Ligi ya Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 2 - 1 AS Club Vita | Simba yafuzu kucheza hatua ya mtoano 2019

Dah! Kiukweli munatia huruma sana


Ni kweli ...uko sahihi...lakini hiki ni kipindi cha mpito...kwani wewe unadhani itapita miaka mitatu bila kibao kugeuka?? itafika muda Yanga itaifunga Simba....Mwaka 1981 Yanga iliifunga Simba baada ya kugaragazwa kwa karibu miaka mitano kikiwemo kipigo cha goli 6-0 cha mwaka 1977 kilichotokana na Yanga kufukuza wachezaji karibu wote 25 na kuamua kuanza upya...goli la Yanga la 1981 lilifungwa na Juma Mkambi kwa kona ya Amasha...kabla ya hapo Simba nayo ilikuwa na kipindi kigumu kuanzia mwaka 1968 hadi mwaka 1973 pale ilipojikomboa kwa goli la Willy Mwaijibe...Yanga kwa sasa inajijenga upya...haina kikosi kizuri sana...inashinda mechi zake kutokana na wachezaji kupigwa saikolojia na Zahera na nguvu za wanachama na hasa mikoani...Simba ina kikosi kizuri kwa sasa chenye wachezaji karibu wanane wa kigeni kwenye kikosi cha kwanza..Yanga ya Manji nayo ilikuwa hivyo hivyio lakini kwa waelewa ilikuwa ni wazi kuwa Manji akiondoka Yanga itakuwa kwenye kipindi kigumu ..na hicho ndicho kilichotokea..Ila kwa bahati nzuri Yanga haijasambaratika, bado iko vizuri na kuwashangaza wale wote wasioitakia mema klabu hii..kwa hiyo Yanga itakuja na nguvu mpya muda siyo mrefu ujao...
 
Mzee wetu aliwatakia kila la kheri. Sasa lazima atawaita Ikulu. Baba hoyeee
 
Hahaaa.....!!dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante Mtani. Kuhama timu sisi kina YANGA lialia ni ngumu mno Mtani kama Ngamia kupita kwenye tundu la Sindano. Hivyo nakomaa na Yanga yangu tu mpaka mwisho.

Nauliza tu jana ulipata usingizi kweli Mtani?
Mkome kabisa kushabikia timu za nje,harusi si zenu mnaenda na sahani za udongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyinyi mikia bila tunguli msingetoka mshukuru mganga wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni mganga hata Yanga wangeweza kuchangishana. Niyonzima aliona kuwa ili afanikiwe ni bora aje Simba, namsikitikia dogo Ajib, wenzake wanaenda kufanya majaribio Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea kisoka, yeye anakimbilia bwawani. Naamini msimu ujao atarudi Msimbazi.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…