Ligi Kuu ya Tanzania kutumia mfumo wa 'Video Support' (VS) badala ya VAR msimu ujao

Ligi Kuu ya Tanzania kutumia mfumo wa 'Video Support' (VS) badala ya VAR msimu ujao

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amethibitisha kuwa Mfumo wa Video Support (VS) unatarajiwa kuanza kutumika katika Ligi Kuu ya Tanzania msimu ujao.

1783931585946.png

Tanzania inatarajiwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutumia mfumo huu wa Video Support (VS), ambao ni teknolojia rahisi zaidi ya mapitio ya video iliyoundwa kusaidia waamuzi kufanya maamuzi sahihi zaidi wakati wa mechi.

Soma: Karia: Video Support ni nafuu kuliko VAR na ni rahisi kutoa mafunzo kwa waamuzi

Video Support ni nini?
  • Mapitio ya Matukio: Inamruhusu mwamuzi kupitia matukio muhimu kwenye skrini ya video kabla ya kutoa maamuzi ya mwisho.
  • Tofauti na VAR: Tofauti na mfumo wa VAR, hapa hakuna timu ya maafisa wa video wanaokagua kila tukio mfululizo. Mwamuzi ndiye anayeamua muda gani akague marudio ya picha (footage).
  • Urahisi na Gharama: Ni mfumo rahisi na wa gharama nafuu zaidi ukilinganishwa na VAR.
Namna Mfumo wa Video Support unavyoweza kusaidia wakati wa mechi:
  • Kukagua magoli na uwezekano wa madhambi kabla hayajakubaliwa.
  • Kuangalia matukio ya penati ndani ya kisanduku (box).
  • Kuthibitisha makosa makubwa yanayostahili kadi nyekundu au pale mwamuzi anapompa kadi mchezaji asiyehusika (mistaken identity).
  • Kupunguza makosa ya wazi ya uamuzi katika nyakati muhimu za mchezo.
  • Kuwapa waamuzi kujiamini zaidi kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.
 
Zitumike hasa kwenye Mechi za Simba na Yanga:
Timu ndogo zinaonewa sana na hizi timu na Marefa wapenzi wa hizi timu:

Pia Marefa wapenzi wa hizi timu wanazibeba sana timu zao na kuzikandamiza timu pinzani kwenye ubingwa kama Arachuga:
 
Je kwenda kutazama video ni lazima au hiyali ya mwamuz maana ata uko dunian bado kuna utata mwamuz anaweza akagoma kwenda kutazama tukio na uamuz wake ukasimama kama ulivyo
 
Na ili ifanye kazi vizuri refa ambae hatatoa maamuzi sahihi baada ya kuangalia VS afutwe kabisa urefa. Maana marefa wengine sio kwamba wanakuwa hawaoni matukio vizuri bali wako corrupt na wana ushabiki wa kijinga.
 
Back
Top Bottom