HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Kwa kauli niliyomsikia Rais wetu Dr. John Magufuli, dalili zote ligi kuu VPL itarejea hivi karibuni, amesema bado anapata ushauri wa wataalam wake, lakini angependa ligi irejee mapema kwani michezo ni afya, na ndio maana wanamichezo wengi hawapatwi na maradhi. Amesema angependa watu waione kwenye televisheni, hivyo uwezekano wa ligi kurejea bila watazamaji ni mkubwa.
Hii itaipa nafasi Simba kuhalalisha ubingwa wake, kwani sioni uwezekano wa timu yoyote kuipita Simba, na vile vile itakamilisha safari ya Singida United kushuka daraja, na Gwambina kupanda daraja.
Hii itaipa nafasi Simba kuhalalisha ubingwa wake, kwani sioni uwezekano wa timu yoyote kuipita Simba, na vile vile itakamilisha safari ya Singida United kushuka daraja, na Gwambina kupanda daraja.