Ligi Kuu Tanzania, Bara: Singida United 0 - 0 Yanga SC

Kizibo255

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2011
Posts
515
Reaction score
376
Mchezo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Namfua Singida
Twende pamoja
...........
IMG_20190206_183559.jpg

IMG_20190206_183616.jpg

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Singida United dhidi ya Yanga kwa sasa ikiwa ni mzunguko wa pili Uwanja wa Namfua, Singida umekamilika kwa suluhu ya bila kufungana.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuona namna mwendelezo wa Ligi unavyoshika kasi kwa sasa.

Kipindi cha kwanza mchezaji wa Singida United Boniphace Maganga alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumzibia njia mlinda mlango Ramadhan Kabwili.

Hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mpinzani mpaka sasa ikiwa ni kipindi cha pili kwa sasa, timu zote zinapambana kutafuta matokeo.

Kipindi cha pili dakika ya 55 Feisal Salum alionyeshwa kadi ya njano baada ya kucheza rafu, pia nahodha wa Singida United. Kenedy Juma alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 64.

Matheo Anthon alifanyiwa mabadiliko dakika ya 59 nafasi yake ikachukuliwa na Pius Buswita.

Nahodha Ibrahim Ajibu anaingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Feisal Salum, mpira wake wa kwanza ni faulo ambayo ameipasiha mawinguni.

Athanas Adam wa Singida United alifanyiwa mabadiliko dakika ya 64 nafasi yake ikachukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

Dakika ya 83 Habib Kiyombo alitoka nafasi yake ikachukuliwa na Frank Mkumbo.

Mvua ilianza kunyesha uwanja wa Namfua dakika ya 86 ya mchezo.

Heritier Makambo mshambuliaji kinara wa mabao Ligi Kuu Bara alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.
 
Azam kwenye mobile app yao wametoa channel ya azam sports iliokuwa inaonyesha ligi ya Tz
 
Ila viwanja vya mikoani vilivyobaki changamoto in namfua, sokoine , ule wa ndanda nangwanda,mkwakwani na karume musoma ...vingine walau vinachezeka kwa ustadi
 
Kikosi cha Yanga Kinachoanza Leo -:
1. Ramadhani Kabwili
2. Paul Godfrey
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Abdallah Haji
6. Feisal Salum
7. Deusi Kaseke
8. Thabani Kamusoko
9. Heritier Makambo
10. Matheo Anthony
11. Gustafa Simon
AKIBA -: Kindoki, Buswita, Juma Abdul , Tshishimbi, Andrew Vicent, Said Juma, Ajibu.

Mechi imemalizika kwa timu zote kushindwa kufungana.
Full Time : Singida United 0 - 0 Yanga
====

Back
Top Bottom