mpira wa afrika ni mgumu wachezaji wanakaba sana kiasi cha wapinzani kushindwa kufunga, halafu wakati huo huo hakuna timu yoyote iliyowahi kufanya makubwa kwenye kombe la dunia. Tunazidiwa hata na Asia wanaocheza soka la kufunguka wamewahi kufikisha timu nusu fainali.
Kiufupi soka la afrika bado ni la ovyo sana, tunacheza mpira wa kunyang'ana nyang'ana sana haukai miguuni na hata kufanya build up ya magoli hatujui ndio maana magoli mengi yanafungwa kutokana na mistakes za wapinzani na sio uwezo halisi wa kupika goli kwa timu husika.
Afrika soka letu bado ndio maana hata wachezaji wetu tunao waona wakifanya vizuri nje ya afrika wakija huku kucheza pamoja na wenzao wanaonekana hawajui tu sababu wanacheza ndani ya set up mbovu.