Ligi Kuu Tanzania Bara: Kagera Sugar yaitandika Simba kwa magoli 2-1

Naona mbute humu walifurahi magego yote nje 😑😑😑 Simba hapotezi tena afe mbwa afe panya πŸ’ͺ
 
Simba niya kawaida sawa.. timu iliyochukua ubingwa msimu uliopita imeongeza watu wapya kama:..
CHAMA
KAGERE
ZANA
Na ndio timu iliyofika robo CAF CL, Sikatai hatuna udhaifu.. tunao , swala la kuhonga marefa atakuwa analifanya Simba tu sababu ya MO??

Humu hatutaji majina ya watu...kumtaja huyo uliyemtaja siyo sahihi kabisa...ni kumuonea...ila bila kuwa na shilingi milioni mbili za marefa huwezi kushinda mechi...
 
wewe umepoteza game 4 ,mimi 2 . . hapo nani anateseka?
N wewe mwenye kikosi kipana uliejinasubu humu ndani kwamba hata ukipangiwa mechi interval kwa siku mbili mbili unatusua tu,
 
Humu hatutaji majina ya watu...kumtaja huyo uliyemtaja siyo sahihi kabisa...ni kumuonea...ila bila kuwa na shilingi milioni mbili za marefa huwezi kushinda mechi...
Bila shaka huo mtindo wa milioni za marefa uliwasaidia enzi za MALINZI na MANJI.
 
N wewe mwenye kikosi kipana uliejinasubu humu ndani kwamba hata ukipangiwa mechi interval kwa siku mbili mbili unatusua tu,
Kikosi kipo.. haina maana huwezi kupoteza mechi.
 
Timi inaonekana imekosa energy nadhani uchovu umechangia pia

Pasaka ishaharibika *****
Nnachokiona mimi kocha wa Kagera aliziangalia sana video za gemu za Simba ugenini kwenye champions league akagundua kuwa mkicheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka Simba hawakabi wanaangalia kwa macho tu. Kingine alijua Simba ulinzi ni koti tu limewekwa hasa upande wa Coulybaly, ndio siri ya ushindi.

Alliance nao wanaziweza sana pasi sijui kama tutaweza kuwazuia, tunacheza nalenale sana.
 
Hizo pasi walipiga taifa wakala 5... ngoja tuone Kirumba
 
Bila shaka huo mtindo wa milioni za marefa uliwasaidia enzi za MALINZI na MANJI.

Inawezekana kabisa...ila hapana shaka yoyote ile kwa sasa klabu ya Simba inatumia fedha kuhonga marefa na hata baadhi ya wwachezaji wa timu pinzani...binafsi sina shaka na hili
 
Inawezekana kabisa...ila hapana shaka yoyote ile kwa sasa klabu ya Simba inatumia fedha kuhonga marefa na hata baadhi ya wwachezaji wa timu pinzani...binafsi sina shaka na hili
Hata wanaoongoza ligi nina shaka nao
 
Kiporo tangu lini kikaliwa na juice ya miwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…