*MPIRA SHIKAMOO*[emoji460][emoji460][emoji460]
Mpira hauna adabu, mpira hauna mwenyewe,mpira unauma, mpira shikamoo.
Poleni wana Simba wenzangu huu ndio mpira asikwambie mtu hakuna timu ya mpira yeyote duniani ambayo haijawahi kupitia machungu tunayoyapitia sasa.
Mpira hauna mwenyewe maana leo wewe kesho yule cha muhimu ni kukubali yale matokeo matatu ya mpira *KUSHINDA,KUFUNGWA, DROO* ingawa hilo neno la katikati huwa gumu kulizoea.
Simba Nguvu Moja mwakani tutakuja na nguvu kubwa sababu uwanja wetu tutakuwa tumekamilisha na mambo mengi mapya ya muhimu na mazuri yatakuwa yamefanyika cha muhimu tusonge mbele.
Ninayo imani kubwa sana na usajili huu uliofanywa msimu huu pamoja na kutolewa mapema kwenye mashindano. Sababu kubwa na iliyotugharimu ni kuwa CAF msimu huu walibadilisha ratiba ya michuano hii na mbaya zaidi imetukuta ndio tumetoka kwenye pre season na hata ligi hatujaanza hata mechi moja na hata Mwalimu bado hajawa na ile first eleven anayiiamini hii imechangia pia sisi kutolewa mapema.
Msimu uliopita tulianza michuano hii wakati tayari tumecheza michezo 9 ya ligi kuu tayari wachezaji walikuwa wameshapata muunganiko tayari kocha alikuwa na uhakika na first eleven yake ndio maana tulifanya vizuri. But huu mwaka ni tofauti imetukuta bado timu haijakaa sawa na UD Songo wenyewe wapo kwenye ligi tayari wanaendelea hiyo imewasaidia hata tulivyowaona wachezaji wao wanao muunganiko mzuri katika uchezaji wao wa mpira sababu tayari wamezoeana tofauti na timu yetu.
Hatuna wa kumlaumu kilichotokea ni kinawatokea timu nyingi duniani Bahati haikuwa kwetu maana mliona wenyewe namna wachezaji wakivijitoa japo makosa madogo madogo ya kibinadamu yalikuwepo na hayawezi kukosekana ninachilaumu ni michuano hii ya cuf kuanza mapema sana huku timu ikiwa bado haina muungamiko mzuri maana hata ligi yetu haijaanza wala hautacheza mechi ya ligi hata 1.
Lakini pia watu mkumbe kuwa hatujafungwa tumetoka 1-1 kilichotutoa ni faida ya wao kupata goli la ugenini tu ila ninachokijua ni kuwa timu tuliyonayo ni nzuri sana na kudhibitisha hilo wacha ligi ianze tutakumbushana hapa yale niliyoyasema.
Ndio kwanza kazi imeanza.... *ALUTA CONTINUAR*
By Simba fans kindakindaki.
[emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460][emoji460]