Ligi VPL kurejea hivi karibuni

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Kwa kauli niliyomsikia Rais wetu Dr. John Magufuli, dalili zote ligi kuu VPL itarejea hivi karibuni, amesema bado anapata ushauri wa wataalam wake, lakini angependa ligi irejee mapema kwani michezo ni afya, na ndio maana wanamichezo wengi hawapatwi na maradhi. Amesema angependa watu waione kwenye televisheni, hivyo uwezekano wa ligi kurejea bila watazamaji ni mkubwa.

Hii itaipa nafasi Simba kuhalalisha ubingwa wake, kwani sioni uwezekano wa timu yoyote kuipita Simba, na vile vile itakamilisha safari ya Singida United kushuka daraja, na Gwambina kupanda daraja.
 
Gate collection ndio tegemeo la vilabu hivyo ligi haiwezi endelea
Mjomba we bila shaka unaangalia tu mechi za kweny tv na nnamashaka na uelewa wako wa ligi kuu siku moja moja kaangalie mechi za viwanja vya mikoani ndo uje utuambie maswala ya gate collection

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja tuendelee kutekeleza mawazo ya mtu mmoja bila kuchanganya na zetu.

Kama hujapata mtu au ndugu yako aliyeugua,aliyekufa na ukahudhulia yale mazishi ya usiku lazima utakuwa unashangilia sana.......

Corona ipo........
 
Gate collection ndio tegemeo la vilabu hivyo ligi haiwezi endelea
Itabidi vijipange tu, hata hivyo ukweli ni kwamba ukiondoa mechi zinazochezwa na Simba pamoja na Yanga, mapato ya mechi nyingine ni finyu sana hayatoshi hata asilimia 5% kugharimia timu, hivyo kucheza bila washabiki halina impact kubwa kwenye kugharimia timu, ila linaweza kuwa na impact kubwa kwenye msisimko wa mechi za simba na Yanga, pamoja na wadhamini wa ligi na vilabu. Itapunguza kodi ya serikali kutokana na viingilio, italeta madhara makubwa kwa TFF, bodi ya ligi na wamiliki wa viwanja, lakini vile vile itaongeza mapato kwa serikali kupitia betting.
 
Gate collection ndio tegemeo la vilabu hivyo ligi haiwezi endelea
Wewe kuna mechi imewahi kuingiza mashabiki 9, sasa wasije kusingizia mapato

"Not everything is for everybody"
 
Rais Magufuli amesema anafikiria kurudisha michezo ya ligi kuu iendelee

Mzee baba umesahau na shule,fungueni shule watoto warudi shule Tanzania haina corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wanafunzi warudi shule Kama Ni hivo
 
Kwa sababu kina dyabala ni wacheza mieleka ndo mana

Its not over until its over...[emoji769]
 
Wamililk wa viwanja???

Viwanja vyote n vya CCM
Wanahasara gani kama
Mwenyekiti wao ndo karuhusu??

stidy
 
Ngoja tuendelee kutekeleza mawazo ya mtu mmoja bila kuchanganya na zetu.

Kama hujapata mtu au ndugu yako aliyeugua,aliyekufa na ukahudhulia yale mazishi ya usiku lazima utakuwa unashangilia sana.......

Corona ipo........
Ndugu waliougua corona na wakapona ni wengi tu wengine tumewafanyia bethdei hapo hapo amana pia kumbuka hata kabla ya corona watu tulipata misiba na Maisha yaliendelea so ligi pia itaendelea sawa
 
Ndugu waliougua corona na wakapona ni wengi tu wengine tumewafanyia bethdei hapo hapo amana pia kumbuka hata kabla ya corona watu tulipata misiba na Maisha yaliendelea so ligi pia itaendelea sawa
Hakuna anayetaka Bingwa wa mezani,na misiba haiwezi kuisha corona ikiondoka,ila si busara kuwa na misiba ambayo inaepukika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…