeid Arusha majira ya saa 10:00 jioni.

Majira ya saa 10:00 jioni Mbeya City wakuwa wageni wa Dododa Jiji katika dimba la CCM Liti Singida.

Mchezo wa mwisho leo utawakutanisha Wanalambalamba, Azam FC dhidi ya Wanankurukumbi, Kagera Sugar katika dimba la Azam Complex, Chamazi majira ya saa 2:15 usiku.

#KitengeSports
 
LEO NDYO WANAUME WANACHEZA A.K.A LAST BORN WA CAF [emoji881][emoji881][emoji881][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Timu inayojulikana caf na fifa
 
Breki hakuna ... Treni imefeli breki atakayekuwa mbele shauri Yake... NGUVU MOJA
 
Geita Gold, kama vipi kazeni tu. Maana hakuna namna nyingine. Mkikubali kufungwa kizembe shauri yenu wenyewe. Mimi simo.
 
Kocha afanye tena ujinga wake wa kumtoa namba 6 akasababisha tukapigwa
 
Back
Top Bottom