Ligi Kuu Tanzania Bara | Samora Stadium: Lipuli FC 1 - 3 Simba SC

Ligi Kuu Tanzania Bara | Samora Stadium: Lipuli FC 1 - 3 Simba SC

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
IMG-20190226-WA0002.jpg

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba SC, leo Februari 26, 2019 wanashuka dimbani wakiwa ni wageni kumenyana na Lipuli FC katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili msimu huu 2018/2019

Mchezo huo unapigwa katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa majira ya saa kumi za jioni
======

Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Lipuli FC: Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohamed Hussein, Yusuph Mlipili, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin,Clatous Chama, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi

Benchi la Simba: Deo Munishi, Asante Kwasi, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Adam Salamba

Kikosi cha Lipuli kitakachoanza; Yusuph Mohamed, William Gallas, Paul Ngalema, Ally Sonso, Haruna Shamte, Fred Tangulu, Seif Karihe, Jimmy Shoji, Paul Nonga, Daruwesh Saliboko na Steve Mganga

Benchi la Lipuli; Abdallah Makangana, Novalty Lufunga, Shaban Adda, Issa Rashid, Ibrahim Job, Keneth Masumbuko na Mussa Nampaka

UPDATES:

FT: Lipuli FC 1 - 3 Simba SC

>>> Ni patashika katika dimba la Samora mjini Iringa, Simba wanaanza na bao likifungwa na Clatous Chama dakika ya 6.

>>> Lipuli FC wanasawazisha dakika ya 18 kupitia kwa Paul Nonga.

>>> Ni yule yule Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama anaingia tena kimiani na kuipatia Simba goli la 2 mnamo dakika ya 44

IMG_20190226_174854.png


>>> Meddie Kagere anaifungia Simba bao la tatu dakika ya 58.

IMG_20190226_182421.png
 
Kadiri ligi inavyokata mbuga.., ndivyo ambavyo hamasa inazidi kupunguza kwa wanajangwani,juzi taifa walijitokeza kiduuchu. Leo msituanģshe tuwe pamoja dk hizi 90.Na kwa ushauri tu bidiii ielekezwe FA huku TPL ndo basi tena...Lipuli analala mapema
 
Back
Top Bottom