Ligi ya Tanzania yapanda nafasi (9) imekuwa ya 62 duniani kwa ubora

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Shirikisho la kimataifa la historia na takwimu duniani (IFFHS) limetangaza orodha ya ligi kuu bora duniani kwa mwaka 2021

Ambapo Tanzania imepanda kwa nafasi 9 kwa mwaka 2020 ambapo ilishika nafasi ya 71 na imepanda hadi nafasi ya 61 kwa ubora duniani

Kwa Africa Tanzania imeshika nafasi ya 10 na kuwa ligi pekee Bora kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati

Pongezi kwa TFF kuendelea kutupeleka nchi ya ahadi ya kisoka

Maendeleo hayana chama

 
Ligi ya bongo imekua sana hasa tukianzia uwekezaji pia pongezi nyingi nazani wanastahili Azam TV kwa kurusha live mechi za ligi hii imeipaisha sana ligi yetu pia mishahara ni mitamu kwa wachezaji thus y hata wachezaji wa madaraja ya juu kutoka nje ya tz wanacheza timu za kawaida au daraja la kwanza..

Changamoto nazoziona kwenye ligi yetu ni tatu ambazo tukizipunguza kama sio kuzimaliza zitatuboost ni hizi.

1. Viwanja.. Inabidi tuweke nyasi yaani pitch iwe nzuri hapo sasa tutakua tumepiga hatua moja matata sana.

2. TTF bado ni kikwanzo kwenye kubadili idadi ya timu zinazoshiriki ligi ovyo ovyo mara Leo kuna timu 20 kesho 18 mara sahivi 16 hii inaipunguzia "image" nzuri ligi yetu.

3. Waamuzi hapa ndo pabaya zaidi japo improvement ipo ila bado inatakiwa tuboreshe zaidi.

All in all utani wa jadi wa Simba na Yanga unazidi kuifanya ligi yetu ifatiliwe sana japo natamani ipatikane timu nyingine ambayo italeta challenge sijajua Azam fc wanakwama wapi...
 
Umeongea fact Sana mkuu, binafsi natamani hata TFF wangetengeneza hata tuzo ya heshima kwa Azam ......coz Hawa jamaa wameleta mageuz makubwa Sana kwenye soka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…