Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Baada ushindi wa goli 3-0 wa Yanga SC dhidi ya klabu ya Coastal Union katika mchezo wao wa mwisho uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 30, 2020, leo vijana wa Jangwani watakipiga na Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani
Kuelekea mchezo huo takwimu zinaibeba Coastal union maarufu Wagosi wa Kaya kwasababu Yanga hajashinda Mkwakwani kwa takribani misimu mitatu. Na kwa upande wa Coastal haijawahi kupoteza Mkwakwani tangu ligi kuanza
Yanga itawakosa wachezaji wake watano kutokana na sababu mbalimbali wakiwemo Saido Ntibazonkiza Mapinduzi Balama na Ramadhan Kabwili, ambao ni majeruhi,
Huku Carlos Carlinhos akiwa anatumikia kadi nyekundu aliyopata katika mchezo uliopita wa FA dhidi ya Ken Gold, huku beki Dickson Job akiwa na ruhusa maalumu.
Hata hivyo, Kaze atakuwa akitabasamu baada ya kurejea kwa mshambuliaji wake, Yacouba Sogne aliyekuwa majeruhi na hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao manne kwenye ligi.
Michezo mingine itakayopigwa hii leo ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Biashara United, Polisi Tanzania dhidi ya KMC huku Tanzania Prisons ikipimana ubavu na vijana wa nyumbani Mbeya City