Ligi ya Mabingwa Afrika 2019/20 Simba SC dhidi ya UD do Songo, Yanga SC dhidi ya Township Rollers

Ligi ya Mabingwa Afrika 2019/20 Simba SC dhidi ya UD do Songo, Yanga SC dhidi ya Township Rollers

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), leo Jumapili Julai 21, 2019 limetoa ratiba ya awali ya michezo ya ligi ya mabingwa wa Afrika CAFCL msimu ujao 2019/2020 ambapo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo Simba na Yanga wamepangwa kuanza na timu kutoka ukanda wa COSAFA (kusini mwa Afrika).

Mabingwa wa Tanzania Simba SC, wamepangwa kuanza na UD do Songo ya Msumbiji na wataanza ugenini huku Yanga SC, walioshika nafasi ya pili msimu uliopita kwenye ligi kuu Tanzania wakipangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana.

Kwa mijibu wa ratiba mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Agosti 9, 10, na 11 huku mechi za marudiano zikipigwa kati ya Agosti 23, 24, na 25.

Endapo Simba SC na Yanga SC wanafanikiwa kupenya kwenye hatua hiyo, wataingia kwenye raundi ya pili ambapo Simba SC, inakutana na mshindi kati ya Nyasa Big Bullets ya Malawi dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe huku Yanga SC ikikutana na Green Mamba ya Eswatini dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Mechi za raundi ya pili zitapigwa kati ya Septemba 13, 14 na 15 na marudiano itakuwa kati ya Septemba 27, 28, na 29.

IMG_20190721_194005_117.jpeg
 
Msimu ulipita Yanga walipigiwa mpira mwingi sana, pasi na hapa na pale hadi golini na Township Rollers...Safari hii huenda wakaomba mechi yao ibadilishwe..!
Acha uongo. Game ya Taifa iliisha 0-0
 
Hapo timu ya wananchi tutajiandaa dhidi ya hao Zesco tu! Walau timu za kutoka Zambia huwa zinatusumbua kiasi chake. Ila siyo hao makhirikhiri wa Botswana.

Awamu hii hawatapata mteremko kama mwaka ule timu ilipoanza kuyumba kiuchumi na hivyo kuathiri wachezaji.
 
Back
Top Bottom